Monday, February 27, 2017

MARUFUKU KULIMA KARIBU NA VYANZO VYA MAJI

Na Riziki Manfred,
Bonzuma, Mbinga

katika kuendana na sera ya mazingira wilaya ya Mbinga imepiga marufuku shuguri zote za kibanadamu zinazo endelea katika vyanzo vya maji na pembezoni mwa mito ili kunusuru mabadiriko ya hali ya hewa katika ukanda huu wa kusini mwa Tanzania.

Marufuku hiyo limetolewa na mkuu wa wilaya Mbinga Consimas Nshenyi  ambapo amewaagiza mafias mazingira na  viongozi wa vijiji kuhakikisha wanasimamia sheria ya mazingira inayo kataza shughuri bza kibinada ndani ya mita 60 kutoka chanzo cha maji na pembezoni mwa mto ambapo shughuli za kibinadamu ambazo mara nyingi zimepelekea kuharibifu mkubwa wa mazingira katika.

Pia Nsenyi amesema kwanzia sasa hakuna namna nyingine ya kufanya juu ya wanao haribu mazingira zaidi ya kusimamia sheria za mazingira “hatuwezi kuwavumilia wanao haribu mazingira kwani tuatakuwa tunajiangamiza wenyewe sheria zipo na zipo wazi hivyo kila mtu anatakiwa kufuata sheria na kuna uharibifu mkubwa wa mazingira kwa watu wachache kuamua kulima, kuanzisha viwanda jambo ambalo tusipo angalia tutakosa hata vyanzo vya maji jambo ambalo ni hatari” alisema Nsenyi.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amepiga maruku kwa baadhi ya wafanya biashara kuwakopesha  fedha wakulima kwaajiri ya kununulia pembejeo na baadae mkulima  kulipa  mavuno anayo yapata  alimarufuka kama MAGOMA ambapo amesema kuwa ni kumfanya mkulima ashindwe kujikwamua katika kilimo kwani wamekuwa wakilipa mavuno tofauti na dhamani ya fedha aliyoichukua awali.”mtu anachukua shilingi elfu hamsini lakini analipa zaidi ya magunia matatu mpaka manne ukiangalia hikini kiwango kikubwa cha gunia moja laki moja magunia matutu ni shilingi laki tatu lakini mkulima alipewa elfu hamsini”alisema mkuu huyo wa wilaya

Aidha Nsenyi amewashauri wanachi kuacha kubweteka na MAGOMA badala yake wachape kazi na inapo bidi kupata pembejeo watumia taasisi za fedha kama benki ambazo mashart na vigezo vya benki vipo kisheria na ni vya wazi.

Baada ya tamko hilo la mkuu wa wilaya  uchunguzi ulio fanya na mtandao huu ibebaini kuwa bishara hii bado inaumaarufu kutokana na wanajamii wa kutoka wilaya hii wanapenda mfumo huu kwani kipindi cha mavuno wanachi hutumia fedha walizo pata kwaajiri ya mambo mengine tofauti na kilimo ikiwemo ngoma za kihoda na mganda ambazo ni maarufu katika wilaya hii hususani kipindi cha mavuno

No comments:

Post a Comment