Friday, February 24, 2017

Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga vijijini yapani kurudisha hadhi ya elimu iliyo Anza kushuka katika wilaya hiyo

Wadau wa elimu na viongozi halmashauri ya Mbinga vijijini wamekutana kufanya tathimini ya elimu ikiwemo kushuka kwa ufaulu kwa wa elimu ya msingi miaka ya hivi karibuni

Wakizungumza katika kikao hicho baadhi ya wadau wa elimu  wamezitaja changamoto zinazowasilishwa pelekea kushuka kwa elimu kuwa ni pamoja kutoboreshwa kwa masirahi ya walimu, upungufu wa walimu, ushiriki hafifu wa wazazi hususani kufuatilia maendeleo ya watoto wao na kuchangia shughuli za elimu

Pia wadau wameainisha changamoto zingine kuwa ni pamoja na kuto wahamisha walimu wakuu walio shushwa vyeo pamoja na kuongeza uwiano wa vitabu hasa vya kiada katika shule za halmashauri hiyo

Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga vijijini Gombo Samandito Gombo amesema halmashauri hiyo imejipanga kuhakikisha inaongeza ufaulu kimkoa na kitatifa hasa elimu ya msingi ambayo imeonekana kulegalega huku akiwataka walimu kuto fanya uzembe katika kufundisha ikiwemo utoro "sitakuwa na msamaha kwa walimu wanao acha kazi wanaenda kupiga boda boda ukiona nimekubaini nitakufukuza hata usiangaike kuniomba msamaha pia wapo walimu wanao kopa mpaka wanapiriliza muda wa kufundisha wanakimbia madeni waache mara moja" alisema Samandito

Awali katika maada za utangulizi mkuu wa Polisi wilaya ya Mbinga OCD Maganga amekemea baadhi ya wazazi kuwahusisha wanafunzi katika biashara ya dawa za kulevya na kuwataka viongozi ngazi ya vijijini na kata kutoa taarifa za wahusika wa biashara hiyo pamoja na wale wanao wapa mimba wanafunzi

Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya ya Mbinga Consimas Nshenyi  amendelea kukazia maagizo yaliyo tolewa wa na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Binilith Mahenge wakati wa ziara yake wilaya Mbinga  mapema mwaka huu juu ya uharibifu wa mazingira ikiwemo kufanya shughuli za kibinaadamu ndani ya mita sitini kutoka vyanzo vya maji pamoja na kuhakisha Benki tofauti zinatukamika katika kujenga majengo sio kukaa katika matanuru 

Matokeo ya darasa la saba mwaka 2016 yanaonyesha kushuka kwa elimu katika halmashauri hiyo ya  wilaya ya Mbinga baada ya kushika nafasi ya 8 katika mkoa wa Ruvuma kati ya Halamashauri 8 za mkoa huo

No comments:

Post a Comment