Sunday, October 30, 2016

Wanafunzi wapingwa na radi Mang'oto sekondari


Kutoka kwa Mwl Mgaya Mang'oto sekondari

Wanafunzi kumi wa Mang'oto Sekondari wamepigwa na RADI leo saa 07:30 mchana, wakati wamefoleni kupata chakula cha mchana. Nao ni Bruno Ilomo wa Usungilo, Ageth Tave wa Utweve, Manfred Mwageni wa Uwemba, Hasani Idawa wa Ilindiwe, Basili Mbilinyi wa Usungilo hawa wametibiwa na kurudi shuleni. Fainess Sanga wa Utweve, Atuganile Mbilinyi wa Usungilo, Frida Chengula wa Usungilo, Himidi Chengula wa Usungilo na Isaya Choza Sanga wa Makete Mjini wamelazwa Ikonda Hospitali. Huyu wa mwisho ameunguzwa zaidi upande wa kulia toka begani hadi mapajani. Tuwaombee wapone haraka. Amen!

No comments:

Post a Comment