Thursday, October 17, 2019
Wafanyabiashara Manyara wampongeza JPM
Wafanyabiashara mkoani Manyara, wameahidi kuendelea kulipa kodi kwa hiari baada kuridhishwa na utendaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Wafanyabiashara hao wamemweleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji aliyekutana nao Mjini Babati ili kujadili fursa na changamoto zinazoikabili sekta binafsi pamoja na kuwaelimisha namna Serikali ilivyofuta kodi lukuki kwa lengo la kuwawezesha kufanyabiashara zao kwa tija Zaidi.
Pamoja na ahadi hiyo ya kulipa kodi kwa hiari, wafanyabiashara hao wamemwomba Dkt. Ashatu Kijaji awasaidie kufikisha kilio chao kwa Serikali ili idadi kubwa ya taasisi za Serikali zinazowabana kulipa kodi zipunguzwe, ama kodi zinazodaiwa ziunganishwe ili kumwondolea mfanyabiashara adha ya kudhibitiwa na Mamlaka nyingi.
Baadhi ya Mamlaka zilizotajwa ni pamoja na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Wakala wa Usalama Mahali pa Kazi (OSHA) na nyingine nyingi ambazo wamesema mbali na kuwatoza kodi kubwa lakini wamekuwa wakipata usumbufu wa aina mbalimbai.
Akijibu hoja mbalimbali za wafanyabiashara hao, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amewapongeza wafanyabishara hao kwa kulipa kodi ambayo imeiwezesha Serikali kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya.
“Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii, mwezi Septemba, tumekusanya Zaidi ya shilingi trilioni 1.76 kiasi ambacho hakijawahi kutokea tangu nchi ipate uhuru” alisema Dkt. Kijaji
Alisema kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya ufanyajibiashara ambapo mpaka sasa imeondoa Zaidi ya kodi 50 zilizokuwa zikiwakwaza wafanyabiashara lengo likiwa ni kuwawezesha kufanyabishara yao kwa ufanisi zaidi ili waendelee kulipa kodi
“Tumepunguza kodi nyingi sana!, Mwaka uliopita wa fedha (2018/2019) tulipunguza kodi 108 na mwaka huu wa fedha (2019/2020 tumepunguza kodi na tozo 54 kwa makusudi, Dkt, John Pombe Magufuli ameamua kuwawezesha watanzania, kila mmoja kwenye eneo lake la kazi afyanye kazi vizuri” alisisitiza
Aidha, Dkt. Kijaji aliwataka wafanyabiashara waliopata msamaha wa riba kwenye kodi mbalimbali walizokuwa wanadaiwa, walipe madeni yao kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa na kwamba hakutakuwa na muda mwingine utakao ongezwa.
Aliwataarifu wafanyabiashara hao kwamba Serikali imesitisha kwa muda utoaji fedha kwenye miradi mikubwa ya kimkakati iliyopangwa kutekelezwa na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI yenye lengo la kuziwezesha Halmashauri kujitegemea kimapato hadi pale mfumo madhubuti wa kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo utakapo wekwa.
Dkt. Kijaji alitoa kauli hiyo baada ya kupokea maombi kutoka kwa Mbunge wa Babati Mjini Mhe. Pauline Gekul, aliyeomba shilingi bilioni 5.5 kutoka Serikalini kwa ajili ya kujenga kituo cha mabasi ili kuboresha mazingira ya biashara na utoaji huduma kwa wananchi.
Kwa upande wake Naibu Kamishna Operesheni ya Kodi Bw. Simon Kingu, alisema TRA iko tayari kushirikiana na wafanyabishara na kuhakikisha wanatatua kero zao ili walipekodi kwa hiari kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Alisema juhudi kubwa inayofanywa na Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya kuifikisha nchi katika uchumi wa kati wa viwanda unategemea mchango mkubwa wa wafanyabiashara katika kulipa kodi stahiki.
Wednesday, March 29, 2017
Pitia hii
Friday, March 10, 2017
Ripoti ya Dawa ya Ukimwi kugundulika Nchini Israel
MAMILIONI ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) ulimwenguni, sasa wanaweza kupata tumaini jipya baada ya wanasaynsi wa nchini Isreali kugundua dawa ambayo inasemekana kuwa na uwezo mkubwa wa kutibu Ukimwi.
Wanasayansi hao kutoka Chuo Kikuu cha Hebrew kilichopo Jerusalem nchini Israeli wamegundua dawa yenye protini ambayo wanadai inaweza kupunguza virusi vya Ukimwi kwenye mwili wa mgonjwa kwa asilimia 97 ndani ya siku saba tu, hii ni kwa mujibu wa gazeti la Times la Israel.
Ugunduzi huu mpya sasa unatoa tumaini jipya katika utafutaji wa dawa ya ungonjwa huu ambao mpaka sasa hauna tiba ukiwa umeshaua watu zaidi ya milioni moja kwa mwaka 2015 pekee.
Virusi vya Ukimwi hushambulia chembe chembe nyeupe za damu zinazojulikana kama CD4 ambazo husaidia kupigana na magonjwa yanayoingia mwilini.
Virusi vya Ukimwi huingia ndani ya chembe chembe hai nyeupe na kujizalisha kwa wingi jambo ambalo husababisha uharibifu wa CD4.
CD4 zinapokuwa chini ya 200 kwa kyubiki milimita za ujazo wa damu, mgonjwa anahesabika kuwa tayari ameanza kuugua Ukimwi.
Ugunduzi huo mpya umehusisha majarabio ya dawa hiyo mpya ambayo iliwekwa kwenye damu ya wagonjwa 10 wa Ukimwi iliyokuwa kwenye chupa maalumu kwa ajili ya majaribio.
Sehemu kubwa ya dawa hiyo ambayo ilipewa jina la Gammora na watafiti, ilisababisha uzalishaji wa DNA ya virusi hao ndani ya CD4 iliyoathirika kujizalisha kwa wingi badala ya utaratibu wa kawaida ambao huzalisha moja au mbili.
