Wednesday, March 1, 2017

Ajiua kwa kurazimiswa kunyonyesha mtoto

Na Furahisha Nundu
makete

Afariki Dunia kwa kukataa kunyonyesha na kumuacha mtoto wa kiume mwenye miezi mawili

Mwanamke mmoja Bi. Olida Sanga (19)amekutwa jana akiwa amekufa mto Luvanyina kijiji cha Isapulano kata ya Isapulano Wilayani Makete

Akizungumza na mwandishi wetu Mwenyekiti wa kijiji cha Isapulano mara baada za Mazishi ya Marehemu Olida,Bw. Mwatindi Mbilinyi amesema Marehemu wakati wa Uhai wake alikuwa analazimishwa kumnyonyesha mwanaye jambo ambalo huenda lilimkera na kuamua kuchukua maamuzi hayo

Inaelezwa kuwa Marehemu alikuwa anaugua ugonjwa wa kifafa kwa siku nyingi

Marehemu amemwacha mwanaye Mwenye Miezi miwili wa kiume ambaye kwa sasa analelewa na Ndugu zake wa Karibu

Wananchi walianzisha jitihada za kumtafuta mnamo jumapili saa 10 jioni na kwa bahati mbaya waliopoa maiti yake kwenye mto Luvanyina hapo jana saa 5:30 asubuhi

No comments:

Post a Comment