Monday, February 27, 2017

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye atuma salamu za pole shirikisho la 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye ametoa salamu za pole kwa Rais wa Shirikisho la  Riadha  nchini, Anthony Mtaka kufuatia kifo cha mshiriki kutoka nchini Kenya, Charles Rioba (36) aliyefariki  katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika Februari, 26 mkoani Kilimanjaro.

Rioba alishiriki kwa hiari mbio zijulikanazo kama ‘run for fun’ za Kilometa 21, zilizohusisha wananchi mbalimbali wakiwemo pia viongozi wastaafu.

Lakini akiwa katika mbio hizo alianguka na kupatiwa huduma ya kwanza kisha  kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) na baadae kufariki dunia.

Waziri Nape ametoa pole pia kwa waandaaji wa mashindano hayo na wote ambao wameguswa na msiba huo

No comments:

Post a Comment