Monday, October 17, 2016

Mbunge wa Makete Mtumishi hewa

Sakata la watumishi hewa sasa limefikia pabaya
baada ya msako wa watu wanaolipwa fedha bila
kuwapo kazini kumkumba Mbunge Makete
(CCM), Profesa Norman Sigalla ambaye alikuwa
mkuu wa Wilaya ya Songea.
Wadau walishawahi kueleza kuwa msako wa
watumishi hewa uliwahusu wafanyakazi wa
kariba ya chini na hivyo kuokoa fedha kidogo,
lakini sakata la Profesa Sigalla limeonesha kuwa
hata kariba ya juu serikalini inahusika.
Profesa Sigalla anadaiwa kupokea mshahara wa
ukuu wa wilaya kwa miezi mitano baada ya
kuacha kazi hiyo wakati wa Uchaguzi Mkuu na
baadaye kuchaguliwa kuwa mbunge kwa tiketi ya
CCM.
Hali hiyo imeisababishia Serikali hasara ya Sh23
milioni.
Baada ya kuacha kazi hiyo ya kuteuliwa na Rais,
inadaiwa kuwa Profesa Sigalla aliendelea
kupokea mshahara wake wa ukuu wa wilaya wa
Sh4.6 milioni kutokana na ofisa utumishi wa ofisi
ya katibu tawala wa Mkoa wa Ruvuma
kumrudisha kwenye orodha ya malipo ya
mshahara.
chanzo:gazeti la mwananchi

No comments:

Post a Comment