Hii inasababisha chembe chembe nyeupe zilizojeruhiwa kujiharibu zenyewe na kuzifanya zishindwe kusambaza virusi zaidi.
Majarabia yanahusisha dawa hii mpya ya Gammora yataendelea kukiwa na matumaini makubwa kuwa itaweza kuua asilimia 100 ya seli zilizoathiriwa na Virusi vya Ukimwi.
Abraham Loyter mmoja ya wagunduzi wa dawa hiyo mpya, aliliambia gazeti moja la Israeli kuwa ugunduzi huo mpya unaleta tumaini jipya.
“Tunachokifanya sisi ni kuharibu seli ambazo zimeathirika na kwa hiyo zitakufa moja kwa moja na hazitaweza kusambaza tena virusi,” anasema.
Katika hatua nyingine, Wizara ya Afya ya Israeli ilitangaza kwa mara ya kwanza kugawa dawa zenye uwezo wa kuzuia maambukizi kwa makundi yenye hatari zaidi ya kupata maambukizi mapya. Dawa hizo zinazojulikana kama prophylactic drugs zinapomezwa mara kwa mara zimeonyesha uwezo mkubwa wa kuzuia maambukizi.
Kwa sasa, dawa pekee kwa watu wenye virusi vya ukimwi, ni dawa za kupunguza makali ambazo humezwa kila siku ambazo pia hupunguza uwezekano wa maambukizi mapya.
Historia inaonyesha kuwa VVU ilitokea kwa nyani waliopo katika Afrika ya kati katika miaka ya 1900. Kutokana na mwingiliano kati ya tamaduni tofauti na mataifa, vilianza kusambaa duniani.
Ukimwi uligundulika nchini Marekani miaka ya 1980 na ulijulikana kama Ukosefu wa Kinga kwa Mashoga (GRID). Kadiri muda ulivyokwenda, wagonjwa wengine watano waligundulika nchini humo, wote wakiwa ni mashoga mwaka 1981.
Wakati watafiti na wanasayansi wakiendelea kuumiza vichwa kupata majibu ya dawa ya ugonjwa huu unaendelea kugharimu maisha ya mamilioni ya watu kote ulimwenguni kila mwaka, bado tiba au kinga yake ya uhakika imekuwa mtihani mkubwa ambao hadi sasa hakuna aliyeufaulu. Hata hivyo, wugunduzi huu wa wanasayansi wa Israeli unaweza kubadilisha matokeo.
Nchi za Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini zina asilimia ndogo mno ya maambukizi yanayokadiriwa kuwa 0.1. Hii ni tofauti na nchi za Kiafrika zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo karibu asilimia tano ya watu wake wanakadiriwa kuwa wameaambukizwa VVU.
Kwa sasa tuna watu 7,500 ambao wanaishi na VVU hapa Israeli,” anasema Dk. Margalit Lorber ambaye anafanya kazi kwenye kituo cha Afya cha Haifa's Rambam kinachoshughulika na magonjwa yanayotokana na upungufu wa kinga ya mwili. Wagonjwa wapya 450 huripotiwa kila mwaka,” anaeleza.
Wakati asilimia ya watu walioathirika na VVU nchini Israel ikiwa ni asilimia 0.1, nchi hiyo ilianza tafiti kuhusiana na ugonjwa huo miaka 1990 wakati kulipokuwa na msukumo mkubwa duniani juu ya utafiti wa VVU na Ukimwi.
Wanasansi walioshiriki katika utafiti wa dawa hiyo mpya wanasema, majaribio ya ufanisi wa dawa hiyo yataanza ndani ya kipindi cha mwaka mmoja na wanatarajia kuifanya tiba hiyo kuwa ya gharama nafuu kuliko dawa zozote za ugonjwa huo.
Thursday, March 9, 2017
Siku ya wanawake duniani. mbinga wanawake watakiwa kudhubutu kwenye viwanda
Na Riziki Manfred Bonzuma
Mbinga
Wanawake kote nchini wametakiwa kuwa mfano katika jamii kwa kufungua fursa katika sekta ya viwanda kwani mwanamke ni kiungo mhimu katika maendeleo nchini
Akisoma hotuba kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Mbinga Afisa tarafa ya Mbinga mjini ndugu Eniard Nguguru katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kiwilaya yalifanyika Katika kata ya Wukilo ambapo amesema katika kuelekea Tanzania ya viwanda wanawake wanatakiwa kufungua fursa kwenye sekta ya viwanda na kuacha kutegemea kila kitu kifanywe na Wanaume pia ameitaka jamii kutofumbia macho vitendo vya udhalilishaji na ukatili kwa wanawake ikiwemo ubaguzi na unyanyanyasaji
Aidha ndugu Eniard Nguguru amesema moja ya changamoto zinazo wakabili wanawake ni unyanyanyasaji na ubaguzi hasa katika mgawanyo wa wa mali pindi wanawake wanapo ondokewa na waume zao "lazima jamii ibadilike kumekuwa na vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake huku jamii iliendelea kufumbia macho vitendo hivyo kwa kuto lipoti katika vyombo husika" alisema Nguguru
Awali wakisoma lisala kwa mgeni rasimi wanawake wa wilaya ya Mbinga wameiomba wilaya kuendelea kuwawezesha wanawake kwa kuwaongezea mikopo ili wapate mitaji na kuinua maendeleo ya mwanamke kwa kuwekeza kwenye kilimo na ufugaji pia wameviomba vyombo vya dola na mahakama kusimamia na kuwatia nguvu wale wote watakao bainika kufanya ukatili wa aina yoyote ile kwa mwanamke
Vitendo vya kikatili na udhalilishaji vimeongezeka kwa mwaka 2016 ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo halmashauri ya Mbinga vijijini pekee zaidi ya kesi 26 zimelipotiwa katika vyombo vya kisheria ikiwemo mahakama na dawati la jinsi katika ofisi ya maendeleo ya Jamii
Siku ya wanawake duniani hufanyika kila mwaka kote duniani kwa lengo la kuendelea kupinga vitendo kandamizi kwa kwa wanawake na kauli mbiu mwaka huu ni Tanzania ya viwanda wanawake ni msingi wa mabadiliko ya kiuchumi.
