Tuesday, May 29, 2012

Zanzibar bado si shwari

MIRADI YA MAENDELEO YA MABILONI YA FEDHA YAZINDULIWA NA MWENGE WA UHURU MAKETE

Mwenge wa uhuru ukiwa eneo la mkesha Mabehewani wilayani hapa
 
Miradi tisa yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni mbili imezinduliwa na mwenge wa uhuru ambao unaendelea na mbio zake katika wilaya ya Makete

Hayo yamebainika baada ya miradi hiyo kuzinduliwa rasmi na mwenge huo wa uhuru ambapo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete Bi Imelda Ishuza amewaeleza maelfu ya wakazi wa Makete waliofurika katika viwanja vya Mabehewani wilayani Hapo kuupokea mwenge huo ambao pia utakesha hapo

Akitoa taarifa hizo Bi Ishuza ameitaja miradi hiyo iliyozinduliwa na Mwenge huo wa uhuru kuwa ni pamoja na Ofisi ya kijiji kipya cha Ikovo, kituo cha CTC kilichopo ndani ya Kituo cha afya Matamba, Nyumba bora ya Nuhu Ngogo iliyopo Matamba na Hoteli ya Kitulo iliyopo Matamba


Mingine ni Vyumba vya madarasa na nyumba ya mwalimu mkuu shule ya msingi Manga, Mradi wa maji katika kijiji cha Nkenja, shamba la miti katika kijiji cha Ivalalila pamoja na nyumba tatu za watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Makete

Akizungumza na wakazi wa Makete kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Kapteni Honest Ernest Mwanosa amewataka wananchi kuhakikisha wanaitunza miradi hiyo hasa mradi wa maji, ambao kwa kiasi kikubwa utawahudumia wananchi wenyewe

"Unajua wananchi utunzaji wa vyanzo vya maji ni kitu muhimu sana, wilaya ya Makete ni miongoni mwa wilaya chahe zilizojaliwa kuwa na vyanzo vingi vya maji, tujiepushe kulima kwenye vyanzo vya maji pamoja na kuendesha shughuli za kibinadamu katika vyanzo hivyo na badala yake tuvitunze" alisema Mwanosa

Pia amewataka wananchi wa Makete kujitokeza kushiriki katika mchakato wa katiba mpya kwa kutoa maoni yao pamoja na kushirikkikamilifu katika sensa ya watu na makazi itakayofanyika nchi nzima Usiku wa kuamkia Agosti 26 mwaka huu

Mwenge wa uhuru upo wilayani Makete na kesho utakabidhiwa katika wilaya ya Njombe, na kaulimbiu ya mwaka huu ni sensa ni msingi wa maendeleo yetu mwananchi shiriki kikamilifu Agosti 26 2012, mabadiliko ya katiba toa maoni

SIMBA SC WALIVYOSHEREHEA UBINGWA WAO DAR LIVE

Wachezaji na viongozi wa timu ya Simba wakiwa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla (katikati aliyeshika kombe).
TIMU ya Simba SC ya jijini Dar jana ilisherehekea ubingwa wake wa 2011/2012 pamoja na mashabiki wake katika ukumbi wa burudani wa DAR LIVE.

Sherehe hizo zilitanguliwa na msafara wa magari, pikipiki na watembea kwa miguu ambao walianzia safari yao makao makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Msimbazi na kupitia mitaa kadhaa ya jiji kabla ya kumalizikia katika ukumbi wa Dar Live.

Katika msafara huo wachezaji wa Simba walikuwa katika lori la wazi lililopambwa bendera na vitambaa vya rangi nyekundu na nyeupe huku wakiwa na kombe lao walilolibeba.

Mashabiki na wapenzi wa Simba SC wakiwa katika msafara kuelekea katika Ukumbi wa Dar Live kusherehekea ubingwa wa timu yao jana.
Wachezaji na viongozi wa Simba wakifungua shampeini wakati wakisherehekea ubingwa wao ndani ya ukumbi wa Dar Live jana
Meneja wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (kulia) akimkabidhi nahodha wa Simba SC, Juma Kaseja shilingi milioni 3 zilizotolewa na Dar Live kama pongezi kwa timu hiyo kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom 2011/2012
Naibu Waziri Amos Makala akimvisha medali Uhuru Selemani
Wachezaji wa Simba wakipata menyu pembeni ya kombe lao
Baadhi ya mashabiki waliohudhuria sherehe hizo.

