Monday, October 31, 2016

Mtihani kidato cha nne umeanza leo

bonzuma Meadia Group  imetembelea shule mbalimbali wilayani wa Makete nakuona wanafunzi wakiwa katika vyombo vya mtihani

Pitia hii

Picha ya Muimbaji wa nyimbo za injiri na mzarishaji wa nyimbo mbalimbali Godluck Gozbet amepata jiko maana yake ameoa

Sakata Polisi aliyepiga picha na Lipumba la chukua sura mpya

Kitendo cha askari polisi kumpigia saluti
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi
(CUF) anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili
wa vyama vya siasa, Profesa Ibrahim
Lipumba imezua gumzo la kuhoji uhalali
wake.
Askari huyo alionekana juzi akimpigia
saluti Profesa Lipumba katika eneo la
Buguruni ambapo mwanasiasa huyo
alienda kushiriki zoezi la usafi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Salum
Hamduni alipoulizwa kuhusu usahihi wa
askari polisi kuwapigia saluti viongozi
wa vyama vya siasa wasio wabunge
alijibu kwa ufupi, “sio sawa.”
Kwa mujibu wa Kanuni za Jeshi la Polisi
(PGO) namba 102, haiwataji viongozi wa
vyama vya siasa wasio wabunge kati ya
watu wanaopaswa kupewa salamu hiyo
ya jeshi yenye kuonesha heshima.
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani wa Serikali ya Awamu ya Tatu,
Kapteni John Chiligati aliwahi kueleza
Bungeni kuwa saluti ni ishara ya
kuonesha heshima kwa kiongozi mkuu
kwenye asasi za kijeshi.
Kapteni Chiligati alisema kuwa mbali na
viongozi wa kijeshi, viongozi wengine
wanaopaswa kupewa saluti ni wa
mihimili ya Serikali, Bunge na
Mahakama.
Wengine ni majaji wote, wabunge,
wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na
mahakimu wa mikoa na wilaya wakiwa
kwenye mahakama zao.
Katibu Mkuu wa Chama Cha CCK,
Renatus Muabhi alisema kuwa huenda
askari huyo alipiga saluti kwa kupaniki
kutokana na maagizo aliyopewa ya
kumlinda Profesa Lipumba katika zoezi
hilo.

Taarifa kamili ya kifo cha mashali

Bondia mahiri na machachari ulingoni,
Thomas Mashalli, almaarufu 'Simba
asiyefugika', amefariki dunia usiku wa
kuamkia leo huko maeneo ya Kimara baada
ya kupigwa na watu wasiojulikana.
Imeelezwa kuwa bondia huyo alifika maeneo
ya Kimara katika moja ya baa na kuanza
kunywa bia na baadaye ukazuka ugomvi
baina yake na kijana mmoja aliyekuwa
maeneo hayo jambo lililofamfanya bondia
huyo kumwadhibu kijana huyo kwa kumchapa
mangumi.
Baada ya ugomvi huo, imeelezwa kuwa
kijana huyo alianza kupiga kelele huku
akimuitia mwizi bondia huyo, jambo
lililowafanya watu wasioujua ukweli wa tukio
hilo kufika eneo hilo na kuanza
kumshambulia bondia huyo kwa silaha
mbalimbali zikiwemo mapanga.
Baada ya watu hao kumjeruhi imeelezwa
kuwa waliamua kumburuza hadi barabarani
na kumtupa na kisha kumwacha akiugulia
maumivu.
Akizungumza na promoter
Kaike Siraju, amethibitisha kufariki kwa
bondia huyo aliyekuwa apande uliongoni
mwezi ujao huko mjini Morogoro.
bongohotz.com
Msiba wa bondia huyo upo maeneo ya
Tandale nyumbani kwa wazazi wake.
Bwana alitoa na bwa

Sunday, October 30, 2016

Breaking news

Bondia Thomasi mashari afariki Dunia jiji dar es Salaam

Wanafunzi wapingwa na radi Mang'oto sekondari


Kutoka kwa Mwl Mgaya Mang'oto sekondari

Wanafunzi kumi wa Mang'oto Sekondari wamepigwa na RADI leo saa 07:30 mchana, wakati wamefoleni kupata chakula cha mchana. Nao ni Bruno Ilomo wa Usungilo, Ageth Tave wa Utweve, Manfred Mwageni wa Uwemba, Hasani Idawa wa Ilindiwe, Basili Mbilinyi wa Usungilo hawa wametibiwa na kurudi shuleni. Fainess Sanga wa Utweve, Atuganile Mbilinyi wa Usungilo, Frida Chengula wa Usungilo, Himidi Chengula wa Usungilo na Isaya Choza Sanga wa Makete Mjini wamelazwa Ikonda Hospitali. Huyu wa mwisho ameunguzwa zaidi upande wa kulia toka begani hadi mapajani. Tuwaombee wapone haraka. Amen!

Burudani Kutoka Bonzuma Meadia Group

https://www.spreaker.com:443/episode/9759471

TAARIFA KWA UMMA KUHUSIANA NA UPOTOSHAJI WA TAARIFA ZINAZOSAMBAZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII JUU YA MSHINDI WA SHINDANO LA MISS TANZANIA 2016

Hivi karibuni kumeibuka upotoshaji
mkubwa kutoka kwa baadhi ya watu
wenye nia ovu ya kutaka kuharibu taswira
nzima ya Mshindi wa shindano la Miss
Tanzania 2016,aliyevishwa taji hilo jana
usiku ndani ya jiji la Mwanza,taarifa hizo
ambazo zimekuwa zikisambazwa katika
mitandao ya kijamii zikieleza upotoshaji
wa taarifa mbalimbali za mlimbwende
huyo zikiwemo na elimu yake.
SEHEMU YA TAARIFA ILIYOKUWA
IKIPOTOSHWA KATIKA MITANDAO
MBALIMBALI YA KIJAMII HII HAPA CHINI;
MISS TANZANIA 2016
🙊🙊🙊🙊🙊🙊
JINA:Diana Edward Lukumai
UMRI:Miaka 18
ELIMU:Shahada(degree)
Hii ina maana;
Alianza Chuo akiwa na miaka 15
Alianza Form one akiwa na miaka 9
😂😂😂😂😂😂
Ingawa sio mshabik wa haya mambo
napenda nchukue hii nafasi kuwapongeza
Wazazi wote kama wazazi wa Diana
ambao watoto wao wameanza shule ya
msingi wakiwa na miaka miwili
HII NDIO TAARIFA SAHIHI YA MSHINDI
WA SHINDANO LA MISS TANZANIA
2016,DIANA EDWARD LOY.
Napenda kuujulisha Umma yafuatayo;
1. Miss Tanzania 2016/2017 aliyeshinda taji
jana jijini Mwanza, anaitwa Diana Edward
Loy na siyo Diana Lukumai kama
inavyotajwa mitandaoni.
2. Mlimbwende huyo amemaliza kidato cha
nne 2015 Shule ya Sekondari Arusha Day
na si 2011 kama inavyotajwa mitandaoni
kwa malengo ovu.
3. Diana hajawahi kujiunga na Elimu ya
Chuo Kikuu chochote Tanzania au duniani
bali anatarajia kujiunga mwaka huu
katika chuo cha IFM kusomea masula ya
kodi ngazi ya stashahada (cheti) ingawa
kulingana na ratiba zake na majukumu
yake mapya ikiwemo kushiriki Miss world
mapya huenda akaahirisha mwaka wake
wa masomo.
4. Tunawasihi watanzania kutumia vyema
mitandao ya kijamii na si kufanya
"Character assassination" lakini pia
tunaheshimu haki yao ya msingi ya kuhoji
masuala ya msingi kabisa kuhusu mtu
ambaye ni Public figure na ataliwakilisha
taifa katika anga za kimataifa.
Tumuunge mkono mlimbwende wetu ili
atuletee Taji la Dunia.
Ahsanteni.
Charles William
Kaimu Ofisa Habari wake.
(wilflow101@gmail.com)