Monday, March 6, 2017
Prof.Lipumba amemteua Naibu Katibu Mkuu Bara huku mgogoro wa Uongozi ndani ya Cuf ukiendelea kufukuta
Mgogoro wa Uongozi ndani ya Prof.Lipumba amemteua Naibu Katibu Mkuu Bara huku mgogoro wa Uongozi ndani ya Cuf ukiendelea kufukuta Chama cha wananchi Cuf umeendelea Kufukuta ambapo M/kiti wa Chama hicho Prof.Ibrahim Lipumba amemteua Naibu Katibu Mkuu Bara Magdalena Sakaya kukaimu nafasi ya Katibu Mkuu Maalim Seif shariff Hamad baada ya Maalim Seif kukaidi wito wa M/KIti wake kwenda ofisi Kuu Buguruni kwa zaidi ya mara nne.
Prof Lipumba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam pamoja na wafuasi wa chama hicho amesema Maalim Seif amekaidi wito wa kwenda Makao makuu Buguruni tangu Septemba 23 mwaka jana kwa ajili ya kusimamia mkutano wa kamati ya Utendaji ambao ulitakiwa kujadili mambo kadhaa ya chama hicho.
Aidha Prof. Lipumba amewavua madaraka wakurungezi kutoka zanzibar akiwemo Salim Bimani aliyekuwa Mkurugenzi wa habari na Uenezi, Omar Ali Salehe Mkurugenzi Mipango na Uchaguzi, Abdallah Bakar Khamis Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi, Pavu Juma Abdallah – Haki za Binadamu, Mahima Ali Mahima Katibu Mtendaji JUvicuf pamoja na Yusuph Salim Naibu Mkurugenzi Ulinzi na Usalama Cuf wote kutoka Znz.
Chama cha wananchi Cuf kimekumbwa na mgogoro wa uongozi tangu Prof.Lipumba alipotanga kujiuzuru uongozi wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu 2015,ambapo baadae alitangaza kurudi na kufanyika mkutano mkuu ambao ulivurugika na kusababisha mpasuko kati ya Cuf bara na cuf Zanzibar.
SMZ yachanganyikiwa kutokana na agizo la Rais Magufuli
Dar es Salaam/Zanzibar. Wakati Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) likijipanga kuikatia umeme Zanzibar kama alivyoagiza Rais John Magufuli, SMZ inajipanga kuzungumza na shirika hilo ili kuona namna ya kulipa.
Alipotafutwa kwa simu jana kuzungumzia utekelezaji wa agizo hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Dk Tito Mwinuka alisema yupo safarini na hakuzungumza kutokana na mawasiliano kuwa mabaya. Baadaye mwandishi wetu alimtumia ujumbe mfupi, lakini Dk Mwinuka hakujibu.
Baada ya kukwama kupata maelezo ya Dk Mwinuka, mwandishi wetu alimtafuta kwa simu, Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji ambaye alisema shirika hilo litatekeleza agizo la Rais kama alivyoagiza. “Rais ametoa kauli na kuagiza… lazima tutekeleze,” alisema Muhaji ambaye hakubainisha siku ya kuanza utekelezaji wa agizo hilo.
Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa SMZ, Mohamed Aboud Mohamed alipoulizwa kuhusu deni hilo, alisema wamejiandaa kufanya mazungumzo kati ya mawaziri husika wa pande mbili za Muungano kuona namna wanavyoweza kufanikisha ulipaji wa deni hilo.
“Lengo letu ni kulipa deni lote kwa sababu ukidaiwa lazima ulipe. Tupo tayari kulipa ndiyo maana tumeanza kufanya mazungumzo na wenzetu wa Tanzania Bara, ili kuona namna tunavyoweza kukubaliana juu ya Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco) kulipa hatua kwa hatua ili kumaliza deni lote,
Klabu ya Chelsea Wakubaliwa Kujenga Uw.anja Mpya Wa Kisasa Ambao ni ghali zaidi
Meya wa jiji la London hatimaye amepitisha mpango wa kuendeleza uwanja wa Stamford Bridge unaotumiwa na klabu ya Chelsea ambao utagharimu kiasi cha paundi milioni 500 na kuufanya kuwa uwanja wa kisasa ambao utakuwa na uwezo wa kuingiza jumla ya washabiki 60000.
Chelsea walipewa ruksa ya kuanza mipango ya maendeleo ya uwanja huo na Hammersmith pamoja na halmashauri ya mipango ya Fulham na kamati ya maendeleo mwezi Januari na huku ikiwa ilitegemewa kupatikana sapoti ya meya wa London, Mayor Sadiq Khan kukubali kwake imekuwa ni hatua kubwa kwa timu ya kusimamia mpango huo wa maendeleo uliopo chini ya mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich.
Katika ujumbe wake, Khan alisema: “London ni moja ya majiji yanayojihusisha na michezo kwa kiasi kikubwa na nina furaha kuwa karibuni tutaongeza uwanja wa Chelsea kama moja ya viwanja vinavyovutia vya michezo.
“Baada ya kutizama kwa umakini mpango wenyewe, nimeridhika kuwa huu ni mtindo wa kipekee uliochaguliwa na unaovutia ambao pia utaongeza idadi ya watizamaji huku pia ukihakikisha kuwa washabiki wanaweza kupata njia rahisi za usafiri.
“Nina imani kuwa uwanja huu mpya utakuwa kama kito katika jiji la London na utajivika taji la kuwa kiwanja bora cha michezo huku pia kikiwa kivutio kikubwa cha wageni na washabiki wa soka duniani kote.”
Kupitia tovuti yao, Chelsea walionyesha kufurahishwa na maamuzi ya Khan na kuongeza kuwa hii ni hatua kubwa kuelekea mpango wa kuendeleza uwanja huu na kupanua huduma za kijamii kwa ujumla.