BAADA ya Kanisa la Assemblies of God kuchomwa moto katika vurugu zilizoanza mwishoni mwa wiki

BAADA ya Kanisa la Assemblies of God kuchomwa moto katika vurugu zilizoanza mwishoni mwa wiki iliyopita, jana Kanisa Katoliki Parokia ya Mpendae nalo limechomwa moto.

Akizungumzia hali hiyo jana, kiongozi wa Kanisa hilo, Ambaros Mkenda, alidai kwamba Kanisa hilo lilichomwa moto na watu wasiojulikana na kusababisha uharibifu mkubwa.


Alidai Kanisa hilo lilichomwa moto jana saa 8.30 mchana na watu wanaohisiwa kuwa wafuasi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Uamsho, waliokuwa wakitoka katika Mahakama ya Mwanakwerekwe kusikiliza kesi ya wenzao waliokamatwa juzi.


Mkenda alidai kuwa watu hao waliwazidi nguvu walinzi wawili wa Kanisa hilo na kuvunja lango kuu la kuingilia ndani ya Kanisa na kuchoma moto na waliharibu madirisha na vifaa kadhaa vyenye thamani ya Sh milioni 20.


“Tunasikitika sana na uharibifu mkubwa uliofanywa katika Kanisa letu ambalo lilikuwa tegemeo kubwa kwa wafuasi wapatao 2,000 wa eneo la Parokia ya Mpendae na jirani,” alisema Mkenda.


Mkenda alidai kuanzia juzi, viongozi wa makanisa mbalimbali waliwasilisha maombi yao Polisi kuhusu kupewa ulinzi katika nyumba za ibada, baada ya kupokea vitisho. Hata hivyo, Mkenda alidai ombi lao hilo halikutekelezwa na Polisi na uharibifu mkubwa ukatokea katika Kanisa la Assemblies of God la Kariakoo.


Wafuasi na waumini wa Kanisa hilo walikusanyika nje ya jengo hilo, huku vijana wakishikwa na hasira wakitaka kwenda kulipiza kisasi katika maeneo ya jirani wakidai wanawatambua vijana waliofanya vitendo hivyo.


Mmoja wa waumini wa Kanisa hilo ambaye ni mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC), Susan Kunambi alilazimika kuwatuliza wafuasi vijana wa Kanisa hilo waliopandwa na jazba wakitaka kulipa kisasi.


“Hakuna sababu ya kupandisha jazba na kutaka kufanya vitendo ambavyo vitasababisha hasara na uharibifu ... Kanisa siku zote linahimiza amani na upendo na si chuki,” alisema Kunambi.


Polisi walifika haraka katika eneo la tukio na kurusha mabomu ya machozi ili kutawanya makundi ya vijana waliojikusanya na wengine kurusha mawe.


Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alithibitisha kuchomwa moto Kanisa hilo na kusema ulinzi umeimarishwa katika baadhi ya maeneo ya nyumba za ibada yakiwamo makanisa. Baadhi ya mitaa ya Jang’ombe na Mwanakwerekwe njia zimewekwa mawe na vikundi vya vijana waliochoma mipira ya gari na kusababisha moshi mkubwa.


Vikundi marufuku Wakati huo huo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imepiga marufuku maandamano, mihadhara ya kidini na mikusanyiko isiyo na kibali.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud alisema hayo wakati akitoa taarifa rasmi ya SMZ baada ya vurugu zilizofanywa na wafuasi wa Uamsho baada ya kukamatwa kwa viongozi wao wa kidini.


Aboud alisema Serikali haitakubali kuona kikundi cha watu wanafanya vitendo vya uvunjifu wa amani na kuvuruga utulivu wa nchi kwa kisingizio cha kudai mabadiliko ya Katiba na imani ya dini.


“Wapo watu wanataka kuona tunarudi nyuma katika kipindi cha fujo na vurugu za kisiasa...wakati huo umepita,” alisema Aboud. Kutokana na hatua hiyo ya Serikali, mihadhara na maandamano kuanzia sasa italazimika kupata kibali kutoka taasisi husika ikiwamo Polisi. Alitaka wazazi wakataze watoto wao kujishughulisha na ushawishi wa kufanya vitendo vitakavyohatarisha amani na utulivu wa nchi.