Friday, October 28, 2016

watakao sababisha ajari kukiona

Na Riziki Manfred makambako

Mkuu wa Mkoa wa njombe Rehema Nchimbi
amewataka madereva kufuata sheria barabarani
na kutoendeswa na askari wa usalama
barabarani
Akihutubia wakazi wa mji wa makambako Katika
maadhimisho ya kilele cha wiki ya usalama
barabarani ambayo kimkoa yamefanyika katika
mji wa makambako Nchimbi amesema
kumekuwa na tabia ya madereva kuonyeshana
alama za kujulisha mahara askari wa usalama
barabarani wamesema hivyo kuendelea
kuongeza ajari za barabarani ambazo zinaweza
kupungua au kuisha kabisa "najua madereva
wengi wanawaogopa askari wa usalama
barabarani hivyo wanafuta alama za barabarani
eneo ambalo Kuna askari wa usalama
barabarani nje ya hapo hawafuati hivyo kufanya
imani ya ajali kuongeza
Awali akisoma Risala Mkuu wa usalama
barabarani Mkoa wa njombe Kelvin Ndimbo
amesema kuwa ajali za barabarani zimepungua
katika mkoa wa njombe japo kwa mwaka 2016
kwa asilia 20 huku akizitaja sababu kubwa
kuwa ni elevi wa kulindukia mwendo kasi ubovu
wa vyombo vya usafiri na barabara
pia Ndimbo amesema jeshi la polisi kupitia
askari wa usalama barabarani wamejipanga
kuhakikisha wanaendelea kusimamia sheria kwa
kuwachukulia hatua kali madereva
wanaosabisha ajari
Katika maadhimisho hayo yaliyohudhuliwa na
wanafunzi wa shule mbalimbali ambao
wameuomba uongozi wa TANLODS Mkoa
kuwawekea alama za pundamilia (zebra crros)
katika eneo la barabara kuu ya Makambako
Songea eneo la ghorofa la Japipo

Breaking news

Check out @BBCBreaking's Tweet: https://twitter.com/BBCBreaking/status/792052432033484800?s=09

watakao sababisha ajari kukiona

Na Riziki Manfred makambako 

Mkuu wa Mkoa wa njombe Rehema Nchimbi amewataka madereva kufuata sheria barabarani na kutoendeswa na askari wa usalama barabarani 
Akihutubia wakazi wa mji wa makambako Katika maadhimisho ya kilele cha wiki  ya usalama barabarani ambayo kimkoa yamefanyika katika mji wa makambako Nchimbi amesema kumekuwa na tabia ya madereva kuonyeshana alama za kujulisha mahara askari wa usalama barabarani wamesema hivyo kuendelea kuongeza ajari za barabarani ambazo zinaweza kupungua au kuisha kabisa "najua madereva wengi wanawaogopa askari wa usalama barabarani hivyo wanafuta alama za barabarani eneo ambalo Kuna askari wa usalama barabarani nje ya hapo hawafuati hivyo kufanya imani ya ajali kuongeza 
Awali akisoma Risala Mkuu wa usalama barabarani Mkoa wa njombe Kelvin Ndimbo amesema kuwa ajali za barabarani zimepungua katika mkoa wa njombe japo kwa mwaka 2016 kwa asilia 20 huku akizitaja sababu  kubwa kuwa ni elevi  wa kulindukia mwendo kasi ubovu wa vyombo vya usafiri na barabara 
pia Ndimbo amesema jeshi la polisi kupitia askari wa usalama barabarani wamejipanga kuhakikisha wanaendelea kusimamia sheria kwa kuwachukulia hatua kali madereva  wanaosabisha ajari 
Katika maadhimisho hayo yaliyohudhuliwa na wanafunzi wa shule mbalimbali ambao wameuomba uongozi wa TANLODS Mkoa kuwawekea alama za pundamilia (zebra crros) katika eneo la barabara kuu ya Makambako Songea eneo la ghorofa la Japipo 

     

   

Picha mbalimbali za maadhimisho ya kilele cha siku ya usalama barabarani makambako

1.mkuu wa usalama barabarani Mkoa wa njombe  Kelvin Ndimbo Akisoma Risala ya kilele cha siku ya usalama barabarani mkoani njombe yaliofanyika katika mji wa makambako
2.msafala wa bodaboda wakielekea viwanja vya polisi yaliofanyika maadhimisho ya kilele cha siku ya usalama barabarani
3.mkuu wa Mkoa wa njombe Rehema Nchimbi akihutubia hadhara katika  kilele Cha wiki yanenda kwa usalama  mkoani

Plujim arejea Yanga tena

Hatimaye Uongozi Wa Yanga Umekataa Maombi Ya Kocha Wa Timu Hiyo Hans Van Plujim Kujihuzuru na Hivyo Amerejea Kuendelea na Kibarua Chake ,  Waziri Wa Mambo Ya Ndani  Mwigulu Nchemba Ni Miongoni Mwa Walio Saidia Kulimaliza  Sakata hilo na Kocha George Lwandamina Atakuwa Mkurugenzi wa Ufundi Klabuni Hapo.

Thursday, October 27, 2016

Mvua kubwa zaanza Makete

Mvua zilizonyesha katika maeneo mengi wilaya Makete licha ya mamlaka ya Hali ya hewa kutangaza Kutokuwa na mvua za uhakika mwanzoni mwa mwaka huu

Hakuna ripoti ya madhara yoyote yaliyotoke

Matokeo ya darasa la saba 2016

http://necta.go.tz/matokeo/2016/psle/psle.htm

Tuesday, October 25, 2016

Yanga yamkacha pluijm

Ni Siku moja baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans Hans van Pluijm atangaze kujiuzulu nafasi yake hiyo, baada ya kusikia kuwa kuna kocha kutoka Zesco United ya Zambia George Lwandamina amekuja tayari Tanzania kuchukua nafasi yake, leo October 25 amewaaga rasmi wachezaji wake na benchi la ufun

Hans amewaaga wachezaji wake pamoja na benchi la ufundi katika mazoezi ya leo asubuhi yaliofanyika katika uwanja wa Polisi Kilwa Road, kocha Hans anaondoka Yanga akiwa kaipa mafanikio makubwa ikiwemo kukushiriki hatua ya Makundi ya Kombe la shirikisho barani Afrika CAF, hatua ambayo Yanga wana miaka mingi toka waifikie.

Rais Magufuli ameteuliwa kuwania tuzo ya Forbes kwa watu maarufu barani Afrika

David King

Ikiwa leo ni October 25, 2016, Rais John Pombe Magufuli anatimiza mwaka mmoja tangu alipopigiwa Kura na wananchi wa Tanzania na kumchagua kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jarida linalofanyia tafiti watu maarufu na shughuli wanazozifanya la Forbes, limetangaza watu wanaowania tuzo ya Mtu Maarufu wa Mwaka.

Forbes wamemtaja Rais Magufuli kama kiongozi ambaye amefanikiwa kuongeza kiwango cha uchumi wa nchi yake huku akishindana na watu wengine kama Michael Le Roux ambaye ni muanzilishi wa Capitec Bank nchini Afrika Kusini, Benki ambazo zimeonekana kuwa rahisi zaidi kutumika na wananchi wa Afrika Kusini.

Wengine ni Thuli Madonsela, Ameenah Gulib pamoja na watu wa Rwanda.

Anachuana na watu wengine wanne wakiwemo: Rais wa Mauritania, Ameenah Gulib, Mwanzilishi wa Capitec Bank, Michiel Le Roux na Thuli Madonsela wa Afrika Kusini pamoja na watu wa Rwanda. Tuzo hii iliwahi kutolewa pia kwa mtanzania Mohamed Dewji mwaka 2015.

Mtu wangu unaruhusiwa kumpigia kura ya ushindi Rais Magufuli kupitia Hapa. Kumbuka mwisho wa kupiga Kura ni November 17, 2016 na tuzo hiyo itatolewa Nairobi Kenya

Mufahamu Diwani

1. DIWANI NI NANI?

(i) Ni Mwakilishi wa wananchi kwenye Kata.
(ii) Ni Mjumbe wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (Halmashauri ya Mji,
Wilaya, Manispaa au Jiji).
(iii) Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata

2. KUNA AINA NGAPI ZA MADIWANI?

Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura ya 287 na Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji), Sura ya 288, zinataja aina nne za madiwani, ambao ni:
• Madiwani wa kuchaguliwa;
• Madiwani wa kuteuliwa;
• Madiwani wa viti maalum (wanawake); na
• Wabunge (wa kuchaguliwa au kuteuliwa).

3. DIWANI ANAPATIKANAJE?

(i) Kwa kuchaguliwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano;
(ii) Kwa kuchaguliwa kwenye uchaguzi mdogo pindi nafasi ya Diwani inapokuwa wazi kwa sababu za: kifo cha Diwani; Diwani kukosa sifa za kuwa Diwani kwa mujibu wa sheria; kubatilishwa kwa uchaguzi wa Diwani; nafasi ya Diwani kuwa wazi kwa mujibu wa Sheria; na Diwani kukoma kuwa mwanachama wa chama cha siasa kilichomteua akiwakilishe; na

(iii) Kwa kuteuliwa na chama chake (kwa madiwani wa kuteuliwa wa viti maalum).

4. SIFA ZA KUGOMBEA UDIWANI

Mtu anaweza kugombea na kuchaguliwa kuwa Diwani iwapo anakidhi
sifa zifuatazo:
(i) Awe ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
(ii) Awe ametimiza umri wa miaka ishirini na moja au zaidi;
(iii) Awe na akili timamu;
(iv) Awe ni mkazi wa kawaida wa eneo la Mamlaka ya Serikali za Mtaa husika;
(v) Anaweza kusoma na kuandika Kiswahili na Kiingereza;
(vi) Awe ni mwanachama wa chama cha siasa kilichosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 na chama chake kimemteua akiwakilishe kwenye uchaguzi husika;
(vii) Awe na njia halali za kujipatia kipato;
(viii) Asiwe amehukumiwa kwa kosa la ukwepaji kodi ndani ya kipindi cha miaka mitano kabla ya uchaguzi.
(ix) Asiwe amehukumiwa kifo au amehukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi sita jela.

5. DIWANI ANA MAJUKUMU GANI?

Majukumu ya Diwani yanatokana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977; Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura ya 287; Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura ya 288; na

Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292.

Kwa ujumla Majukumu ya Diwani ni:

• Uwakilishi wa wananchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo
• Kuongoza wananchi kwa makini na uadilifu
• Usimamizi wa rasilimali na sheria
• Mgawaji wa Rasilimali kwa kufuata taratibu zilizowekwa
• Kusimamia Michakato ya Utungaji na upitishaji wa Sheria ndogo ndogo katika eneo lake la kazi
• Kuwawezesha wanajamiiwa eneo lake kupata fursa mbalimbali za kimaendeleo
• Kuongoza na kufanikisha wananchi wake katika kutatua migogoro mbalimbali katika kata
• Kuhamasisha shughuli za maendeleo katika eneo lake la kazi

6. DIWANI ANAWAWAKILISHA NANI?

Kifungu cha 14 (1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292, kinaeleza kuwa Diwani ni mwakilishi wa wananchi kwenye Kata aliyochaguliwa.

a.) Diwani kama Mwakilishi wa wananchi ana wajibu gani?

Diwani kama Mwakilishi wa wananchi ana wajibu ufuatao:

• Kuwakilisha wananchi wa Kata yake katika vikao vya Halmashauri.
• Kuhudhuria na kushiriki vikao vya Halmashauri.
• Kuwa kiungo kati ya wananchi na Halmashauri husika.
• Kutetea maslahi ya watu wa eneo analoliwakilisha.
• Kukutana na wananchi katika eneo lake ili kusikiliza na kuchukua maoni, mapendekezo, kero na matatizo ya watu wa eneo analoliwakilisha.
• Kutoa taarifa kwa wapiga kura kuhusu maamuzi ya jumla ya halmashauri na hatua zilizochukuliwa na Halmashauri ili kuondoa matatizo yaliyowahi kuelezwa na wakazi wa eneo lake la uchaguzi.
• Kusimamia na kudhibiti utumiaji wa rasilimali ya umma kupitia kamati za kudumu za madiwani.

b.) Je! Diwani ni Mwajiriwa wa Halmashauri?

Diwani si mwajiriwa wa Halmashauri, bali ni “Mwakilishi wa watu”, na hivyo anawajibika kwa watu anaowawakilisha na wakazi wa eneo la Halmashauri yake.

7. DIWANI KAMA KIONGOZI ANA WAJIBU GANI?

• Kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye shughuli za maendeleo.
• Kushirikisha wananchi katika uandaaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo.
• Kuitisha na kuendesha vikao vya Kamati ya Maendeleo ya Kata (Ward Development Committee -WDC).
• Kushiriki katika kufikia maamuzi na kutoa maelekezo kupitia vikao halali vya baraza la madiwani.
• Kuhamasisha wananchi kutunza mazingira na kuhifadhi maliasili za nchi.
• Kushiriki katika kufikia maamuzi na kutoa maelekezo kupitia vikao halali vya baraza la madiwani.
• Kuhakikisha kwamba watumishi wote waliopo katika eneo la kata yake wanafanya kazi zao kwa uadilifu na ufanisi na endapo utendaji wao hauridhishi anapaswa kutoa taarifa kwenye kamati husika au kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri yake.
• Kuhamasisha utawala bora.
• Kuhamasisha wananchi kulipa kodi na ushuru wa Halmashauri husika.

a). Je! Diwani ni Mtendaji?

Diwani si Mtendaji, bali ni Kiongozi na Mwakilishi wa wananchi, hivyo:
• Diwani hapaswi kuingilia utendaji wa idara yoyote katika Halmashauri kwa maslahi yake binafsi.

• Diwani hapaswi kuzuia au kujaribu kuzuia utekelezaji wa maamuzi ya baraza la madiwani au kamati au mwajiriwa au wakala wa Halmashauri.

8. DIWANI KAMA MSIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UMMA ANA WAJIBU GANI?

• Kufuatilia utekelezaji wa maamuzi ya vikao vya Baraza la Madiwani.
• Kufuatilia matumizi ya fedha za Halmashauri kwa lengo la kujiridhisha kuwa matumizi ya fedha hizo hayavuki bajeti iliyoidhinishwa na kwamba fedha zote zimetumika kwa madhumuni yaliyopangwa.
• Kusimamia matumizi bora ya rasilimali za umma kwenye Halmashauri yake.
• Kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Kata yake.
• Kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria, Taratibu, Kanuni, Miongozo, Sheria ndogo ndogo na miongozo ya Halmashauri.
• Kufuatilia utekelezaji wa maamuzi, mipango na utoaji wa huduma katika kata yake na kutoa taarifa kwenye vikao vya Halmashauri au kamati za Halmashauri endapo kuna kasoro za msingi za utekelezaji.
• Kushiriki katika kufanya maazimio na maamuzi ya kuwawajibisha watendaji wazembe na wasio waadilifu.
• Kusimamia utekelezaji wa mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

9. DIWANI KAMA MSIMAMIZI WA UGAWAJI WA RASILIMALI ANA WAJIBU GANI?

• Kuwashirikisha wananchi katika kuainisha vyanzo vya mapato, mahitaji, fursa na vipaumbele vyao.
• Kuhakikisha ukusanyaji na matumizi sahihi ya mapato kulingana na mahitaji na vipaumbele vya wananchi.
• Kusimamia mchakato mzima wa mipango na bajeti.
• Kuidhinisha makisio ya mapato na matumizi ya Halmashauri baada ya kuzingatia tathmini ya mahitaji na rasilimali zilizopo.
• Kuhakikisha kuwa kazi zilizopangwa zimetengewa bajeti.

10. KAMA JUKUMU LA KUTUNGA SHERIA NI LA BUNGE, DIWANI AMEPATA WAPI MAMLAKA YA KUTUNGA SHERIA?

Diwani amepewa mamlaka ya kusimamia na kutunga sheria ndogo ndogo na kifungu cha 153 (1) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura 287, kifungu cha 89 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Mji), Sura 288 na Kifungu cha 122 (1) (d) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura ya 287. Mamlaka haya hutekelezwa kupitia vikao halali vya Baraza la Madiwani.

Uwezo huu wa kutunga Sheria ndogo ndogo unahusisha mambo mawili:

i) Kutunga Sheria ndogo zitakazotumika katika eneo la mamlaka yao; na
ii) kupitisha sheria ndogo ndogo zilizotungwa na Halmashauri za vijiji zilizopo katika eneo la mamlaka yao.

Sheria ndogo ndogo ni Zipi?

Sheria ndogo ndogo (by-laws) ni kanuni zilizotungwa kwa mujibu wa sheria ya bunge kwa ajili ya kurahisisha au kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya mamlaka husika au kusaidia utekelezaji wa sheria mama.

11. DIWANI KAMA MUWEZESHAJI ANA WAJIBU GANI?

i) Kusikiliza matatizo ya wananchi, kujadiliana na kuwashauri hatua za kuchukua mfano kutafuta mtaalam wa kilimo katika eneo lake
ii) Kuwezesha watu kupata taarifa muhimu kuhusu masuala ya maendeleo.
iii) Kuwasaidia wananchi waone fursa zinazowazunguka katika nyanja za sekta kuu kama uchumi, maji, afya, miundombinu, elimu na siasa.
iv) Kupitia wataalamu waliomo kwenye Kata yake, kuwawezesha wananchi kupata mafunzo kuhusu masuala mbalimbali ya
kiuchumi, kisiasa na kijamii kama vile kilimo, ujasiriamali, afya bora, makazi bora, n.k.
v) Kuhamasisha wananchi kujitegemea
vi) Kuondoa vikwazo vya kisheria na kiutawala, kama vile urasimu usio wa lazima.
vii) Kufanikisha ushirikishwaji wa wananchi katika mipango, utekelezaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo katika
maeneo yao.
viii) Kuhamasisha ulinzi wa amani, usalama, demokrasia, utawala bora na uzingatiaji wa sheria katika maeneo yao.

