Kitendo cha askari polisi kumpigia saluti
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi
(CUF) anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili
wa vyama vya siasa, Profesa Ibrahim
Lipumba imezua gumzo la kuhoji uhalali
wake.
Askari huyo alionekana juzi akimpigia
saluti Profesa Lipumba katika eneo la
Buguruni ambapo mwanasiasa huyo
alienda kushiriki zoezi la usafi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Salum
Hamduni alipoulizwa kuhusu usahihi wa
askari polisi kuwapigia saluti viongozi
wa vyama vya siasa wasio wabunge
alijibu kwa ufupi, “sio sawa.”
Kwa mujibu wa Kanuni za Jeshi la Polisi
(PGO) namba 102, haiwataji viongozi wa
vyama vya siasa wasio wabunge kati ya
watu wanaopaswa kupewa salamu hiyo
ya jeshi yenye kuonesha heshima.
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani wa Serikali ya Awamu ya Tatu,
Kapteni John Chiligati aliwahi kueleza
Bungeni kuwa saluti ni ishara ya
kuonesha heshima kwa kiongozi mkuu
kwenye asasi za kijeshi.
Kapteni Chiligati alisema kuwa mbali na
viongozi wa kijeshi, viongozi wengine
wanaopaswa kupewa saluti ni wa
mihimili ya Serikali, Bunge na
Mahakama.
Wengine ni majaji wote, wabunge,
wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na
mahakimu wa mikoa na wilaya wakiwa
kwenye mahakama zao.
Katibu Mkuu wa Chama Cha CCK,
Renatus Muabhi alisema kuwa huenda
askari huyo alipiga saluti kwa kupaniki
kutokana na maagizo aliyopewa ya
kumlinda Profesa Lipumba katika zoezi
hilo.
Monday, October 31, 2016
Sakata Polisi aliyepiga picha na Lipumba la chukua sura mpya
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment