Monday, March 6, 2017

Klabu ya Chelsea Wakubaliwa Kujenga Uw.anja Mpya Wa Kisasa Ambao ni ghali zaidi

Meya wa jiji la London hatimaye amepitisha mpango wa kuendeleza uwanja wa Stamford Bridge unaotumiwa na klabu ya Chelsea ambao utagharimu kiasi cha paundi milioni 500 na kuufanya kuwa uwanja wa kisasa ambao utakuwa na uwezo wa kuingiza jumla ya washabiki 60000.

Chelsea walipewa ruksa ya kuanza mipango ya maendeleo ya uwanja huo na Hammersmith pamoja na halmashauri ya mipango ya Fulham na kamati ya maendeleo mwezi Januari na huku ikiwa ilitegemewa kupatikana sapoti ya meya wa London, Mayor Sadiq Khan kukubali kwake imekuwa ni hatua kubwa kwa timu ya kusimamia mpango huo wa maendeleo uliopo chini ya mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich.

Katika ujumbe wake, Khan alisema: “London ni moja ya majiji yanayojihusisha na michezo kwa kiasi kikubwa na nina furaha kuwa karibuni tutaongeza uwanja wa Chelsea kama moja ya viwanja vinavyovutia vya michezo.

“Baada ya kutizama kwa umakini mpango wenyewe, nimeridhika kuwa huu ni mtindo wa kipekee uliochaguliwa na unaovutia ambao pia utaongeza idadi ya watizamaji huku pia ukihakikisha kuwa washabiki wanaweza kupata njia rahisi za usafiri.

“Nina imani kuwa uwanja huu mpya utakuwa kama kito katika jiji la  London na utajivika taji la kuwa kiwanja bora cha michezo huku pia kikiwa kivutio kikubwa cha wageni na washabiki wa soka duniani kote.”

Kupitia tovuti yao, Chelsea walionyesha kufurahishwa na maamuzi ya Khan na kuongeza kuwa hii ni hatua kubwa kuelekea mpango wa kuendeleza uwanja huu na kupanua huduma za kijamii kwa ujumla.

“Kuna hatua nyingi zaidi mbele yetu, yote kabla na baada ya mipango iliyopo, kabla ya matengenezo hayajakamilika tunaweza kuanza kazi. Tunaendelea kushirikiana na wadau na tutatoa taarifa zaidi juu ya maendeleo kwa ujumla.

Pamoja na ongezeko la gharama za uharibifu utakaojitokeza Stamford Bridge na ujenzi wa uwanja mpya wenye uwezo wa kubea watu 60,000, Chelsea imetuma ombi linalohusu uwekezaji wa kiasi cha paundi milioni 12 kwenye shughuli tofauti za kijamii na kiasi cha paundi milioni 3.75 kwenye makazi yenye unafuu katika maeneo ya  Hammersmith na Fulham.

Mpango huo unamaanisha kuwa Chelsea itabidi wahamie kwenye uwanja wa nyumbani wa muda ikitegemewa kuwa uwanja wa Wembley kwa miaka 3 wakati Stamford Bridge ikiwa inaharibiwa ili uwanja mpya upate kujengwa, huku makadirio ya sasa yakiwa kukamilika kwake kuwa msimu wa 2021-22.

***************

No comments:

Post a Comment