12. DIWANI ANATAKIWA KUWA NA MWENENDO GANI?

Diwani anapaswa kuwa na mwenendo wenye maadili mema kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za Maadili na Mwenendo wa Madiwani (Tangazo la Serikali Na. 280 la mwaka 2000).

Kwa kifupi , Diwani anapaswa awe na mwenendo ufuatao:

• Kuendesha shughuli zake kwa kujenga imani ya wananchi
• Kuheshimu na kuzingatia sheria
• Kutotumia nafasi yake kwa faida yake, au familia yake, marafiki zake n.k.
• Kutojiweka katika hali ya mgongano na maslahi yake.
• Kuwajibika kwa jamii na Halmashauri yake kutokana na matendo yake na maamuzi ya Halmashauri.
• Kuwa muwazi, mkweli na muaminifu.
• Kufanya maamuzi bila upendeleo au ubaguzi na kwa kuzingatia sheria na haki.
• Kuhakikisha kuwa habari zote za siri za wananchi zinahifadhiwa kwa mujibu wa sheria, na hazitumiki kwa maslahi au faida binafsi.
• Kutoshiriki katika majadiliano au kupiga kura kuhusu jambo ambalo ana maslahi nalo.
• Kutoa taarifa kuhusu maslahi na mali zake pale inapobidi kufanya hivyo.
• Kuheshimu nafasi na hadhi ya madiwani wenzake na watumishi wa Halmashauri.
• Kutokuwa na uhusiano wa kimapenzi usiokubalika kati yake na Diwani mwenzake au watumishi wa Halmashauri.
• Kutoomba wala kupokea rushwa/hongo au zawadi kutoka kwa mtu anayemhudumia.

NB.
SIYO LAZIMA DIWANI WA ENEO LAKO AWE NA SIFA ZILIZOTAJWA HAPO JUU HASA DIWANI WA CCM, NDIYO MAANA KILA BAADA YA MIAKA MITANO UNAPEWA FULSA EWE MWANANCHI WA KUCHAGUA DIWANI BORA: HASA KUTOKA CHADEMA /UKAWA

CC: Ephely Ng'ondya Ibrahim Mwavulili Ngogo Jackson Taifa Mbogela Tumaini Kamaghe Tito Ngajilo

Friday, October 21, 2016

Pikipiki yaajabu dar es Salaam

Na Dotto Mwaibale
PIKIPIKI yenye namba za usajili T 684 CJZ aina
ya Fokon iliyotelekezwa kwa zaidi ya mwaka
mmoja katika kituo cha waendesha bodaboda
cha Maganga Veterinary Temeke jijini Dar es
Salaam inazua hofu kwa wananchi na hata kwa
askari polisi ambao wameshindwa kuipeleka
kituoni.
Imeelezwa kwamba pikipiki hiyo iliegeshwa katika
eneo hilo na mtu mmoja ambaye alifika nayo
akiwa akiiendesha mwishoni mwa mwaka jana.
Akizungumza jana na mtandao wa www. habari
za jamii.com mmoja wa waendesha bodaboda
wa kituo hicho ambaye hakupenda kujitambulisha
jina lake alisema pikipiki hiyo inawapa hofu
wananchi wa eneo hilo na hata waendesha
bodaboda.
"Hata sisi wenyewe tuna hofu na pikipiki hii ndio
maana tunaegesha mbalimbali na pikipiki zetu na
ndio maana sitaki kutaja jina langu" alisema
mwendesha bodaboda huyo.
Aliongeza kuwa awali baada ya pikipiki hiyo
kutelekezwa katika kituo hicho mtu yeyote
alipokuwa akiisogelea au kuigusa ilikuwa
ikijiwasha yenyewe lakini baada ya kupita mwezi
mmoja iliacha kujiwasha jambo ambalo
limeongeza hofu kwa wananchi.
Mkazi mwingine wa eneo hilo aliyejitambulisha
kwa jina moja la Ismail alisema hata walipotoa
taarifa kituo cha polisi cha Maganga walishindwa
kuichukua pikipiki hiyo kutokana na tabia ya
kujiwasha.
Alisema askari wa kituo hicho ambacho kipo mita
10 na eneo ambalo ipo pikipiki hiyo walitoa
taarifa kwa wenzao wa kituo cha Chang'ombe
ambao nao wameshindwa kuichukua na kwenda
nayo kituoni kwa ajili ya kumtambua mmiliki wa
pikipiki hiyo kupitia namba zake za usajili.
Ismail alisema inawezekana pikipiki hiyo
ilifungwa kifaa maalumu cha utambuzi iwapo
kama imeibiwa na ndio maana ilipokuwa ikiguswa
au kusogelewa inajiwasha yenyewe licha ya
baadhi ya watu wanahusisha kujiwasha kwake na
imani za ushirikina.
Imeelezwa kuwa pikipiki hiyo wakati inatelekezwa
ilikuwa katika hali ya upya lakini hivi sasa
imeanza kupoteza upya wake kwa kukosa
huduma ya matunzo.
Jitihada za mtandao huu kumpata Mwenyekiti wa
Serikali ya mtaa huo wa Maganga ili
kuzungumzia suala hilo zimeshindika baada ya
kuelekezwa alikuwa Manispaa ya Temeke
kwenye mkutano.

Boda Boda agonga roli apoteza maisha

Na Riziki Manfred mbinga

FRANK Ndunguru (24), mkazi wa
Mbinga mjini, amekufa papo
hapo baada ya bodaboda
aliyokuwa akiendesha kugonga
gari aina ya Mitsubishi Fuso kwa
nyuma.
Ndunguru alikutwa na mauti
alipokuwa akiendesha chombo
hicho akitokea Mbinga mjini
kwenda Mbamba Bay wilayani
nyasa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Ruvuma, Zuberi Mwombeji,
alisema jana ofisini kwake kuwa
tukio hilo lilitokea juzi saa tatu
asubuhi, katika eneo la Tangi la
Maji, Mbinga mjini, baada ya
bodaboda hiyo yenye namba za
usajili MC 238 AUJ, aina ya
SunLG kugonga Fuso iliyokuwa
imebeba mizigo.
Alisema Ndunguru aligonga gari
hilo kwa nyuma lililokuwa
likiendeshwa na Said Mohamed
(36) kutoka Mbinga kwenda Mbamba Bay, likiwa
limesheheni mizigo.
Mwombeji alisema chanzo cha ajali hiyo ni
mwendokasi wa dereva wa bodaboda aliyekuwa
akiendesha bila kuchukua tahadhari, hali ambayo
ilimfanya ashindwe kuumudu usukani.
Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo
kasi wa mwendesha bodaboda hivyo, amewataka
waendesha bodaboda kuwa makini
wanapoendesha bodaboda hizo.
Wakati huo huo, Mwombeji alisema polisi mkoni
humo, katika wilaya ya Tunduru, juzi walikamata
watu wanne wakiwa na lita 13.5 za pombe
haramu aina ya gongo ikiwa kwenye ndoo tayari
kwa kuuza.
Aliwataja watu waliokamatwa katika doria
iliyofanyika katika kata ya Kichangani kuwa ni
Hadija Hamanzi (24), Abdalah Hashim (20),
Rashidi Charles (42) na Shabani Mussa (29),
wote wakazi wa Kijiji cha Kadewele, Tunduru.
Pia alisema katika wilaya ya Songea, polisi
wakiwa kwenye doria eneo la Bombambili,
walimkamata Mapambano Seif (30) akiwa na
gramu 250 za bangi alizokuwa amehifadhi
kwenye mfuko wa plastiki.
Kamanda Mwombeji alieleza kuwa watuhumiwa
wote katika matukio mawili tofauti, wanatarajiwa
kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi
kukamilika.

Thursday, October 20, 2016

Kutoka kwenye kurasa za watu maarufu

Majaribu hayana Budi Kuja
na Kyaka kya Pakano 

Nilivosikia sakata la wanafunzi wa elimu ya Juu kukosa mikopo nimeanza kupata hofu.

Nimeanza kupata hofu kwasababu nikiunganisha nukta naona hazioani vizuri. Nilimsikia na kumsoma mkuu wa nchi akiwa kwenye kampeini mwaka jana akisema kila mwanachuo mwenye sifa atapata mkopo.

