Wednesday, October 19, 2016

Scopion afunguliwa mashitaka mengine

Mahakama ya Wilaya
ya Ilala, imemfungulia mashtaka
mapya Salum Njwete (Scorpion).
Amefunguliwa mashtaka mengine
yanayofanana na ya awali ya
unyang’anyanyi wa kutumia silaha.
Hata hivyo Njwete amekana shtaka
na kurudishwa rumande,huku
Hakimu Flora Haule anayesimamia
kesi hiyo akizuia dhamana.
Awali Mahakama hiyo ilimfutia
mashtaka yanayomkabili Scorpion
baada ya upande wa mashtaka
kuomba shtaka hilo liondolewe
mahakamani kwa sababu hawana
nia ya kuendelea na kesi hiyo na
Kutokana na maombi hayo, Hakimu
Adelf Sachore alikubaliana na ombi
hilo kwa kuzingatia kifungu namba
91 kifungu kidogo cha kwanza cha
sheria ambacho kinampa Mamlaka
Mkurugenzi Wa Mashtaka nchini
(DPP) kuondoa shtaka mahakamani
muda wowote ili mradi kama kesi
hiyo haijatolewa hukumu.
Lakini kifungu hicho kinampa
Mamlaka DPP kumshtaki upya
mshtakiwa huyo kama ana nia ya
kuendesha shtaka hilo.
Njwete anakabiliwa na shtaka la
unyang'anyi wa kutumia silaha na
kumjeruhi Saidi Mrisho.

No comments:

Post a Comment