Monday, March 6, 2017

Prof.Lipumba amemteua Naibu Katibu Mkuu Bara huku mgogoro wa Uongozi ndani ya Cuf ukiendelea kufukuta

Mgogoro wa Uongozi ndani ya Prof.Lipumba amemteua Naibu Katibu Mkuu Bara huku mgogoro wa Uongozi ndani ya Cuf ukiendelea kufukuta Chama cha wananchi Cuf umeendelea Kufukuta ambapo M/kiti wa Chama hicho Prof.Ibrahim Lipumba amemteua Naibu Katibu Mkuu Bara Magdalena Sakaya kukaimu nafasi ya Katibu Mkuu Maalim Seif shariff Hamad baada ya Maalim Seif kukaidi wito wa M/KIti wake kwenda ofisi Kuu Buguruni kwa zaidi ya mara nne.

Prof Lipumba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam pamoja na wafuasi wa chama hicho amesema Maalim Seif amekaidi wito wa kwenda Makao makuu Buguruni tangu Septemba 23 mwaka jana kwa ajili ya kusimamia mkutano wa kamati ya Utendaji ambao ulitakiwa kujadili mambo kadhaa ya chama hicho.

Aidha Prof. Lipumba amewavua madaraka wakurungezi kutoka zanzibar akiwemo Salim Bimani aliyekuwa Mkurugenzi wa habari na Uenezi, Omar Ali Salehe Mkurugenzi Mipango na Uchaguzi, Abdallah Bakar Khamis Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi, Pavu Juma Abdallah – Haki za Binadamu, Mahima Ali Mahima Katibu Mtendaji JUvicuf pamoja na Yusuph Salim Naibu Mkurugenzi Ulinzi na Usalama Cuf wote kutoka Znz.

Chama cha wananchi Cuf kimekumbwa na mgogoro wa uongozi tangu Prof.Lipumba alipotanga kujiuzuru uongozi wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu 2015,ambapo baadae alitangaza kurudi na kufanyika mkutano mkuu ambao ulivurugika na kusababisha mpasuko kati ya Cuf bara na cuf Zanzibar.

No comments:

Post a Comment