Sunday, October 16, 2016

Pitia hii Enzi za Tutemeke sanga

Ndugu zangu,
Hakika, mwaka 1995 unabaki kuwa ni uliokuwa
na matukio mengi makubwa; mengine ya
kushangaza na hata kustaajabisha.
Na matukio makubwa kwenye siasa hutanguliwa
na ishara. Kwa tuliokuwepo, tuliziona mapema
ishara za mwaka huo kutawaliwa na matukio
makubwa. Ikumbukwe, mwaka 1995 ndio nchi
iliingia kwenye Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa
vyama vingi tangu sheria ya vyama vingi ifutwe
mwaka 1964 na kurudishwa tena Julai 2, 1992.
Kwenye maktaba yangu naweza kuona, kuwa
hata wakati huo, ndani ya CCM, kulikuwa na
Kangi Lugora wake, wakati huo alikuwa Mbunge
aliyeitwa Tuntemeke Sanga. Huyu alikuwa
Mbunge machachari sana na aliyeaminika kuwa
alikuwa ni msomi sana. Akiwa Dar, mara kadhaa
nilimwona pale iliyokuwa Agip Hotel.
Kuelekea Bunge la Aprili 1995, Tuntemeke
Sanga alijipanga kuisulubu Serikali ya Chama
chake, CCM, iliyokuwa chini ya Mzee Ali Hassan
Mwinyi. Ni kuhusu sakata la Chavda na mpango
wa taifa wa ununuzi wa madeni ya taifa.
Ilisemekana kulikuwa na ufisadi kwenye mradi
huo. Waziri Mkuu Msuya aliahidi kulishughulikia
suala hilo huku Waziri wa Fedha, Profesa
Kighoma Malima akiweka wazi kuwa hakukuwa
na cha fedha za umma zinazodaiwa kwa
Mfanyibiashara Chavda.
Tuntemeke Sanga alitishia kuhamasisha
Wabunge wenzake wapige kura ya kukosa imani
kwa Serikali. Hivyo, kuangusha Serikali ya Mzee
Mwinyi.
Bunge la Aprili likafanyika na Waziri Mkuu
Cleopa Msuya alihimili tetemeko lile la
Tuntemeke Sanga. Na hivyo, Serikali ya Mzee
Mwinyi ilibaki salama.
Tumetoka Mbali.

No comments:

Post a Comment