Tuesday, October 18, 2016

Fuatilia makala hii kutoka mkono salama

La Norman ni Dili sio Dili??
Na: Kyaka kya Pakano.

Mwaka 2000 Dr. Hassy Kitine alichaguliwa kwa mara ya pili kama mbunge wa Maketekuwa ndio anaanza kipindi chake cha kwanza kama Mbunge. Hii ni kwasababu kipindi cha kwanza alikuwa amemalizia miaka 2 ya aliyekuwa mbunge wa wakati huo ambaye alifariki Hayati Dr. Tuntemeke Mesaka Nung'wa Sanga.

Kitine alijikuta anaianza awamu yake ya Ubunge kwa machungu. Akiwa amejitwalia ujiko kuwa ni mtu wa karibu kabisa na Rais wa wamu ya Tatu, Ben Mkapa, Kitine aliteuliwa mara moja kuwa Mkuu wa mkoa wa Tanga, akateuliwa kuwa waziri  ofisi ya Rais anayesimamia utawala bora.

Lakini kabla jina la Kitine halijachanua sawa sawa mara mingong'ono kuwa anahusishwa na kashfa. baadaye ikaja ikaja kuwekwa wazi, Gazeti ambalo lilikuwa maarufu wakati huo la RAI likatoka na article Kitine amepiga deal la milioni 60 kwa kusingizia kuwa Mke wake anaenda kutibiwa Ulaya kumbe sivyo.

Kashfa ya ufisadi ya Kitine ikafika Bungeni, ikajadiliwa, Kitine alikataa kata kata kuwa hakuhusika na kashfa hiyo, lakini baadaye maji yalizidi unga, Mh. Kitine akawa hana namna bali kujiuzuru nafasi ya Ukuu wa Mkoa, akapigwa chini pia na nafasi ya Uwaziri katika ofisi ya Rais. Hatujakaa sawa muda wa uchaguzi ulipofika kitine akapoteza kiti cha ubunge katika kura za maoni kwa mtu ambaye hakuwa maarufu wakati huo Binilith S Mahenge.

Miaka 15 baadaye nimekuwa nikijiuliza kama Historia inaweza kujirudia? Mh. Norman Sigalla ambaye naye hajakaa muda mrefu amekuwa akiandamwa na jinamizi la kashafa za ufisadi.

Kwanza kulianza kusikika minong'ono ya chini chini kuwa Mheshimiwa kasajili chuo anachotumia kupigia madili ya pesa chafu kwenye taasisi anazozisimamia. Mheshimiwa alikanusha habari hizo.

Lakini kabla hiyo haijapoa, kama ilivyokuwa wakati wa Kitine, Gazeti maarufu la wakati huu " mwananchi" linaibuka na kashfa kuwa Mh. Alipiga dili chafu la karibu milion 5 kila mwezi kwa kipindi cha miezi 5 kama mfanyakazi hewa.

Sio nia yangu kuthibitisha hayo kama yametokea au kukanusha, ninachotaka kusema ni kuwa naona kama Mh. Normana anatembea njia inayofanana na Njia ya Kitine.

Lakini kuna mambo ya kujiuliza, kwa mujibu wa maelezo ya katibu tawala wa Mkoa inasemekana kuna kijana wa idara ya Utumishi pale mkoani alirudisha jina la Normana kwenye system. Na kijana huyo amechukuliwa hatua za kinidhamu. Hapa Songea wanasema jamaa akasimamishwa kazi na anasubiri kupelekwa mahakamani.

Sasa swali tunalojiuliza vijiweni, huyu kijana aliingiza jina la Norman Sigalla ili iweje?

Angekuwa ameingiza alafu akatengeneza akaunti fake achukue pesa tungesema basi huyu kijana alitaka kuiba pesa, lakini hakufanya hivyo, aliingiza jina pamoja na account namba zote za Mh. Norman Sigalla bila shaka huyu kijana alilenga kuw apesa zimfikie Norman Sigalla

Baadhi yetu tunadhani kuwa huenda yule kijana alikuwa ameingiza jina lile kimakosa. Lakini cha kushangaza ni kuwa baada ya jina kuingizwa Mkoani lilihitaji kupitishwa na maofisa wa wizara ya Utumishi, jina lilifika kule likapitishwa. Baada ya kutoka wizara ya Utumishi jina lilitakiwa liende Hazina lipate checque namba na kulipangia mshahara, jina likaenda hazina (wizara ya Fedha) likapata Cheque namba na kupangia mshahara.
Baada ya hapo mshahara ukaanza kutiririka. Kosa la Norman alipoona mshahara unaingia akajisemea kale kamsemo ketu ka kitoto, "Cha kuokota si cha kuiba, mwenye mali ni mzembe" akawa anapiga zile pesa kimya kimya, bila kumwmabia mtu. Ukizingatia alikuwa ametokea kwenye uchaguzi akaona hapa ndio pa kuzibia matobo ya mfuko yaliyotoboka wakati wa uchaguzi. KOSA LA KWANZA. Akapiga 4,600,000 kila mwezi kwa miezi 5 mpaka Rais alipowashtua kuwa kuna watu wanakwiba pesa za umma kwa mishahara hewa.

