Tuesday, February 28, 2017

Soma Ujumbe huu, Usipuuzie usije ukaingia mkenge


KUTOKA JESHI LA POLICE:

USALAMA WA MAISHA YAKO
Usinunue simu za Android kwa mtu usiyemjua. Hiyo ni hatari kwani hujui huyo jamaa kaitoa wapi, mwisho wa siku unapewa kesi ya wizi au mauaji. Inawezekana simu hiyo iliibiwa kwa mtu aliyeuawa.

  Usimpe mtu usiyemjua simu yako apige sehemu yoyote.
  Unapoiona line njiani ipo chini, usitake kuiokota na kuiweka simuni mwako ujue ina shilingi ngapi ili uchukue salio.

Simu inapoibiwa au
mwenye simu kuuawa, line hutupwa, unapoiweka simuni mwako,simuyako inahusishwa na tukio hilo
Unapoweka salio, hakikisha karatasi ya vocha unaichana. Unapoitupa, watu wanaweza kufanya mauaji, wakachukua karatasi ya vocha ile na kuweka sehemu ya tukio au pale ulipoitupa kukatokea tukio na wewe kuhusishwa.

 Usikubali kumsajilia mtu line yake kwa jina lako, hata kama baba yako, usikubali.
Kumbuka namba yako umesajiliwa, moja ya matukio hayo yakitokea na namba yako kuonekana, moja kwa moja unakuwa mtuhu-miwa namba moja.

Wengi wamepewa kesi za mauaji, wizi bila kujua. Polisi wapo kazini, wanapoona vidhibiti wanakuchukua kwani hawatojua kama umehusika au la. Kuweni makini ili usije kuingia matatizoni, simu yako, fedha zako, ukifanya kisicho sahihi kama uzembe, utaishia pabaya.
SIMU YAKO JEMBE LAKO
SHARE UJUMBE HUU UMPE ONYO NA MWENZAKO.

No comments:

Post a Comment