Na Riziki Manfred makambako
Mkuu wa Mkoa wa njombe Rehema Nchimbi amewataka madereva kufuata sheria barabarani na kutoendeswa na askari wa usalama barabarani
Akihutubia wakazi wa mji wa makambako Katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya usalama barabarani ambayo kimkoa yamefanyika katika mji wa makambako Nchimbi amesema kumekuwa na tabia ya madereva kuonyeshana alama za kujulisha mahara askari wa usalama barabarani wamesema hivyo kuendelea kuongeza ajari za barabarani ambazo zinaweza kupungua au kuisha kabisa "najua madereva wengi wanawaogopa askari wa usalama barabarani hivyo wanafuta alama za barabarani eneo ambalo Kuna askari wa usalama barabarani nje ya hapo hawafuati hivyo kufanya imani ya ajali kuongeza
Awali akisoma Risala Mkuu wa usalama barabarani Mkoa wa njombe Kelvin Ndimbo amesema kuwa ajali za barabarani zimepungua katika mkoa wa njombe japo kwa mwaka 2016 kwa asilia 20 huku akizitaja sababu kubwa kuwa ni elevi wa kulindukia mwendo kasi ubovu wa vyombo vya usafiri na barabara
pia Ndimbo amesema jeshi la polisi kupitia askari wa usalama barabarani wamejipanga kuhakikisha wanaendelea kusimamia sheria kwa kuwachukulia hatua kali madereva wanaosabisha ajari
Katika maadhimisho hayo yaliyohudhuliwa na wanafunzi wa shule mbalimbali ambao wameuomba uongozi wa TANLODS Mkoa kuwawekea alama za pundamilia (zebra crros) katika eneo la barabara kuu ya Makambako Songea eneo la ghorofa la Japipo
No comments:
Post a Comment