Friday, February 17, 2017

Video: Ndugu wa Masogange wakiondoka Kisutu baada ya kukosa matumaini ya ndugu yao




 Baada ya Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro kutangaza kumshikilia Agnes Masogange kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kudai huwenda Ijumaa hii angepandishwa mahakamani, ndugu wa mrembo huyo wameshinda mahakamani hapo wakimsubiria video queen huyo bila mafanikio yoyote.

 



Kamera  imeshuhudi ndugu hao wakienda huku na kule ili kujua hatma ya ndugu yao huyo bila mafanikio.

Mmoja kati ya ndugu hao ambaye hakutaka jina lake litajwe, alidai alienda sentro Polisi na kuambiwa ndugu yao huyo hatapandishwa Mahakamani leo kutokana na majibu ya mkemia mkuu kuchelewa.

Mapema jana Kamanda huyo aliwaambia wanahabari kuwa mrembo huyo anachunguzwa kwa mambo matatu. “Tunamchunguza Masogange katika mambo matatu ili kujua kama anauza , anatumia au anasafirisha dawa za kulevya.”

No comments:

Post a Comment