Thursday, March 9, 2017

Siku ya wanawake duniani. mbinga wanawake watakiwa kudhubutu kwenye viwanda

Na Riziki Manfred Bonzuma
Mbinga

Wanawake kote nchini wametakiwa kuwa mfano katika jamii kwa kufungua fursa katika sekta ya viwanda kwani mwanamke ni kiungo mhimu katika maendeleo nchini

Akisoma hotuba kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Mbinga Afisa tarafa ya Mbinga mjini ndugu Eniard Nguguru katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kiwilaya yalifanyika Katika kata ya Wukilo ambapo amesema katika kuelekea Tanzania ya viwanda wanawake wanatakiwa kufungua fursa kwenye sekta ya viwanda na kuacha kutegemea kila kitu kifanywe na Wanaume pia ameitaka jamii kutofumbia macho vitendo vya udhalilishaji na ukatili kwa wanawake ikiwemo ubaguzi na unyanyanyasaji

Aidha ndugu Eniard Nguguru amesema moja ya changamoto zinazo wakabili wanawake ni unyanyanyasaji  na ubaguzi hasa katika mgawanyo wa wa mali pindi wanawake wanapo ondokewa na waume zao "lazima jamii ibadilike kumekuwa na vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake huku jamii iliendelea kufumbia macho vitendo hivyo kwa kuto lipoti katika vyombo husika" alisema Nguguru

Awali wakisoma lisala kwa mgeni rasimi wanawake wa wilaya ya Mbinga wameiomba wilaya kuendelea kuwawezesha wanawake kwa kuwaongezea mikopo ili wapate mitaji na kuinua maendeleo ya mwanamke kwa kuwekeza kwenye kilimo na ufugaji pia wameviomba vyombo vya dola na mahakama kusimamia na kuwatia nguvu wale wote watakao bainika kufanya ukatili wa aina yoyote ile kwa mwanamke

Vitendo vya kikatili na udhalilishaji vimeongezeka kwa mwaka 2016 ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo halmashauri ya Mbinga vijijini pekee zaidi ya kesi 26 zimelipotiwa katika vyombo vya kisheria ikiwemo mahakama na dawati la jinsi katika ofisi ya maendeleo ya Jamii

Siku ya wanawake duniani hufanyika kila mwaka kote duniani kwa lengo la kuendelea kupinga vitendo kandamizi kwa kwa wanawake na kauli mbiu mwaka huu ni Tanzania ya viwanda wanawake ni msingi wa mabadiliko ya kiuchumi.

No comments:

Post a Comment