Friday, October 21, 2016

Boda Boda agonga roli apoteza maisha

Na Riziki Manfred mbinga

FRANK Ndunguru (24), mkazi wa
Mbinga mjini, amekufa papo
hapo baada ya bodaboda
aliyokuwa akiendesha kugonga
gari aina ya Mitsubishi Fuso kwa
nyuma.
Ndunguru alikutwa na mauti
alipokuwa akiendesha chombo
hicho akitokea Mbinga mjini
kwenda Mbamba Bay wilayani
nyasa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Ruvuma, Zuberi Mwombeji,
alisema jana ofisini kwake kuwa
tukio hilo lilitokea juzi saa tatu
asubuhi, katika eneo la Tangi la
Maji, Mbinga mjini, baada ya
bodaboda hiyo yenye namba za
usajili MC 238 AUJ, aina ya
SunLG kugonga Fuso iliyokuwa
imebeba mizigo.
Alisema Ndunguru aligonga gari
hilo kwa nyuma lililokuwa
likiendeshwa na Said Mohamed
(36) kutoka Mbinga kwenda Mbamba Bay, likiwa
limesheheni mizigo.
Mwombeji alisema chanzo cha ajali hiyo ni
mwendokasi wa dereva wa bodaboda aliyekuwa
akiendesha bila kuchukua tahadhari, hali ambayo
ilimfanya ashindwe kuumudu usukani.
Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo
kasi wa mwendesha bodaboda hivyo, amewataka
waendesha bodaboda kuwa makini
wanapoendesha bodaboda hizo.
Wakati huo huo, Mwombeji alisema polisi mkoni
humo, katika wilaya ya Tunduru, juzi walikamata
watu wanne wakiwa na lita 13.5 za pombe
haramu aina ya gongo ikiwa kwenye ndoo tayari
kwa kuuza.
Aliwataja watu waliokamatwa katika doria
iliyofanyika katika kata ya Kichangani kuwa ni
Hadija Hamanzi (24), Abdalah Hashim (20),
Rashidi Charles (42) na Shabani Mussa (29),
wote wakazi wa Kijiji cha Kadewele, Tunduru.
Pia alisema katika wilaya ya Songea, polisi
wakiwa kwenye doria eneo la Bombambili,
walimkamata Mapambano Seif (30) akiwa na
gramu 250 za bangi alizokuwa amehifadhi
kwenye mfuko wa plastiki.
Kamanda Mwombeji alieleza kuwa watuhumiwa
wote katika matukio mawili tofauti, wanatarajiwa
kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi
kukamilika.

No comments:

Post a Comment