Utulivu wajirudia mjini Jana hali ya utulivu ilirejea kisiwani hapa ikiwamo Mji Mkongwe na sehemu za mitaa ya Ng’ambo, huku wananchi wakifanya shughuli zao za maendeleo na biashara bila matatizo.


Maduka na huduma za usafiri viliendelea kama kawaida huku wafanyakazi wa Manispaa wakifanya usafi ikiwa ni pamoja na kuondoa matairi ya magari yaliyochomwa barabarani katika vurugu za juzi.




“Tunasafisha barabara zilizoharibiwa na waandamanaji kwa kuchoma moto mipira ya magari,” alisema Ali Juma mfanyakazi wa Manispaa ya Mji wa Unguja. Kamishna Mussa alisema Polisi waliendelea kuweka doria katika maeneo mbalimbali ya mji kwa kushirikiana na vikosi vya SMZ.


“Tutaendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ikiwamo nyumba za ibada ili kuhakikisha hakuna vitendo vya uvunjifu wa amani,” alisema Mussa.


Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi alionya kuwa suala la amani na ulinzi wa raia na mali zao halina mjadala na kuvihadharisha vikundi vinavyohatarisha amani, kwamba vitapambana na mkono wa Dola.


Dk Nchimbi aliyekuja hapa ili kukutana na viongozi wa vikundi vya dini na mihadhara na Polisi, alisema athari ya kuvunja amani na utulivu ni kubwa na wananchi wa Zanzibar wanafahamu vizuri mazingira yalivyokuwa miaka ya nyuma.


Alitaka viongozi wa dini wajifunze sheria za nchi na kuzifuata na kuwataka wasihusishe Uislamu na vurugu na fujo kiasi cha kuhatarisha amani ya nchi.


Pia alitaka wananchi walioharibiwa mali zao kwenye vurugu na fujo kutoa taarifa Polisi kwa hatua zaidi.


Awali Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Said Mwema, alisema Polisi itaendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yote ya nchi.


Watu 30 wakiwamo wafuasi wa Uamsho walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe kujibu mashitaka yakiwamo ya kuandamana kinyume cha sheria na ukorofi wa kuwashambulia polisi kwa mawe.


Watuhumiwa hao walisomewa mashitaka katika makundi matatu tofauti; kundi la kwanza likiwa la viongozi wawili wa jumuiya hiyo; Mussa Juma Issa (57) na Mbarouk Said Khalfan (45). Walisomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mohamed Ali Sheni ya kujikusanya kinyume cha sheria na kufanya maandamano ambayo yalianzia Uwanja wa Lumumba kupitia Msikiti wa Kwabiziredi na kumalizia uwanjani hapo.


Watuhumiwa hao walikana mashitaka na kupewa dhamana ya masharti ya Sh 300,000 kila mmoja kwa kiasi hicho hicho; walitimiza masharti na wako nje kwa dhamana hadi Juni 11 kesi yao itakapotajwa. Kundi la pili la watuhumiwa wengine sita walisomewa mashitaka mbele ya Hakimu Janet Sekihola ambayo ni ya uzembe, ukorofi na kushambulia polisi waliokuwa doria.


Watuhumiwa hao ni Abdulrahman Simai Khatib, Hashim Juma Issa, Martar Said Ramadhan, Mbwana Hamad Juma, Masoud Hamad Mohamed na Mohamed Juma Salum.


Kesi ya watuhumiwa hao iliahirishwa hadi Juni 11 itapotajwa huku baadhi yao wakitafuta wadhamini na kutakiwa kuwa na wadhamini wawili kila mmoja kwa Sh 500,000.


Maimamu wawakana Jumuiya ya Maimamu na Mihadhara ya Jumaza, imesema waliofanya fujo na vurugu zilizosababisha uharibifu mkubwa wa mali za wananchi si wafuasi wao.


Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Muhidin Zubeir Muhidin ambayo pamoja na jumuiya hiyo ndizo taasisi zinazojishughulisha na mihadhara ya dini ya Kiislamu ambayo hutoa elimu kuhusu marekebisho ya Katiba.


Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Shehe Zubeir alisema jumuiya hiyo haijatuma watu kufanya fujo, kwa sababu katika dini hiyo ni makosa mtu kuharibu mali ya mwenzake. “Tunataka Waislamu wote na wafuasi wa Jumaza na Uamsho kuacha fujo na kurudi nyumbani kusubiri hatma ya viongozi wao,” alisema Shehe Zubeir.