“Kuna hatua nyingi zaidi mbele yetu, yote kabla na baada ya mipango iliyopo, kabla ya matengenezo hayajakamilika tunaweza kuanza kazi. Tunaendelea kushirikiana na wadau na tutatoa taarifa zaidi juu ya maendeleo kwa ujumla.
Pamoja na ongezeko la gharama za uharibifu utakaojitokeza Stamford Bridge na ujenzi wa uwanja mpya wenye uwezo wa kubea watu 60,000, Chelsea imetuma ombi linalohusu uwekezaji wa kiasi cha paundi milioni 12 kwenye shughuli tofauti za kijamii na kiasi cha paundi milioni 3.75 kwenye makazi yenye unafuu katika maeneo ya Hammersmith na Fulham.
Mpango huo unamaanisha kuwa Chelsea itabidi wahamie kwenye uwanja wa nyumbani wa muda ikitegemewa kuwa uwanja wa Wembley kwa miaka 3 wakati Stamford Bridge ikiwa inaharibiwa ili uwanja mpya upate kujengwa, huku makadirio ya sasa yakiwa kukamilika kwake kuwa msimu wa 2021-22.
***************
Mbunge Godbless Lema - Nilipokuwa Gerezani Nilimuombea Sana Rais Magufuli
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amesema hana kinyongo wala uadui na mtu yeyote kuhusu hatua ya serikali kumweka mahabusu kwenye gereza la Kisongo kwa muda wa miezi 4 kwa kukosa dhamana.
Kauli hiyo aliitoa Jumapili hii mjini Arusha wakati akizungumza katika ibada ya kwenye Kanisa la Winners Chaple, ambapo alitoa sadaka na shukrani kwa Mungu na waumini wa kanisa hilo.
Alisema amefurahi kwa sababu Mungu alimpa likizo muhimu kwa kumpendelea kwa kuwa mbunge wa kwanza kula Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya akiwa gerezani.
“Nimeomba sana, nimewaombea sana nikiwa gerezani na sikuwa najua nina uwezo wa kuomba masaa manne ila nimemhubiri Mungu sana gerezani nimeombea taifa, viongozi, Bunge, Mahakama, Ofisi ya DPP na Rais Dk. Magufuli,” alisema.
Aliongeza “Ukweli kabisa sina adui kwenye jambo hili na sina kinyongo kwenye jambo hili, ni mara ya kwanza nilimuona mke wangu akinitetea gerezani kwa hiyo mimi nilipendelewa kuliko ninyi na hamtakaa mlie Krismasi gerezani, mkimjua Mungu alivyonibadilisha kupitia gereza mtatamani muende gerezani,”
Lema aliwaeleza waumini hao kuwa Yusuph alisema wao walimkusudia mabaya lakini Mungu alimkusudia mema huku akinukuuu andiko lake la shukrani kutoka katika Biblia kitabu cha Luka 6: 27-28 na kusema kuwa hakuna mbegu dhalimu inayopandwa itakayovuna rehema.
“Lakini nawaambia ninyi mnaonisikia wapendeni adui zenu,watendeeni mema wale ambao wanawachukia ninyi, wabarikini ambao wanawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wanawaonea ninyi,” alinukuu kitabu hicho.
**************
Friday, March 3, 2017
Hispania yateua waziri wa maswala ya ngono
Katika juhudi za kuongeza idadi ya watu inayoendelea kupungua, nchini Uhispania sasa serikali imeamua kumteua waziri wa masuala ya ngono.
Waziri mkuu wa nchi hiyo Mariano Rajoy amethibitisha uteuzi wa Edelmira Barreira kuwa afisa mkuu wa masuala ya ngono.
Hatua ya kubuni wizara nzima ya maswala ya ngono na mahaba huko Uhispania imetokana na hofu waliyo nayo wanasiasa.
Wakati kwengineko duniani watu wana hofu kwamba idadi ya watu nchini mwao inaongezeka kushinda rasilmali zilizopo , huko Spain hofu ni kwamba idadi ya watu inapungua, tena kwa kasi ya Katika juhudi za kuongeza idadi ya watu inayoendelea kupungua, nchini Uhispania sasa serikali imeamua kumteua waziri wa masuala ya ngono.
Waziri mkuu wa nchi hiyo Mariano Rajoy amethibitisha uteuzi wa Edelmira Barreira kuwa afisa mkuu wa masuala ya ngono.
Hatua ya kubuni wizara nzima ya maswala ya ngono na mahaba huko Uhispania imetokana na hofu waliyo nayo wanasiasa.
Wakati kwengineko duniani watu wana hofu kwamba idadi ya watu nchini mwao inaongezeka kushinda rasilmali zilizopo , huko Spain hofu ni kwamba idadi ya watu inapungua, tena kwa kasi ya kutisha.
Mbali na kwamba wengi ya wanandoa huko nchini humo wanashiriki zaidi mbinu na mipango ya uzazi pia kutokuwa na nafasi muafaka wa wanandoa au hata wapenzi kuonana kimwili, kuna laumiwa kwamba ndiko kulikosababisha idadi ya watoto wanaozaliwa kupungua mno.
Takwimu za hivi karibuni za Umoja wa Mataifa zinaorodhesha Uhipania kama moja wapo ya mataifa yanayoongoza kwa kuporomoka kwa idadi ya watoto wanaozaliwa.
Nae waziri wa elimu hivi majuzi amewasilisha ripoti yake kwa serikali na baraza la mawaziri akilalamika kwamba madarasa ya shule hayana idadi ya kutosha ya watoto na akaonya kwamba hili huenda likaathiri Uhispania kiuchumi katika miaka ijayo.
Katika kushghulikia swala hilo kwa haraka waziri mkuu wa taifa hilo Mariano Rajoy amemteua Bi Edelmira Barreira kuwa waziri wa maswala ya ngono na mahaba
Kazi kubwa ya waziri huyo mpya ni kuja na mbinu za mikakati ya kuwahamasisha na kuuchochea umma wa Uhispania kurudi vitandani na kusaidia kutengeneza watoto ili kuijaza tena Uhispania. .