Baada ya hili dili kushtukiwa katibu tawala wa Mkoa akamuandikia Katibu wa  Bunge Dkt. Thomas Kashilila kumfahamisha kuwa mbunge wake anatuhumiwa kukwapua hizo pesa. Katibu wa Bunge akampa Norman Soft terms kuwa akakae na uongozi wa mkoa wakubaliane ili hizo pesa zikatwe kwenye mshahara wake wa ubunge na kurudishwa kimya kimya Hazina. Hapa inaonesha bunge lilitaka kumbeba Norman, waue soo hili kimya kimya.

Sijui nini kilikuwa kimemsibu kaka yangu Norman, maana lipigwa upofu hakuiona hii ofa, wengine wanasema Mheshimiwa ana kiburi san ahata akiona ushauri wa wazi kutokana na tabia yake ya kujiamini huwa anaupuuza, Akaupuuza ushauri huu. Kama angefuata ushauri huu, maana yake angekuwa amerudisha pesa kimya kimya na hakuna ambaye angekuja kujua. Kukataa Ushauri wa kuwa akapige magoti mkoani arudishe pesa hizo ni KOSA LA PILI.

Jambo linguine ambalo Norman angefanya ilikuwa baada ya kusikia kuwa Rais ametangaza kusaka wafanyakazi hewa na yeye jina lake linatajwa alitakiwa ashtuke ajifanye ndio kwanza ameona pesa kwenye akaunti yake, aitishe vyombo vya habari awalalamikie ofisi ya Mkoa, wizara ya Utumishi na hazina (wizara ya fedha). Maana yake nini? Kama angejitokeza wazi hadharani mapema aseme jamani kuna mtu kaweka pesa kwenye akaunti yangu simjui ni nani? Ingemfanya angalau ajisafishe aonekane hakuhusika na kusuka dili la kumpa mshahara wa Mkuu wa wilaya. Kitendo cha Mh. Norman kuacha jambo hili liendelee lenyewe ni KOSA LA TATU.

Baada ya sakata hili kusikika kwenye vyombo vya habari leo, washabiki na wapenzi wa Mh. Norman wamesikika wakisema huu ni ugomvi wa kisiasa wa jimbo la Makete. Unajiuliza kwani Kitine alivyochafuka kwa ile kashafa alikuwa anagombea jimbo na nani? Uchaguzi ulikwisha na sasa Mbunge yupo kazini na mpinzani wake kapewa cheo kikubwa kuliko nafasi ya Ubunge, ni Mkuu wa Mkoa. Lakini embu tuone, Je ingewezekana Mehenge kufanya hii fitina. Gazeti linasema Jina la Norman liliingizwa kwenye mshahara mwezi wa 9 mwaka jana. Mahenge hakuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma. Alafu Rais ametangaza kusaka watumishi Hewa mwezi wa tatu  (Machi) Mahenge alikuwa bado hajateuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma wala hakujua kama atakuja kuwa mkuu wa Mkoa wa Songea. Habari za Mitaani zinasema kuwa Jina la Norman Limekuja kubainika kuwa yumo kwenye watumishi Hewa Mwezi wa 4 Mahenge alikuwa bado hajapewa nafasi ya Ukuu wa Mkoa. Sasa Mahenge aliingizaje jina la Norman kwenye ordha?? Kuendelea kujaribu kutafuta kisingizio cha kuonyesha watu kuwa Norman amebambikizwa kesi hii na Mahenge inampotezea direction ya kutafuta njia muafaka ya kutatua tatizo hilo. KOSA LA NNE

Norman aliposikia kuwa jina lake limetoka katika watumishi hewa alishauriwa kuwa matafute kijana aliyeliingiza lile jina ili yule kijana atoroke asionekane  hapa Songea. Lakini kwa hulka ile ile ya kujiamini Norman akasema hakuna haja ya kukimbia, waliamini hakuna mtu atajua yule kijana ndio aliingia kwenye mfumo na kuingiza jina kwenye data base. Baadaye msako ulivyoendelea yule kijana si akabambwa, mtandao ukaonyesha aliingia lini, na aliingiza jina lipi na lipi. Sasa yule kijana amesimamishwa kazi na anasubiri kupelekwa mahakamani. Sasa huyo kijana atakubalia aende mahakamni peke ake? Atakubali msala huu aubebe mwenyewe mwenyewe ukizingatia yeye hakula hizo pesa?? Kutokufanya utaratibu kabla msala haujasanuka kumsafirisha huyo mshikaji nje ya nchi ni KOSA LA TANO.

Inafact kuna makosa KUMI lakini kwa leo niishie hapa nisiwachoshe.

Sasa hivi issue ya Norman inategemea sana huruma za Rais. Ninasema inategemea huruma za Rais kwasababu, Rais akisema watuhumiwa wote wa makossa ya Utumishi hewa wapelekwe mahakamani, Unadhani atasema Muacheni Mh. Norman? Itakuwa double standard. Kama Norman ataruidisha pesa sasa kama ambavyo katibu wa Bunge alishauri, Je itakubalika? Watumishi wengine nao wataruhusiwa kurudisha pesa?? Mmmh sijui. Lakini Rais akisema waruidhse pesa, basi hiyo ndio pona yake.

Ninajua Norman ni mzoefu wa kupambana na majanga, nimtakie kila la Kheri.

No comments:

Post a Comment