Na Charles Sanga
Njombe
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Ruth Msafiri Amejikuta akimtandika makofi Mwenyekiti wa Mtaa wa Buguruni –Matalawe Emmanuel Ngelime mara baada ya kutokuwepo kwa maelewano baina ya viongozi hao wawili.
Mapema leo katika ziara ya kushtukiza ya mkuu huyo wa wilaya katika ofisi ya mtaa wa Buguruni Mjini Njombe kumeibuka hali ya Taharuki iliyomfanya mkuu wa wilaya kushindwa kuzuia hasira zake na kumtandika makofi mwenyekiti huyo.
Imebainika kuwa Mpaka sasa Mwenyekiti wa Mtaa huo Bwana Emmanuel Ngelime Anatumikia kifungo cha Nje cha Mwaka Mmoja kwa kosa la kujaribu kumbaka mwanamke mmoja mtaani kwake.
Mara Kadhaa Mkuu huyo wa wilaya amesikika akimtaka Mwenyekiti huyo kutojihusisha na maswala ya kazi kama kiongozi wa mtaa lakini Mwenyekiti Huyo amekuwa akikaidi kwa kuendelea kufanya kazi ili hali amekosa sifa ya kuwa Mwenyekiti.
Ziara ya mkuu wa wilaya imefuatia mara baada ya kupewa taarifa za kuwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo amehukumiwa kwa kifungo cha mwaka mmoja kwa madai ya kutaka kumwingilia kingono mwanamke mmoja mtaani hapo bila ridhaa yake .
Hata hivyo tafsiri ya sheria imeweka wazi kuwa kiongozi yeyote wa serikali atakae hukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi sita basi kisheria atakuwa amepoteza uharali wa kuwa kiongozi katika
nafasi yoyote kwa mujibu wa sheria.
No comments:
Post a Comment