Thursday, October 20, 2016

Wanachuo 600 kukosa mkopo

Dar es Salaam.

Ahadi iliyotolewa na
Rais John Magufuli wakati wa
kampeni mwaka jana kwamba katika
Serikali yake hakuna mwanafunzi
atakayekosa mkopo wa masomo ya
elimu ya juu imekuwa ngumu
kutekelezeka.
Uchunguzi wa Mwananchi umebaini
kwamba kati ya wanafunzi 88,000
walioomba mikopo kutoka Bodi ya
Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya
Juu (HESLB), wengi hawatapata.
Uwezo wa bodi hiyo ni kutoa mikopo
kwa wanafunzi 21,500 pekee sawa
na asilimia 24 na waliopatiwa hadi
sasa ni wanafunzi 11,000 sawa na
asilimia 12.
Takwimu hizi zinaonyesha kwamba
zaidi ya robo tatu ya wanafunzi
wanaohitaji mikopo watakosa
kutokana na uwezo mdogo wa
kifedha.

No comments:

Post a Comment