Bondia mahiri na machachari ulingoni,
Thomas Mashalli, almaarufu 'Simba
asiyefugika', amefariki dunia usiku wa
kuamkia leo huko maeneo ya Kimara baada
ya kupigwa na watu wasiojulikana.
Imeelezwa kuwa bondia huyo alifika maeneo
ya Kimara katika moja ya baa na kuanza
kunywa bia na baadaye ukazuka ugomvi
baina yake na kijana mmoja aliyekuwa
maeneo hayo jambo lililofamfanya bondia
huyo kumwadhibu kijana huyo kwa kumchapa
mangumi.
Baada ya ugomvi huo, imeelezwa kuwa
kijana huyo alianza kupiga kelele huku
akimuitia mwizi bondia huyo, jambo
lililowafanya watu wasioujua ukweli wa tukio
hilo kufika eneo hilo na kuanza
kumshambulia bondia huyo kwa silaha
mbalimbali zikiwemo mapanga.
Baada ya watu hao kumjeruhi imeelezwa
kuwa waliamua kumburuza hadi barabarani
na kumtupa na kisha kumwacha akiugulia
maumivu.
Akizungumza na promoter
Kaike Siraju, amethibitisha kufariki kwa
bondia huyo aliyekuwa apande uliongoni
mwezi ujao huko mjini Morogoro.
bongohotz.com
Msiba wa bondia huyo upo maeneo ya
Tandale nyumbani kwa wazazi wake.
Bwana alitoa na bwa
Monday, October 31, 2016
Taarifa kamili ya kifo cha mashali
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment