Wednesday, October 19, 2016

Pitia hii kutoka viunga vya TFF

Kocha Khalfan Ngassa amekuwa kwenye benchi
la timu ya mpira wa miguu ya Toto Africans ya
Mwanza akiwa kocha msaidizi kwa mechi tatu
mfululizo za Ligi Kuu ya soka Tanzania bara
inayoendelea kwenye viwanja mbalimbali
nchini.
Khalfan Ngassa aliongoza timu kwenye mchezo
Na. 62 dhidi ya Kagera Sugar Oktoba 7, 2016;
mchezo Na. 67 dhidi ya Mbao FC uliofanyika
Oktoba 12, 2016 na Mchezo Na. 79 dhidi ya
Majimaji ya Songea uliofanyika Oktoba 15,
mwaka huu.
Kwa mujibu wa Kanuni ya 72 (3) (5) ya Ligi Kuu,
Kocha Mkuu anatakiwa kuwa na Leseni ya chini
kuanzia Daraja B ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Barani Afrika (CAF) na Daraja C kwa
Kocha Msaidizi pia kutoka CAF.
Idara ya Ufundi ya Shirikisho la soka nchini
(TFF) limethibitisha kuwa Kocha Khalfan
Ngassa hana leseni yoyote kati ya hizo, hivyo
hastahili kukaa kwenye benchi la timu ya Toto
Africans kama kocha mkuu au kocha msaidizi.
Kitendo kinachofanywa na Toto Africans ni
ukikwaji wa kanuni na ni vema uongozi wa Toto
ukamwondoa Khalfan Ngassa kwenye benchi ili
kuepuka adhabu. Kipendele cha (7) cha kanuni
hiyo ya 72, inaelekeza adhabu kuwa inaweza
kutozwa si chini ya Sh 500,000 (shilingi laki
tano).
Pia tunazikumbusha klabu zote kuanzia msimu
ujao wa 2017/18 wa ligi kuu ya soka Tanzania
bara, kocha anayestahili kukaa kwenye benchi ni
yule mwenye leseni Daraja A kwa nafasi ya
Kocha Mkuu na angalau Leseni Daraja B kwa
kocha msaidizi.

No comments:

Post a Comment