Mbali na kwamba wengi ya wanandoa huko nchini humo wanashiriki zaidi mbinu na mipango ya uzazi pia kutokuwa na nafasi muafaka wa wanandoa au hata wapenzi kuonana kimwili, kuna laumiwa kwamba ndiko kulikosababisha idadi ya watoto wanaozaliwa kupungua mno.
Takwimu za hivi karibuni za Umoja wa Mataifa zinaorodhesha Uhipania kama moja wapo ya mataifa yanayoongoza kwa kuporomoka kwa idadi ya watoto wanaozaliwa.
Nae waziri wa elimu hivi majuzi amewasilisha ripoti yake kwa serikali na baraza la mawaziri akilalamika kwamba madarasa ya shule hayana idadi ya kutosha ya watoto na akaonya kwamba hili huenda likaathiri Uhispania kiuchumi katika miaka ijayo.
Katika kushghulikia swala hilo kwa haraka waziri mkuu wa taifa hilo Mariano Rajoy amemteua Bi Edelmira Barreira kuwa waziri wa maswala ya ngono na mahaba
Kazi kubwa ya waziri huyo mpya ni kuja na mbinu za mikakati ya kuwahamasisha na kuuchochea umma wa Uhispania kurudi vitandani na kusaidia kutengeneza watoto ili kuijaza tena Uhispania.
Ratiba ya ligi kuu England EPL wikiendi hii
Ligi kuu ya Uingereza ndio ligi inayoongozwa
kufuatiliwa zaidi na mashabiki wa mchezo huo
duniani. Na wikiendi hii kuna mechi
zinazosubiriwa kwa hamu ikiwemo Liverpool
dhidi ya Arsenal na Tottenham Hotspur dhidi ya
Everton.
Godbless Lema : nitaiandika waraka kwa Rais Baada ya Kutoka Gerezani
Namshukuru sana Mwenyezi Mungu, Jamhuri ilikusudia mabaya kwangu lakini Mungu alikusudia mema kwetu, vilevile namshukuru sana mke wangu, kama ningepata fursa ya kuoa tena ningemuoa yeye.. Nikisema niongee ninachotaka kuongea, leo sitaweza, nimeandaa waraka kwa ajili ya mheshimiwa Rais na nitautoa huo waraka hivi karibuni katika siku ambayo tutawatangazia. Nimeona mateso mengi ya watu, mambo mengi ambayo nafasi hii haitoshi.
Godbless Lema: Mbunge-Arusha mjini
TIRA yatoa elimu umhimu wa Bima Makete
Na mwandishi watu
Makete
Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imetoa Elimu ya Bima kwa Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta Makete na Wananchi wa kijiji cha Tandala na kuwaeleza maana ya Bima na umuhimu wake kwa Mwananchi
Meneja wa Bima kanda ya Nyanda za juu kusini Bw. Hillard Maskini amesema Bima inaumuhimu Mkubwa katika kumsaidia mtu pale anapopatwa na Janga kama Ajali, Moto, Wizi n. k
Pia amesema Bima inalinda Biashara yako, kupata fidia ya Moto, ajali, Wizi ambapo Unaweza kupatwa na janga la aina hiyo kama ni MwanaBima utalipwa fidia yako
Mkoa wa Ruvuma wajipanga kuongeza ufaulu na kuongeza kitaifa
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mh Binilith Mahenge ameziagiza halmashauri na Kamati za shule mkoani humo kuhakikisha wanafunzi wanakula chakula cha mchana shuleni, pamoja na kuimarisha miundombinu katika shule zote zikiwemo nyumba za walimu.
Akifungua kikao cha tathimini ya elimu mkoa wa Ruvuma kilicho fanyika wilaya Mbinga mh Mahenge amesema moja kati ya changamoto zinazowasilishwa sababisha kushuka kwa kiwango cha elimu mkoani humo kutokana na wanafunzi wengi kutumia muda mwingi kufuata chakula majumbambani mwao na wengine kukosa kabisa, pia Mahenge aliwataka walimu wote kukaa katika vituo vyao vya kazi ili kupata muda wa kujiandaa zaidi
Aidha Mh Mahenge ameagiza tathimini ya madawati kutokana na ongezeko la idadi ya wanafunzi walioandikishwa mpaka sasa na baada ya tathimini utengenezaji wa madawati uanze kufanyika pamoja na kuanza ujenzi wa majengo yenye upungufu hususani nyumba za walimu kwa kutumia nguvu za wananchi ikiwemo kutumia Benki tofauti na halmashauri kupeleka vifaa vya kiwandani “vijiji wekeni mipango ya ujenzi wa wa majengo yenye upungufu kwa kutumia Benki tofauti na halmashauri kupeleka vifaa vya kiwandani hakikisheni changamoto moto za nyumba za walimu, vyoo, madarasa inakwisha kabisa”alisema Mahenge
Wakitoa michango baadhi ya wadau wa elimu wamezitaja changamoto zinazochangia kudhoofisha kiwango cha elimu mkoani humo ikiwemo Uhaba uhaba wa walimu katika mkoa huo huku wakizitaka mamlaka husika kufanya msawazo wa walimu na kuwa na uwiano sawa kwa shule zote sambamba na kuboresha masirahi ya walimu kwa kuwalipa malimbikizo ya madeni walimu wanayo idai serikali na pamoja na kuwapandisha madaraja walimu , "walimu wanaishi kwenye nyumba za nyasa watawezaje kufundisha watoto darasani" alisema Alfred Nguguru akiendelea bwana Nguguru ameomba serikali iliangalie suala la mimba shuleni kwa kuwatafutia mabweni wanafunzi "tunaomba pia wanafunzi wawe na mabweni(hosteli) hasa watoto wa kike hata kwa kupanga ili kupunguza mimba shuleni"
Kikao hicho cha tathimini ya elimu mkoa wa Ruvuma chenye lengo la kuhakisha inaongeza ufaulu katika mitiani ya mwisho sambamba na kutatua changamoto zinazo ikabili sekta ya elimu pamoja kutoa zawadi na vyeti kwa shule zilizo fanya vizuri na kutoa vivyago kwa shule zilizo fanya vibaya baada ya matokeo kuonesha kushika nafasi ya 8 kitaifa tofauti na mwaka jana ambapo mkoa huo ulishika nafasi ya 7
Wednesday, March 1, 2017
Njombe Mkuu wa wilaya amtandika Kofi mwenyekiti
Na Charles Sanga
Njombe
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Ruth Msafiri Amejikuta akimtandika makofi Mwenyekiti wa Mtaa wa Buguruni –Matalawe Emmanuel Ngelime mara baada ya kutokuwepo kwa maelewano baina ya viongozi hao wawili.
Mapema leo katika ziara ya kushtukiza ya mkuu huyo wa wilaya katika ofisi ya mtaa wa Buguruni Mjini Njombe kumeibuka hali ya Taharuki iliyomfanya mkuu wa wilaya kushindwa kuzuia hasira zake na kumtandika makofi mwenyekiti huyo.
Imebainika kuwa Mpaka sasa Mwenyekiti wa Mtaa huo Bwana Emmanuel Ngelime Anatumikia kifungo cha Nje cha Mwaka Mmoja kwa kosa la kujaribu kumbaka mwanamke mmoja mtaani kwake.
Mara Kadhaa Mkuu huyo wa wilaya amesikika akimtaka Mwenyekiti huyo kutojihusisha na maswala ya kazi kama kiongozi wa mtaa lakini Mwenyekiti Huyo amekuwa akikaidi kwa kuendelea kufanya kazi ili hali amekosa sifa ya kuwa Mwenyekiti.
Ziara ya mkuu wa wilaya imefuatia mara baada ya kupewa taarifa za kuwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo amehukumiwa kwa kifungo cha mwaka mmoja kwa madai ya kutaka kumwingilia kingono mwanamke mmoja mtaani hapo bila ridhaa yake .
Hata hivyo tafsiri ya sheria imeweka wazi kuwa kiongozi yeyote wa serikali atakae hukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi sita basi kisheria atakuwa amepoteza uharali wa kuwa kiongozi katika
nafasi yoyote kwa mujibu wa sheria.
Ajiua kwa kurazimiswa kunyonyesha mtoto
Na Furahisha Nundu
makete
Afariki Dunia kwa kukataa kunyonyesha na kumuacha mtoto wa kiume mwenye miezi mawili
Mwanamke mmoja Bi. Olida Sanga (19)amekutwa jana akiwa amekufa mto Luvanyina kijiji cha Isapulano kata ya Isapulano Wilayani Makete
Akizungumza na mwandishi wetu Mwenyekiti wa kijiji cha Isapulano mara baada za Mazishi ya Marehemu Olida,Bw. Mwatindi Mbilinyi amesema Marehemu wakati wa Uhai wake alikuwa analazimishwa kumnyonyesha mwanaye jambo ambalo huenda lilimkera na kuamua kuchukua maamuzi hayo
Inaelezwa kuwa Marehemu alikuwa anaugua ugonjwa wa kifafa kwa siku nyingi
Marehemu amemwacha mwanaye Mwenye Miezi miwili wa kiume ambaye kwa sasa analelewa na Ndugu zake wa Karibu
Wananchi walianzisha jitihada za kumtafuta mnamo jumapili saa 10 jioni na kwa bahati mbaya waliopoa maiti yake kwenye mto Luvanyina hapo jana saa 5:30 asubuhi
Tuesday, February 28, 2017
Soma Ujumbe huu, Usipuuzie usije ukaingia mkenge
KUTOKA JESHI LA POLICE:
USALAMA WA MAISHA YAKO
Usinunue simu za Android kwa mtu usiyemjua. Hiyo ni hatari kwani hujui huyo jamaa kaitoa wapi, mwisho wa siku unapewa kesi ya wizi au mauaji. Inawezekana simu hiyo iliibiwa kwa mtu aliyeuawa.
Usimpe mtu usiyemjua simu yako apige sehemu yoyote.
Unapoiona line njiani ipo chini, usitake kuiokota na kuiweka simuni mwako ujue ina shilingi ngapi ili uchukue salio.
Simu inapoibiwa au
mwenye simu kuuawa, line hutupwa, unapoiweka simuni mwako,simuyako inahusishwa na tukio hilo
Unapoweka salio, hakikisha karatasi ya vocha unaichana. Unapoitupa, watu wanaweza kufanya mauaji, wakachukua karatasi ya vocha ile na kuweka sehemu ya tukio au pale ulipoitupa kukatokea tukio na wewe kuhusishwa.
Usikubali kumsajilia mtu line yake kwa jina lako, hata kama baba yako, usikubali.
Kumbuka namba yako umesajiliwa, moja ya matukio hayo yakitokea na namba yako kuonekana, moja kwa moja unakuwa mtuhu-miwa namba moja.
Wengi wamepewa kesi za mauaji, wizi bila kujua. Polisi wapo kazini, wanapoona vidhibiti wanakuchukua kwani hawatojua kama umehusika au la. Kuweni makini ili usije kuingia matatizoni, simu yako, fedha zako, ukifanya kisicho sahihi kama uzembe, utaishia pabaya.
SIMU YAKO JEMBE LAKO
SHARE UJUMBE HUU UMPE ONYO NA MWENZAKO.
Monday, February 27, 2017
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye atuma salamu za pole shirikisho la
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye ametoa salamu za pole kwa Rais wa Shirikisho la Riadha nchini, Anthony Mtaka kufuatia kifo cha mshiriki kutoka nchini Kenya, Charles Rioba (36) aliyefariki katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika Februari, 26 mkoani Kilimanjaro.
Rioba alishiriki kwa hiari mbio zijulikanazo kama ‘run for fun’ za Kilometa 21, zilizohusisha wananchi mbalimbali wakiwemo pia viongozi wastaafu.
Lakini akiwa katika mbio hizo alianguka na kupatiwa huduma ya kwanza kisha kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) na baadae kufariki dunia.
Waziri Nape ametoa pole pia kwa waandaaji wa mashindano hayo na wote ambao wameguswa na msiba huo
MARUFUKU KULIMA KARIBU NA VYANZO VYA MAJI
Na Riziki Manfred,
Bonzuma, Mbinga
katika kuendana na sera ya mazingira wilaya ya Mbinga imepiga marufuku shuguri zote za kibanadamu zinazo endelea katika vyanzo vya maji na pembezoni mwa mito ili kunusuru mabadiriko ya hali ya hewa katika ukanda huu wa kusini mwa Tanzania.
Marufuku hiyo limetolewa na mkuu wa wilaya Mbinga Consimas Nshenyi ambapo amewaagiza mafias mazingira na viongozi wa vijiji kuhakikisha wanasimamia sheria ya mazingira inayo kataza shughuri bza kibinada ndani ya mita 60 kutoka chanzo cha maji na pembezoni mwa mto ambapo shughuli za kibinadamu ambazo mara nyingi zimepelekea kuharibifu mkubwa wa mazingira katika.
Pia Nsenyi amesema kwanzia sasa hakuna namna nyingine ya kufanya juu ya wanao haribu mazingira zaidi ya kusimamia sheria za mazingira “hatuwezi kuwavumilia wanao haribu mazingira kwani tuatakuwa tunajiangamiza wenyewe sheria zipo na zipo wazi hivyo kila mtu anatakiwa kufuata sheria na kuna uharibifu mkubwa wa mazingira kwa watu wachache kuamua kulima, kuanzisha viwanda jambo ambalo tusipo angalia tutakosa hata vyanzo vya maji jambo ambalo ni hatari” alisema Nsenyi.
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amepiga maruku kwa baadhi ya wafanya biashara kuwakopesha fedha wakulima kwaajiri ya kununulia pembejeo na baadae mkulima kulipa mavuno anayo yapata alimarufuka kama MAGOMA ambapo amesema kuwa ni kumfanya mkulima ashindwe kujikwamua katika kilimo kwani wamekuwa wakilipa mavuno tofauti na dhamani ya fedha aliyoichukua awali.”mtu anachukua shilingi elfu hamsini lakini analipa zaidi ya magunia matatu mpaka manne ukiangalia hikini kiwango kikubwa cha gunia moja laki moja magunia matutu ni shilingi laki tatu lakini mkulima alipewa elfu hamsini”alisema mkuu huyo wa wilaya
Aidha Nsenyi amewashauri wanachi kuacha kubweteka na MAGOMA badala yake wachape kazi na inapo bidi kupata pembejeo watumia taasisi za fedha kama benki ambazo mashart na vigezo vya benki vipo kisheria na ni vya wazi.
Baada ya tamko hilo la mkuu wa wilaya uchunguzi ulio fanya na mtandao huu ibebaini kuwa bishara hii bado inaumaarufu kutokana na wanajamii wa kutoka wilaya hii wanapenda mfumo huu kwani kipindi cha mavuno wanachi hutumia fedha walizo pata kwaajiri ya mambo mengine tofauti na kilimo ikiwemo ngoma za kihoda na mganda ambazo ni maarufu katika wilaya hii hususani kipindi cha mavuno
Friday, February 24, 2017
Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga vijijini yapani kurudisha hadhi ya elimu iliyo Anza kushuka katika wilaya hiyo
Wadau wa elimu na viongozi halmashauri ya Mbinga vijijini wamekutana kufanya tathimini ya elimu ikiwemo kushuka kwa ufaulu kwa wa elimu ya msingi miaka ya hivi karibuni
Wakizungumza katika kikao hicho baadhi ya wadau wa elimu wamezitaja changamoto zinazowasilishwa pelekea kushuka kwa elimu kuwa ni pamoja kutoboreshwa kwa masirahi ya walimu, upungufu wa walimu, ushiriki hafifu wa wazazi hususani kufuatilia maendeleo ya watoto wao na kuchangia shughuli za elimu
Pia wadau wameainisha changamoto zingine kuwa ni pamoja na kuto wahamisha walimu wakuu walio shushwa vyeo pamoja na kuongeza uwiano wa vitabu hasa vya kiada katika shule za halmashauri hiyo
Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga vijijini Gombo Samandito Gombo amesema halmashauri hiyo imejipanga kuhakikisha inaongeza ufaulu kimkoa na kitatifa hasa elimu ya msingi ambayo imeonekana kulegalega huku akiwataka walimu kuto fanya uzembe katika kufundisha ikiwemo utoro "sitakuwa na msamaha kwa walimu wanao acha kazi wanaenda kupiga boda boda ukiona nimekubaini nitakufukuza hata usiangaike kuniomba msamaha pia wapo walimu wanao kopa mpaka wanapiriliza muda wa kufundisha wanakimbia madeni waache mara moja" alisema Samandito
Awali katika maada za utangulizi mkuu wa Polisi wilaya ya Mbinga OCD Maganga amekemea baadhi ya wazazi kuwahusisha wanafunzi katika biashara ya dawa za kulevya na kuwataka viongozi ngazi ya vijijini na kata kutoa taarifa za wahusika wa biashara hiyo pamoja na wale wanao wapa mimba wanafunzi
Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya ya Mbinga Consimas Nshenyi amendelea kukazia maagizo yaliyo tolewa wa na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Binilith Mahenge wakati wa ziara yake wilaya Mbinga mapema mwaka huu juu ya uharibifu wa mazingira ikiwemo kufanya shughuli za kibinaadamu ndani ya mita sitini kutoka vyanzo vya maji pamoja na kuhakisha Benki tofauti zinatukamika katika kujenga majengo sio kukaa katika matanuru
Matokeo ya darasa la saba mwaka 2016 yanaonyesha kushuka kwa elimu katika halmashauri hiyo ya wilaya ya Mbinga baada ya kushika nafasi ya 8 katika mkoa wa Ruvuma kati ya Halamashauri 8 za mkoa huo
Hekari 50 za bangi zateketezwa Makete
Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher olesendeka, Mkuu wa wilaya ya Makete Veronica Kessy kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama wameteketeza mashamba ya bangi Katika kata ya Mlondwe wilayani Makete.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh. Christopher Olesendeka ateketeza Bangi zaidi ya Hekari 50 iliyokuwa ikilimwa kwa kilimo cha Umwagiliagi katika mapori yaliyopo kijiji cha Ng'onde kata ya Mlondwe Wilayani Makete
Kwa hisani ya kitulo Fm radio makete
Wednesday, February 22, 2017
Ujue Freemasonry kiufupi
Ni shirika ambalo mambo yake ni siri kuu. Mimi nilifanya utafiki kwenye mitandao, nikafatilia historia yao kama inavyoonyeshwa mara kwa mara kwenye makala za historia katika televisheni za magharibi pamoja na kuongea na watu waliofuatilia kwa karibu mambo yao.
Kwenye maelezo yao kwa nje Free masons wanajitangaza kama shirika zuri tu.
Naomba niorodheshe mambo machache niliyoambiwa kuhusiana na Freemasonry.
1. Ni kweli Freemasonry kama ilivyo maana yake kwanza ilkuwa ni kundi la mafundi waashi (masons) au wajenzi kuwa lugha nyingine. Walikuwa ni wataalamu waliobobea kwenye masuala ya ujenzi wa mahekalu na mabenki ya zama hizo zinazoitwa kwa kizungu (medieval times).
Niliambiwa walikuwa ni watunzaji wa pesa za kanisa katoliki. Kwani walikuwa wanajenga mahekalu(cathedrals) za wakatoliki na mabenki/ mahandaki ya kuhifadhia pesa pamoja na kuzikia(catacombs).
Niliambiwa wanaweza kujenga hayo maandaki kwa utaalamu mkubwa kiasi kwamba ukiingia ndani ya hayo mahandaki bila ramani unaweza ukashindwa kutoka hata unaweza kupotelea humo humo ndani usiweze kutoka tena. Hicho ndicho kilichokuwa ni kiwango cha utaalamu wao.
2. Kwa kuwa walikuwa ni waashi ndiyo maana alama zao ni vifaa vya ujenzi, Pima maji n.k
3. Inasemekana mji mkuu wa marekani (Washington DC) ulisanifiwa na kujengwa na Freemasons. Na inasemekana ni mji makini ambao umejengwa ukizingatia pembe tatu zenye nyuzi zinazowakilisha u freemason.
4. Ikatokea kipindi ambapo hawa freemasons wakaasi kwa kuanza kujishirikisha na mambo ya nguvu za giza. Wengine wanasema walianza kuiba pesa za kanisa katoliki, lakini ukweli halisi haujulikani. Kutokana na sababu hizi na zinginezo ambazo ni siri kati ya kanisa katoliki na freemasons, Freemasons wakafukuzwa kutoka ukatoliki.
Ndio maana hakuna maelewano kati ya freemasons na wakatoliki. Wakatoliki wakaanzisha shirika jingine badala ya hao freemasons lijulikanalo kama Jesuits.
Jesuit Fathers ni mapadri wa katoliki wa daraja la juu sana wenye elimu ya juu zaidi ambao hufanya kazi za siri za utawala na udhibiti ndani ya kanisa katoliki.
5. Kuhusu imani yao (freemasons) nikaelezwa kwa kifupi kuwa wanaamini Yesu na Lucifer ni mtu na ndugu yake. wanaamini kuwa Lucifer ndiye mwema na mzuri lakini wanaamini kuwa Yesu ndiye mwenye mabaya. alimfanyia hila Lucifer aonekane mbaya.
6. Kinachoendelea ndani yake kuhusiana na ibada zake ni siri kwani kuna daraja ambazo muumini wa freemason anapanda kutokana na kubobea katika imani ikiwa ni pamoja na kutunza siri zao. Ninajua kuwa daraja ya juu kabisa ni nyuzi ya 33 (33rd degree)
7. Ni watu wenye nguvu mno na mambo yao ni makubwa mno na siri zao ni nzito mno. Ndiyo maana haziko wazi.
Wafuasi wa kiwango cha chini wala hawajui shirika hili linahusika na nini manake hata wao hawaambiwi kitu. Kwa wafuasi wa daraja ya chini wanakwenda ku socialize tu. Yaani kwa wasio jua kitu kule kwenye lodge zao ni kama ywca au wmca au club hivi. Kwenye nchi kama marekani watu wasio jua siri wanachukulia kama sehemu za kusocialize tu.
8. Freemasonry inawekwa pamoja na makundi mengine makubwa ya siri, yanayoendesha ulimwengu mzima kwa nguvu za kiuchumi, siasa na mambo ya utawala.
Friday, February 17, 2017
Manati ya Kurusha Dawa za Kulevya Toka Mexico Yagunduliwa Marekani
Manati hiyo inaonekana kuundwa mahsusi kwa ajili ya kurusha dawa za kulevya hadi Marekani. Marekani imekuwa ikikabiliana sana na walanguzi wa mihadarati kutoka Mexico pamoja na wahamiaji. Rais Donald Trump ameahidi kujenga ukuta mrefu kuzuia hilo.
Vifurushi hivyo vilikuwa bado havijarushwa.
Video: Ndugu wa Masogange wakiondoka Kisutu baada ya kukosa matumaini ya ndugu yao
Wabunge wazuiliwa kukutana na mfalme wa Rwenzururu Uganda
Wabunge hao ambao wote ni kutoka chama cha upinzani cha FDC, wanasema kuwa ni kama ambaye mkubwa wao yuko katika kizuizi cha nyumbani.