Hivi karibuni kumeibuka upotoshaji
mkubwa kutoka kwa baadhi ya watu
wenye nia ovu ya kutaka kuharibu taswira
nzima ya Mshindi wa shindano la Miss
Tanzania 2016,aliyevishwa taji hilo jana
usiku ndani ya jiji la Mwanza,taarifa hizo
ambazo zimekuwa zikisambazwa katika
mitandao ya kijamii zikieleza upotoshaji
wa taarifa mbalimbali za mlimbwende
huyo zikiwemo na elimu yake.
SEHEMU YA TAARIFA ILIYOKUWA
IKIPOTOSHWA KATIKA MITANDAO
MBALIMBALI YA KIJAMII HII HAPA CHINI;
MISS TANZANIA 2016
🙊🙊🙊🙊🙊🙊
JINA:Diana Edward Lukumai
UMRI:Miaka 18
ELIMU:Shahada(degree)
Hii ina maana;
Alianza Chuo akiwa na miaka 15
Alianza Form one akiwa na miaka 9
😂😂😂😂😂😂
Ingawa sio mshabik wa haya mambo
napenda nchukue hii nafasi kuwapongeza
Wazazi wote kama wazazi wa Diana
ambao watoto wao wameanza shule ya
msingi wakiwa na miaka miwili
HII NDIO TAARIFA SAHIHI YA MSHINDI
WA SHINDANO LA MISS TANZANIA
2016,DIANA EDWARD LOY.
Napenda kuujulisha Umma yafuatayo;
1. Miss Tanzania 2016/2017 aliyeshinda taji
jana jijini Mwanza, anaitwa Diana Edward
Loy na siyo Diana Lukumai kama
inavyotajwa mitandaoni.
2. Mlimbwende huyo amemaliza kidato cha
nne 2015 Shule ya Sekondari Arusha Day
na si 2011 kama inavyotajwa mitandaoni
kwa malengo ovu.
3. Diana hajawahi kujiunga na Elimu ya
Chuo Kikuu chochote Tanzania au duniani
bali anatarajia kujiunga mwaka huu
katika chuo cha IFM kusomea masula ya
kodi ngazi ya stashahada (cheti) ingawa
kulingana na ratiba zake na majukumu
yake mapya ikiwemo kushiriki Miss world
mapya huenda akaahirisha mwaka wake
wa masomo.
4. Tunawasihi watanzania kutumia vyema
mitandao ya kijamii na si kufanya
"Character assassination" lakini pia
tunaheshimu haki yao ya msingi ya kuhoji
masuala ya msingi kabisa kuhusu mtu
ambaye ni Public figure na ataliwakilisha
taifa katika anga za kimataifa.
Tumuunge mkono mlimbwende wetu ili
atuletee Taji la Dunia.
Ahsanteni.
Charles William
Kaimu Ofisa Habari wake.
(wilflow101@gmail.com)
Sunday, October 30, 2016
TAARIFA KWA UMMA KUHUSIANA NA UPOTOSHAJI WA TAARIFA ZINAZOSAMBAZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII JUU YA MSHINDI WA SHINDANO LA MISS TANZANIA 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment