Thursday, October 20, 2016

Mbinu mpya ya ufisadi yagundulika

DAR ES SALAAM
UAMUZI wa Ikulu kufuta mialiko ya viongozi
mbalimbali kushiriki kuzima Mwenge wa Uhuru
mkoani Simiyu umefichua namna fedha za
umma zinavyotafunwa kupitia malipo ya
masurufu (imprest) Raia Mwema likielezwa
kuwa saini moja ya kiongozi katika kitabu cha
wageni wizarani au idara yoyote ya serikali
inaweza kufanikisha uchotaji wa hata shilingi
milioni moja.
Raia Mwema limeelezwa na vyanzo vyake
mbalimbali kwamba umekuwa ni utamaduni
mkongwe kwa viongozi wengi wa umma kufuja
fedha kila wanapokuwa na safari za kikazi na
wamekuwa wakifanya hivyo kupitia masurufu na
kwa ustadi mkubwa wamekuwa wakikwepa
kunaswa katika kashfa za udanganyifu.

No comments:

Post a Comment