"Serikali yangu haitarajii kuona mwanafunzi akifukuzwa chuo kwa kosa la kugoma kisa mkopo, bali ikitokea mgomo, watawajibisha maofisa wa Bodi ya Mikopo kwa kuchelewesha fedha.”  JPM  Kampeini za Urais Oktoba. 2015.

Lakini cha kushangaza mambo hayajawa kama ambavyo yalikuwa yameahidiwa kwenye kampeini. Mwaka mmoja kamili toka ahadi hiyo ilivyotolewa tunasikia habari tofauti juu ya mikopo ya elimu ya Juu.

Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kwamba kati ya wanafunzi 88,000 walioomba mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu  66,000 wakosa mikopo. Mwananchi 20.10.2015

Mpaka sasa serikali imetoa mikopo kwa wanafunzi 11,000 tu nchi nzima na imeahidi kuongeza wanafunzi 10,500 katika awamu nyingine ili kufanya idadi kamili ya waliopewa mikopo ifikie 21,500 tu kati ya 88,000 walioomba mikopo. (Mwanahalisi Online 20.10.2016)

Kinachonitisha ni mambo mawili. La kwanza ni kuwa Mkuu aliahidi kwenye kampeini kuwa ikitokea kuna wanafunzi watakosa mikopo basi mabosi wa bodi ya mikopo wajiandae kuchukuliwa hatua kali.

Pili kutokana na wanachuo kadhaa kukosa mikopo ninaamini kabisa wanaweza wakawa wanafikiria kugoma.

KITENDO cha wanafunzi wa vyuo vikuu kunyimwa mikopo huku wachache waliopewa wakipunguziwa fedha za kujikimu kimeichukiza Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) na kuamua kuwazuia wanafunzi wa mwaka wa kwanza kusaini malipo ya fedha hizo. (Jamiiforums 20.10.2015)

Hatuwezi kukubaliana na uonevu huu, watoto wa masikini hawataweza kuendelea na masomo, wanapewa mpaka Sh. 500/= ya chakula na malazi kwa siku. Elimu ndiyo chimbuko la ukuaji wa sekta zote, lazima serikali iwekeze, kuwatelekeza wanafunzi ni kulitelekeza taifa,” Kasunzu Eliudi, Waziri wa Mikopo DARUSO,

Sasa ninapoona daliliza kugoma naona kama hawa wanataka kum-beep mheshimiwa rais. Mheshimiwa rais alishasema hajaribiwi. Hata alipokuwa anaongea UDSM siku alienda kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa maktaba akifafanua suala la wale wanachuo wa UDOM alisema, nanukuu “Kama (Udoma) wangegoma nilikuwa tayari kukifunga chuo hicho hata kwa miaka  mitano (Juni 2016)

Mheshimiwa alikuwa tayari kuifunga UDOM hata kwa miaka 5, sasa itakuwaje kama mwaka wa kwanza wataamua kugomea kabisa masomo ili mikopo iongezwe na wengine waliokosa wapewe? Je wanachuo watapishana na kauli au msimamo wa Rais alioutoa Singine mwezi wa nane??  Alisema, nanukuu“Sitaki nchi hii iwe ya vurugu, watakaoleta vurugu mimi nitawashughulikia kikamilifu bila huruma na wasije wakanijaribu, mimi ni tofauti sana na kama wapo watu wanaowatumia wakawaeleze vizuri, mimi sijaribiwi na wala sitajaribiwa,” alisema Rais Magufuli.

Nawaonea huruma sana wadogo zangu wanaoingia chuo mwaka huu lakini ninaona jinsi ambavyo itakuwa ngumu kwao kutumia ile njia iliyozoeleka njia ya Kunji.

Lakini nimuombe mheshimiwa Rais kuwa majaribu hayana budi kuja, na awe mvumilivu maana atakayevumilia mpaka mwisho huyo ndiye atakaye kuwa Mshindi.

Mungu Ibariki Tanzania

Tupo kikazi zaidi

Bonzuma Meadia Group full leo Ruvuma da

Wanachuo 600 kukosa mkopo

Dar es Salaam.

Ahadi iliyotolewa na
Rais John Magufuli wakati wa
kampeni mwaka jana kwamba katika
Serikali yake hakuna mwanafunzi
atakayekosa mkopo wa masomo ya
elimu ya juu imekuwa ngumu
kutekelezeka.
Uchunguzi wa Mwananchi umebaini
kwamba kati ya wanafunzi 88,000
walioomba mikopo kutoka Bodi ya
Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya
Juu (HESLB), wengi hawatapata.
Uwezo wa bodi hiyo ni kutoa mikopo
kwa wanafunzi 21,500 pekee sawa
na asilimia 24 na waliopatiwa hadi
sasa ni wanafunzi 11,000 sawa na
asilimia 12.
Takwimu hizi zinaonyesha kwamba
zaidi ya robo tatu ya wanafunzi
wanaohitaji mikopo watakosa
kutokana na uwezo mdogo wa
kifedha.

Mbinu mpya ya ufisadi yagundulika

DAR ES SALAAM
UAMUZI wa Ikulu kufuta mialiko ya viongozi
mbalimbali kushiriki kuzima Mwenge wa Uhuru
mkoani Simiyu umefichua namna fedha za
umma zinavyotafunwa kupitia malipo ya
masurufu (imprest) Raia Mwema likielezwa
kuwa saini moja ya kiongozi katika kitabu cha
wageni wizarani au idara yoyote ya serikali
inaweza kufanikisha uchotaji wa hata shilingi
milioni moja.
Raia Mwema limeelezwa na vyanzo vyake
mbalimbali kwamba umekuwa ni utamaduni
mkongwe kwa viongozi wengi wa umma kufuja
fedha kila wanapokuwa na safari za kikazi na
wamekuwa wakifanya hivyo kupitia masurufu na
kwa ustadi mkubwa wamekuwa wakikwepa
kunaswa katika kashfa za udanganyifu.

Ratiba ya AFCON 2017 NCHINI GABON

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetoa
makundi ya timu zitakazoshiriki michuano ya
AFCON 2017 nchini Gabon, kwa upande wa
wakilishi wa ukanda wa Afrika Mashariki Uganda
The Cranes wamepangwa Kundi D lenye timu za
Ghana, Mali na Misri.
Timu ya taifa ya Ivory Coast itapambana na
kocha wake wa zamani Herve Renard baada ya
kupangiwa katika kundi moja na Morocco katika
michuano ya fainali za kombe la mataifa ya
Afrika.
Michuano hiyo ya AFCON 2017 itaanza rasmi
January 14 2017 na kumalizika February 5 2017
nchini Gabon.

Wednesday, October 19, 2016

Pitia hii kutoka viunga vya TFF

Kocha Khalfan Ngassa amekuwa kwenye benchi
la timu ya mpira wa miguu ya Toto Africans ya
Mwanza akiwa kocha msaidizi kwa mechi tatu
mfululizo za Ligi Kuu ya soka Tanzania bara
inayoendelea kwenye viwanja mbalimbali
nchini.
Khalfan Ngassa aliongoza timu kwenye mchezo
Na. 62 dhidi ya Kagera Sugar Oktoba 7, 2016;
mchezo Na. 67 dhidi ya Mbao FC uliofanyika
Oktoba 12, 2016 na Mchezo Na. 79 dhidi ya
Majimaji ya Songea uliofanyika Oktoba 15,
mwaka huu.
Kwa mujibu wa Kanuni ya 72 (3) (5) ya Ligi Kuu,
Kocha Mkuu anatakiwa kuwa na Leseni ya chini
kuanzia Daraja B ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Barani Afrika (CAF) na Daraja C kwa
Kocha Msaidizi pia kutoka CAF.
Idara ya Ufundi ya Shirikisho la soka nchini
(TFF) limethibitisha kuwa Kocha Khalfan
Ngassa hana leseni yoyote kati ya hizo, hivyo
hastahili kukaa kwenye benchi la timu ya Toto
Africans kama kocha mkuu au kocha msaidizi.
Kitendo kinachofanywa na Toto Africans ni
ukikwaji wa kanuni na ni vema uongozi wa Toto
ukamwondoa Khalfan Ngassa kwenye benchi ili
kuepuka adhabu. Kipendele cha (7) cha kanuni
hiyo ya 72, inaelekeza adhabu kuwa inaweza
kutozwa si chini ya Sh 500,000 (shilingi laki
tano).
Pia tunazikumbusha klabu zote kuanzia msimu
ujao wa 2017/18 wa ligi kuu ya soka Tanzania
bara, kocha anayestahili kukaa kwenye benchi ni
yule mwenye leseni Daraja A kwa nafasi ya
Kocha Mkuu na angalau Leseni Daraja B kwa
kocha msaidizi.

Scopion afunguliwa mashitaka mengine

Mahakama ya Wilaya
ya Ilala, imemfungulia mashtaka
mapya Salum Njwete (Scorpion).
Amefunguliwa mashtaka mengine
yanayofanana na ya awali ya
unyang’anyanyi wa kutumia silaha.
Hata hivyo Njwete amekana shtaka
na kurudishwa rumande,huku
Hakimu Flora Haule anayesimamia
kesi hiyo akizuia dhamana.
Awali Mahakama hiyo ilimfutia
mashtaka yanayomkabili Scorpion
baada ya upande wa mashtaka
kuomba shtaka hilo liondolewe
mahakamani kwa sababu hawana
nia ya kuendelea na kesi hiyo na
Kutokana na maombi hayo, Hakimu
Adelf Sachore alikubaliana na ombi
hilo kwa kuzingatia kifungu namba
91 kifungu kidogo cha kwanza cha
sheria ambacho kinampa Mamlaka
Mkurugenzi Wa Mashtaka nchini
(DPP) kuondoa shtaka mahakamani
muda wowote ili mradi kama kesi
hiyo haijatolewa hukumu.
Lakini kifungu hicho kinampa
Mamlaka DPP kumshtaki upya
mshtakiwa huyo kama ana nia ya
kuendesha shtaka hilo.
Njwete anakabiliwa na shtaka la
unyang'anyi wa kutumia silaha na
kumjeruhi Saidi Mrisho.

Taarifa kwa vyombo vya habari

Hii Taarifa (katika picha) inasambazwa
mitandaoni kwamba Imetoka IKULU.
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais ,Gerson
Msigwa kasema ni ya uongo,
imetengenezwa na watu wenye nia ovu
hivyo

ASKARI POLISI MORO WAMPONZA MKURUGENZI MTENDAJI HALM YA WILAYA YA MKINGA TANGA KWA RAIS Magufuli


RAIS John Magufuli ametengua uteuzi wa
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya
ya Mkinga mkoani Tanga, Emmanuel Mkumbo
siku moja baada ya kufikishwa mahakamani kwa
makosa ya usalama barabarani pamoja na
kutishia kumuua kwa bastola askari wa usalama
barabarani.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais, Ikulu jana kwa vyombo vya
habari, Rais Magufuli ametengua uteuzi huo
kuanzia Oktoba 18, 2016.
“Uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Wilaya ya Mkinga atakayejaza nafasi ya
Emmanuel Mkumbo utafanywa baadaye,” ilieleza
taarifa ya Ikulu.
Julai 7, mwaka huu, Rais Magufuli alifanya uteuzi
wa wakurugenzi wa halmashauri za majiji
matano, manispaa 21, miji 22 na wilaya (DC) 137
za Tanzania Bara.
Katika uteuzi huo uliotangazwa na Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (Tamisemi), Mussa Iyombe, kati ya
wakurugenzi wote 185 walioteuliwa, 65
wameteuliwa kutoka orodha ya wakurugenzi wa
zamani na 120 ni wakurugenzi wapya, akiwamo
Mkumbo aliyepangiwa Halmashauri ya Wilaya ya
Mkinga.
Juzi, Mkumbo (41) alipandishwa kizimbani katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro
kwa tuhuma za kumtishia kumuua kwa bastola
askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani
humo pamoja na kuvunja sheria za usalama
barabarani.
Mkumbo, ambaye ni mkazi wa Tegeta jijini Dar
es Salaam, alipandishwa kizimbani na alisomewa
mashtaka hayo na Mwendesha Mashtaka wa
Serikali, Sunday Hyera, akisaidiana na Ediga
Bantulaki mbele ya Hakimu Agripinas Kimanze.
Kwa mujibu wa waendesha mashitaka hao wa
serikali, mtuhumiwa huyo anakabiliwa na kesi
mbili, ya kwanza ikiwa ni kesi ya jinai kifungu
cha 226 ya mwaka 2016 na ya pili ni kesi ya
Usalama Barabarani Kifungu cha 222.
Mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo
Oktoba 15, mwaka huu, eneo la Mkambarani
Wilaya ya Morogoro katika barabara kuu ya
Morogoro-Dar es Salaam wakati akiendesha gari
aina ya Toyota Pajero yenye namba za usajili T
845 CTJ.
Kosa la kwanza linalomkabiri Mkurugenzi
Mtendaji huyo ni kutishia kumuua kwa bastola
askari aliyejulikana kwa jina la Koplo Titunda,
akiwa katika majukumu yake ya kikazi na makosa
mengine ni kuendesha gari lenye namba T845
CTJ aina ya Toyota Pajero bila ya kuwa na leseni
na kuendesha gari bila bima.
Hyera alidai kuwa makosa mengine ni mwendo
kasi katika eneo lililoruhusiwa kuendesha
mwendo wa spidi 50 kwa saa, lakini alivuka na
kufikia 85, kugoma kupeleka gari kituo cha Polisi
na kuendesha bila kuwa na uangalifu barabarani.
Mtuhumiwa huyo alikana makosa hayo na
kuachiwa kwa dhamana, huku kesi yake
ikitarajiwa kufikishwa tena mahakamani hapo
Oktoba 31, mwaka huu, Hata hivyo, jitihada za
waandishi wa habari kupata picha ya mtuhumiwa
hazikufanikiwa baada ya askari kumziba
mtuhumiwa kwa koti pamoja na kofia aina ya
pama na kumuingiza katika gari aina ya Toyota
na kutokomea naye.

Tuesday, October 18, 2016

Fuatilia makala hii kutoka mkono salama

La Norman ni Dili sio Dili??
Na: Kyaka kya Pakano.

Mwaka 2000 Dr. Hassy Kitine alichaguliwa kwa mara ya pili kama mbunge wa Maketekuwa ndio anaanza kipindi chake cha kwanza kama Mbunge. Hii ni kwasababu kipindi cha kwanza alikuwa amemalizia miaka 2 ya aliyekuwa mbunge wa wakati huo ambaye alifariki Hayati Dr. Tuntemeke Mesaka Nung'wa Sanga.

Kitine alijikuta anaianza awamu yake ya Ubunge kwa machungu. Akiwa amejitwalia ujiko kuwa ni mtu wa karibu kabisa na Rais wa wamu ya Tatu, Ben Mkapa, Kitine aliteuliwa mara moja kuwa Mkuu wa mkoa wa Tanga, akateuliwa kuwa waziri  ofisi ya Rais anayesimamia utawala bora.

Lakini kabla jina la Kitine halijachanua sawa sawa mara mingong'ono kuwa anahusishwa na kashfa. baadaye ikaja ikaja kuwekwa wazi, Gazeti ambalo lilikuwa maarufu wakati huo la RAI likatoka na article Kitine amepiga deal la milioni 60 kwa kusingizia kuwa Mke wake anaenda kutibiwa Ulaya kumbe sivyo.

Kashfa ya ufisadi ya Kitine ikafika Bungeni, ikajadiliwa, Kitine alikataa kata kata kuwa hakuhusika na kashfa hiyo, lakini baadaye maji yalizidi unga, Mh. Kitine akawa hana namna bali kujiuzuru nafasi ya Ukuu wa Mkoa, akapigwa chini pia na nafasi ya Uwaziri katika ofisi ya Rais. Hatujakaa sawa muda wa uchaguzi ulipofika kitine akapoteza kiti cha ubunge katika kura za maoni kwa mtu ambaye hakuwa maarufu wakati huo Binilith S Mahenge.

Miaka 15 baadaye nimekuwa nikijiuliza kama Historia inaweza kujirudia? Mh. Norman Sigalla ambaye naye hajakaa muda mrefu amekuwa akiandamwa na jinamizi la kashafa za ufisadi.

Kwanza kulianza kusikika minong'ono ya chini chini kuwa Mheshimiwa kasajili chuo anachotumia kupigia madili ya pesa chafu kwenye taasisi anazozisimamia. Mheshimiwa alikanusha habari hizo.

Lakini kabla hiyo haijapoa, kama ilivyokuwa wakati wa Kitine, Gazeti maarufu la wakati huu " mwananchi" linaibuka na kashfa kuwa Mh. Alipiga dili chafu la karibu milion 5 kila mwezi kwa kipindi cha miezi 5 kama mfanyakazi hewa.

Sio nia yangu kuthibitisha hayo kama yametokea au kukanusha, ninachotaka kusema ni kuwa naona kama Mh. Normana anatembea njia inayofanana na Njia ya Kitine.

Lakini kuna mambo ya kujiuliza, kwa mujibu wa maelezo ya katibu tawala wa Mkoa inasemekana kuna kijana wa idara ya Utumishi pale mkoani alirudisha jina la Normana kwenye system. Na kijana huyo amechukuliwa hatua za kinidhamu. Hapa Songea wanasema jamaa akasimamishwa kazi na anasubiri kupelekwa mahakamani.

Sasa swali tunalojiuliza vijiweni, huyu kijana aliingiza jina la Norman Sigalla ili iweje?

Angekuwa ameingiza alafu akatengeneza akaunti fake achukue pesa tungesema basi huyu kijana alitaka kuiba pesa, lakini hakufanya hivyo, aliingiza jina pamoja na account namba zote za Mh. Norman Sigalla bila shaka huyu kijana alilenga kuw apesa zimfikie Norman Sigalla

Baadhi yetu tunadhani kuwa huenda yule kijana alikuwa ameingiza jina lile kimakosa. Lakini cha kushangaza ni kuwa baada ya jina kuingizwa Mkoani lilihitaji kupitishwa na maofisa wa wizara ya Utumishi, jina lilifika kule likapitishwa. Baada ya kutoka wizara ya Utumishi jina lilitakiwa liende Hazina lipate checque namba na kulipangia mshahara, jina likaenda hazina (wizara ya Fedha) likapata Cheque namba na kupangia mshahara.
Baada ya hapo mshahara ukaanza kutiririka. Kosa la Norman alipoona mshahara unaingia akajisemea kale kamsemo ketu ka kitoto, "Cha kuokota si cha kuiba, mwenye mali ni mzembe" akawa anapiga zile pesa kimya kimya, bila kumwmabia mtu. Ukizingatia alikuwa ametokea kwenye uchaguzi akaona hapa ndio pa kuzibia matobo ya mfuko yaliyotoboka wakati wa uchaguzi. KOSA LA KWANZA. Akapiga 4,600,000 kila mwezi kwa miezi 5 mpaka Rais alipowashtua kuwa kuna watu wanakwiba pesa za umma kwa mishahara hewa.

Baada ya hili dili kushtukiwa katibu tawala wa Mkoa akamuandikia Katibu wa  Bunge Dkt. Thomas Kashilila kumfahamisha kuwa mbunge wake anatuhumiwa kukwapua hizo pesa. Katibu wa Bunge akampa Norman Soft terms kuwa akakae na uongozi wa mkoa wakubaliane ili hizo pesa zikatwe kwenye mshahara wake wa ubunge na kurudishwa kimya kimya Hazina. Hapa inaonesha bunge lilitaka kumbeba Norman, waue soo hili kimya kimya.

Sijui nini kilikuwa kimemsibu kaka yangu Norman, maana lipigwa upofu hakuiona hii ofa, wengine wanasema Mheshimiwa ana kiburi san ahata akiona ushauri wa wazi kutokana na tabia yake ya kujiamini huwa anaupuuza, Akaupuuza ushauri huu. Kama angefuata ushauri huu, maana yake angekuwa amerudisha pesa kimya kimya na hakuna ambaye angekuja kujua. Kukataa Ushauri wa kuwa akapige magoti mkoani arudishe pesa hizo ni KOSA LA PILI.

Jambo linguine ambalo Norman angefanya ilikuwa baada ya kusikia kuwa Rais ametangaza kusaka wafanyakazi hewa na yeye jina lake linatajwa alitakiwa ashtuke ajifanye ndio kwanza ameona pesa kwenye akaunti yake, aitishe vyombo vya habari awalalamikie ofisi ya Mkoa, wizara ya Utumishi na hazina (wizara ya fedha). Maana yake nini? Kama angejitokeza wazi hadharani mapema aseme jamani kuna mtu kaweka pesa kwenye akaunti yangu simjui ni nani? Ingemfanya angalau ajisafishe aonekane hakuhusika na kusuka dili la kumpa mshahara wa Mkuu wa wilaya. Kitendo cha Mh. Norman kuacha jambo hili liendelee lenyewe ni KOSA LA TATU.

Baada ya sakata hili kusikika kwenye vyombo vya habari leo, washabiki na wapenzi wa Mh. Norman wamesikika wakisema huu ni ugomvi wa kisiasa wa jimbo la Makete. Unajiuliza kwani Kitine alivyochafuka kwa ile kashafa alikuwa anagombea jimbo na nani? Uchaguzi ulikwisha na sasa Mbunge yupo kazini na mpinzani wake kapewa cheo kikubwa kuliko nafasi ya Ubunge, ni Mkuu wa Mkoa. Lakini embu tuone, Je ingewezekana Mehenge kufanya hii fitina. Gazeti linasema Jina la Norman liliingizwa kwenye mshahara mwezi wa 9 mwaka jana. Mahenge hakuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma. Alafu Rais ametangaza kusaka watumishi Hewa mwezi wa tatu  (Machi) Mahenge alikuwa bado hajateuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma wala hakujua kama atakuja kuwa mkuu wa Mkoa wa Songea. Habari za Mitaani zinasema kuwa Jina la Norman Limekuja kubainika kuwa yumo kwenye watumishi Hewa Mwezi wa 4 Mahenge alikuwa bado hajapewa nafasi ya Ukuu wa Mkoa. Sasa Mahenge aliingizaje jina la Norman kwenye ordha?? Kuendelea kujaribu kutafuta kisingizio cha kuonyesha watu kuwa Norman amebambikizwa kesi hii na Mahenge inampotezea direction ya kutafuta njia muafaka ya kutatua tatizo hilo. KOSA LA NNE

Norman aliposikia kuwa jina lake limetoka katika watumishi hewa alishauriwa kuwa matafute kijana aliyeliingiza lile jina ili yule kijana atoroke asionekane  hapa Songea. Lakini kwa hulka ile ile ya kujiamini Norman akasema hakuna haja ya kukimbia, waliamini hakuna mtu atajua yule kijana ndio aliingia kwenye mfumo na kuingiza jina kwenye data base. Baadaye msako ulivyoendelea yule kijana si akabambwa, mtandao ukaonyesha aliingia lini, na aliingiza jina lipi na lipi. Sasa yule kijana amesimamishwa kazi na anasubiri kupelekwa mahakamani. Sasa huyo kijana atakubalia aende mahakamni peke ake? Atakubali msala huu aubebe mwenyewe mwenyewe ukizingatia yeye hakula hizo pesa?? Kutokufanya utaratibu kabla msala haujasanuka kumsafirisha huyo mshikaji nje ya nchi ni KOSA LA TANO.

Inafact kuna makosa KUMI lakini kwa leo niishie hapa nisiwachoshe.

Sasa hivi issue ya Norman inategemea sana huruma za Rais. Ninasema inategemea huruma za Rais kwasababu, Rais akisema watuhumiwa wote wa makossa ya Utumishi hewa wapelekwe mahakamani, Unadhani atasema Muacheni Mh. Norman? Itakuwa double standard. Kama Norman ataruidisha pesa sasa kama ambavyo katibu wa Bunge alishauri, Je itakubalika? Watumishi wengine nao wataruhusiwa kurudisha pesa?? Mmmh sijui. Lakini Rais akisema waruidhse pesa, basi hiyo ndio pona yake.

Ninajua Norman ni mzoefu wa kupambana na majanga, nimtakie kila la Kheri.

Mbunge wa Makete akanusha tuhuma za utumishi hewa

Mbunge wa Makete mh Norman Sigalla amekanusha taarifa za kupokea mshahara wa ukuu wa wilaya huku akisema hakuna hela ya mshahara ulio ingia kwenye account yake.

Akizungumza kwa njia ya simu mh Norman Sigalla amesema mpaka sasa hakuna mshahara ulio ingia kwenye account yake toka alipo sitaafu ukuu wa wilaya na hujui mpaka sasa kilichotokea

Kutoka kurasa maarufu

Ni jambo la kusikitisha ni mwez wa kumi sasa Barabara ya KENJA_IKUWO_ CHIMALA iliharibika sana na mvua zilizonyesha mwaka huu lakin hakuna jitihada zinazochukuliwa kufanya marekebisho ya barabara hii wakati Wilaya inapokea mapato kutoka barabara hii.Cjua kama mwaka huu wakaz wa bonde hili la IKUWO kama watasafirisha mazao yao.
Ujumbe mfikishien taarifa KING kua mambo huku c mazur atoe itikadi za VYAMA

Monday, October 17, 2016

Mbunge wa Makete Mtumishi hewa

Sakata la watumishi hewa sasa limefikia pabaya
baada ya msako wa watu wanaolipwa fedha bila
kuwapo kazini kumkumba Mbunge Makete
(CCM), Profesa Norman Sigalla ambaye alikuwa
mkuu wa Wilaya ya Songea.
Wadau walishawahi kueleza kuwa msako wa
watumishi hewa uliwahusu wafanyakazi wa
kariba ya chini na hivyo kuokoa fedha kidogo,
lakini sakata la Profesa Sigalla limeonesha kuwa
hata kariba ya juu serikalini inahusika.
Profesa Sigalla anadaiwa kupokea mshahara wa
ukuu wa wilaya kwa miezi mitano baada ya
kuacha kazi hiyo wakati wa Uchaguzi Mkuu na
baadaye kuchaguliwa kuwa mbunge kwa tiketi ya
CCM.
Hali hiyo imeisababishia Serikali hasara ya Sh23
milioni.
Baada ya kuacha kazi hiyo ya kuteuliwa na Rais,
inadaiwa kuwa Profesa Sigalla aliendelea
kupokea mshahara wake wa ukuu wa wilaya wa
Sh4.6 milioni kutokana na ofisa utumishi wa ofisi
ya katibu tawala wa Mkoa wa Ruvuma
kumrudisha kwenye orodha ya malipo ya
mshahara.
chanzo:gazeti la mwananchi

Kesi ya madereva Bajaji waliofungua majengo ya halmashauri ya mji makambako yapigwa kalenda

Na Riziki Manfred makambako

Hakimu wa Mahakama ya mwanzo Makambako amesongeza mbele Tarehe ya kusikiliza kesi ya uvamizi katika majengo ya halmashauri ya mji wa makambako unayo wakabili madereva wa Bajaj mjini makambako
  Awali Akisoma kesi hiyo hakimu wa Mahakama ya mwanzo Makambako mh Jackson Banobi  amesema  watuhumiwa wakiwa na wenzake walifanya kosa hilo mnamo Tarehe 10 octoba mwaka huu kwakufanya uvamizi katika majengo ya halmashauri ya mji makambako  na kuvunja madirisha manne na yenye thamani ya uthaminisho ikiwa milioni 3.3

Kesi hiyo imehiriswampaka Tarehe 20 octoba  na watuhumiwa kwa pamoja wamekana kutenda kosa huku wote wakiachiwa kwa dhamana ya mdhamini mmoja 

Sunday, October 16, 2016

Pitia hii Enzi za Tutemeke sanga

Ndugu zangu,
Hakika, mwaka 1995 unabaki kuwa ni uliokuwa
na matukio mengi makubwa; mengine ya
kushangaza na hata kustaajabisha.
Na matukio makubwa kwenye siasa hutanguliwa
na ishara. Kwa tuliokuwepo, tuliziona mapema
ishara za mwaka huo kutawaliwa na matukio
makubwa. Ikumbukwe, mwaka 1995 ndio nchi
iliingia kwenye Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa
vyama vingi tangu sheria ya vyama vingi ifutwe
mwaka 1964 na kurudishwa tena Julai 2, 1992.
Kwenye maktaba yangu naweza kuona, kuwa
hata wakati huo, ndani ya CCM, kulikuwa na
Kangi Lugora wake, wakati huo alikuwa Mbunge
aliyeitwa Tuntemeke Sanga. Huyu alikuwa
Mbunge machachari sana na aliyeaminika kuwa
alikuwa ni msomi sana. Akiwa Dar, mara kadhaa
nilimwona pale iliyokuwa Agip Hotel.
Kuelekea Bunge la Aprili 1995, Tuntemeke
Sanga alijipanga kuisulubu Serikali ya Chama
chake, CCM, iliyokuwa chini ya Mzee Ali Hassan
Mwinyi. Ni kuhusu sakata la Chavda na mpango
wa taifa wa ununuzi wa madeni ya taifa.
Ilisemekana kulikuwa na ufisadi kwenye mradi
huo. Waziri Mkuu Msuya aliahidi kulishughulikia
suala hilo huku Waziri wa Fedha, Profesa
Kighoma Malima akiweka wazi kuwa hakukuwa
na cha fedha za umma zinazodaiwa kwa
Mfanyibiashara Chavda.
Tuntemeke Sanga alitishia kuhamasisha
Wabunge wenzake wapige kura ya kukosa imani
kwa Serikali. Hivyo, kuangusha Serikali ya Mzee
Mwinyi.
Bunge la Aprili likafanyika na Waziri Mkuu
Cleopa Msuya alihimili tetemeko lile la
Tuntemeke Sanga. Na hivyo, Serikali ya Mzee
Mwinyi ilibaki salama.
Tumetoka Mbali.

Pilikapilika leo asubuhi makambako

Ajali yaua mkurugenzi Wizara ya Afya

Dar es Salaam. Ajali ya gari
iliyotokea leo asubuhi imesababisha
kifo cha Mkurugenzi Msaidizi wa
Elimu ya Afya kwa Umma wa
Wizara ya Afya, Maendekleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Hellen Semi.
Akithibitisha kuhusu ajali hiyo
msemaji wa wizara hiyo, Nsachris
Mwamwaja amesema ajali hiyo
imetokea asubuhi Chalinze mkoani
Pwani.
Amesema pia katika ajali hiyo,
mkurugenzi wa huduma za kinga wa
wizara hiyo, Dk Neema Rusibamayila
amejeruhiwa.
Amesema maofisa hao walikuwa
wanakwenda mkoani Dodoma
kuhudhuria mkutano wa waganga wa
mikoa unaoanza kesho.

MAAs ya yaanza kurudisha fadhila Malangali sekondari

Na Riziki Manfred
Mufindi Malangali

Umoja wa wanafunzi waliosoma Malangali sekondari miaka ya nyuma MAAs yaani Malangali allumin associtietion umejipipanga kuimaishalisha hadhi ya shule ya sekondari Malangali kwa kuanza kusaidia utatuzi wachangamoto mbalimbali
  Akizungumza na wanahabari katika mahafari ya 85 katika shule ya sekondari Malangali Mwenyekiti wa MAAs ndugu Paul Mang'ong'o amesema umoja huo una lengo la kurudisha hadhi ya shule hiyo ambayo imetoa wataalamu wengi katika nyanja tofauti wakiwemo wabunge na wengine
  Awali umoja huo ulisidia ukarabati wa ukumbi wa shule hiyo pamoja na skirini na kisimbusi ili kurahisisha upatikanaji wa Habari kwa Wanafunzi na walimu pia kuahidi kuendelea kusaidia shule hiyo
    Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo ndugu Ngonyali ameushukuru umoja huo kwa kuendelea kunisadia shule hiyo kwa kuanza kutatua Changa moto za miundombinu shuleni hapo
Shule hiyo kongwe nchini ambayo imetoa wataalamu mbalimbali imeanza kupoteza ubora wake hususani katika miundombinu licha ya Serikali kutangaza kuanza kukarabati shule kongwe nchini
 

Saturday, October 15, 2016

Mahafali ya 85 shule ya sekondari Malangali


Na Riziki Manfred Bonzuma na Cleef Mlelwa

Pitia Baadhi ya picha  za matukio wakati wa mahafari ya 85 katika shule ya sekondari Malangali pia umoja wa wanafunzi waliosoma Malangali (MAAs )

Mufindi

Wito umetolewa kwa Wanafunzi wote waliosoma katika shule ya sekondari Malangali kuungana na umoja wa wanafunzi waliosoma katika shule hiyo wenye lengo

Wito huo umetolewa na mlezi wa umoja wa wanafunzi waliosoma Malangali  sekondari miaka ya nyuma MAAs  bwana Yonno Stanley kevela amesema shule hiyo imetoa watu wengi katika nyanja tofauti hiyo ni muda wa kulipa fadhila kwa yake waliyo yapata shuleni hapo kwani umoja huo una lengo la kurudisha hadhi ya shule hiyo ambayo imeanza kupotea hususani miundombinu
       Katika mahafali hiyo ambayo pia iliudhuliwa na Viongozi wa umoja wa wanafunzi waliosoma Malangali sekondari yaani Malangali alumin associtietion akiwemo mwenye
Wa umoja huo ndugu Paulo Mng'ong'o ambaye pia ni afisa rasilimali watu kutoka Uhuru Meadia

    Kwaupande wake Mkuu wa Shule hiyo  ndugu ngonyali  ameushukuru umoja huo kwa kuendekeza kuchangia ukarabati wa miundombinu ukiwemo ukumbi skirini kisimbusi pamoja vifaa vya michezo

Shule hiyo kongwe nchini ambayo imetoa wataalamu mbalimbali waziri kama Mack Mwandosa wabunge kama Yonno Stanley kevela na wengine ipo Hatarini kupoteza hadhi yake baada ya miundombinu ya shule hiyo kuchakaa