Friday, March 3, 2017

Mkoa wa Ruvuma wajipanga kuongeza ufaulu na kuongeza kitaifa

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mh Binilith Mahenge ameziagiza halmashauri na Kamati za shule mkoani humo kuhakikisha wanafunzi wanakula chakula cha mchana shuleni, pamoja na kuimarisha miundombinu katika shule zote zikiwemo nyumba za walimu.

Akifungua kikao cha tathimini ya elimu mkoa wa Ruvuma kilicho fanyika wilaya Mbinga mh Mahenge amesema moja kati ya changamoto zinazowasilishwa sababisha kushuka kwa kiwango cha elimu mkoani humo kutokana na wanafunzi wengi kutumia muda mwingi kufuata chakula majumbambani mwao  na wengine kukosa kabisa, pia Mahenge aliwataka walimu wote kukaa katika vituo vyao vya kazi ili kupata muda wa kujiandaa zaidi

Aidha Mh Mahenge ameagiza tathimini ya madawati kutokana na ongezeko la idadi ya wanafunzi walioandikishwa mpaka sasa na baada ya tathimini utengenezaji wa  madawati  uanze kufanyika pamoja na kuanza ujenzi wa majengo yenye upungufu hususani nyumba za walimu kwa kutumia nguvu za wananchi ikiwemo kutumia Benki tofauti na halmashauri kupeleka vifaa vya kiwandani “vijiji wekeni mipango ya ujenzi wa wa majengo yenye upungufu kwa kutumia Benki tofauti na halmashauri kupeleka vifaa vya kiwandani hakikisheni changamoto moto za nyumba za walimu, vyoo, madarasa inakwisha kabisa”alisema Mahenge

Wakitoa michango baadhi ya wadau wa elimu wamezitaja changamoto zinazochangia kudhoofisha kiwango cha elimu mkoani humo ikiwemo Uhaba uhaba wa walimu katika mkoa huo huku wakizitaka mamlaka husika kufanya msawazo wa walimu na kuwa na uwiano sawa kwa shule zote sambamba na kuboresha masirahi ya walimu kwa kuwalipa malimbikizo ya madeni walimu wanayo idai serikali na pamoja na kuwapandisha madaraja walimu , "walimu wanaishi kwenye nyumba za nyasa watawezaje kufundisha watoto darasani" alisema Alfred Nguguru akiendelea bwana Nguguru ameomba serikali iliangalie suala la mimba shuleni kwa kuwatafutia mabweni wanafunzi "tunaomba pia wanafunzi wawe na mabweni(hosteli) hasa watoto wa kike hata kwa kupanga ili kupunguza mimba shuleni"

Kikao hicho cha tathimini ya elimu mkoa wa Ruvuma chenye lengo la kuhakisha inaongeza ufaulu katika mitiani ya mwisho sambamba na kutatua changamoto zinazo ikabili sekta ya elimu pamoja kutoa zawadi na vyeti kwa shule zilizo fanya vizuri na kutoa vivyago kwa shule zilizo fanya vibaya baada ya matokeo kuonesha kushika nafasi ya 8 kitaifa tofauti na mwaka jana ambapo mkoa huo ulishika nafasi ya 7 


Manispaa ya Songea mshindi wa kwanza katika matokeo ya kidato cha nne matokeo ya mwaka 2016 

Picha zote chini ni mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mh Binilith Mahenge akiwasili wilayani Mbinga kwenye kikao cha tathimini ya elimu mkoani humo
 By  (Picha na Riziki Manfred Bonzuma) 

No comments:

Post a Comment