Serikali ya Marekani imesema matukio yaliyotokea kwa siku mbili Zanzibar yanaweza kuchafua taswira nzuri iliyowekwa na visiwa hivyo, katika uchaguzi mkuu uliosababisha kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa mwaka 2010.


Hayo yamesemwa na Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kutokana na ghasia zilizotokea visiwani humo na kusababisha Kanisa na gari la kiongozi wa Kanisa kuchomwa moto.


“Kudumisha mazingira ya amani visiwani Zanzibar ambayo yanaruhusu utalii na maendeleo kuna maslahi kwa Wazanzibari wote na hata wageni waingiao visiwani humo,” alisema Balozi Lenhardt katika taarifa yake iliyotolewa jana Dar es Salaam.


Alisema ni muhimu kwa kila mtu kujizuia na kulinda maisha na mali za watu wasio na hatia na aliunga mkono waliozitaka pande zinazozozana kushirikiana kuleta amani na utulivu katika visiwa hivyo.


“Tunatambua umuhimu wa mjadala wa kisiasa unaoendelea lakini tunavitaka vyama vyote kuendelea kuufanya kwa njia ya amani na kidemokrasia zaidi,” alisema Balozi huyo.


Aliongeza kuwa anakubaliana na anaunga mkono hatua za haraka zilizochukuliwa na viongozi waandamizi wa kisiasa waliojitokeza kushughulikia masuala yaliyosababisha matukio hayo ya kusikitisha.

Tuesday, May 8, 2012

NI BAADA YA MAJADILIANO YA SERIKALI NA TUCTA

 Send to a friend
Rais Jakaya Kikwete

Waandishi Wetu
KUNA taarifa kwamba Serikali imekubali kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma kwa kati ya asilimia 20 na 33.3 katika Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2012/13.Hatua hiyo inamaanisha kwamba kima cha chini cha mshahara sasa kitakuwa kati ya Sh180,000 hadi Sh200,000 kutoka Sh150,000 zinazolipwa sasa.Vyanzo vya habari kutoka serikalini vimeeleza kwamba nyongeza hiyo ya kati ya Sh30,000 hadi Sh50,000 ni matokeo ya mazungumzo kati ya Serikali na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta).Mbali ya kutaja kima hicho, vyanzo hivyo vimeeleza kuwa nyongeza hiyo inaweza kuvuka Sh50,000 kutegemea uwezo wa Serikali.

Hata hivyo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), George Yambesi alipoulizwa kuhusiana na taarifa hiyo alijibu kwa kifupi kuwa hakuwa katika nafasi ya kuzungumzia hilo.

“Sipo katika ‘position’ (nafasi) nzuri ya  kuzungumzia hilo, nadhani suala la mishahara. Mheshimiwa Rais alishalizungumzia kwenye hotuba yake ya Sikukuu ya Wafanyakazi,” alisema.

Katika hotuba yake kwenye kilele cha sherehe hizo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Rais Jakaya Kikwete alisema Serikali inatambua mazingira magumu ya kazi waliyonayo wafanyakazi na kwamba ipo tayari kuyaboresha.

Alisema imesikia madai ya wafanyakazi na itaendelea kuyafanyia kazi. Madai aliyoahidi kuyafanyia kazi ni pamoja na kupunguziwa kodi ya mapato.

Kwa upande wa Tucta, Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Nicolaus Mgaya alipoulizwa jana alisema hajui Serikali itaongeza mshahara kwa kiasi gani lakini akasema anaamini kuwa ni sikivu.

Alisema kwa miaka mingi wafanyakazi wamekuwa wakilalamikia mishahara midogo ambayo haikidhi mahitaji, jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa migongano ya hapa na pale na Serikali akasema kutokana na hali hiyo, wanaamini kuwa wataongezewa.

“Tunaamini linaweza kutekelezeka (suala la kuongezewa mishahara), lakini hakuna anayejua nyongeza hiyo itakuwa ni kiasi gani, kwa hiyo ukinitajia kiwango nashindwa kuelewa umekitoa wapi,” alisema Mgaya alipoulizwa kama nyongeza hiyo ni kati ya Sh30,000 na 50,000.

Mgaya alisema mbali na kuomba nyongeza mshahara, Tucta pia imeiomba Serikali kupunguza gharama za tozo za mifuko ya hifadhi ya jamii huku ikienda pamoja na udhibiti wa mfumuko wa bei ambao umekuwa kikwazo kwa wafanyakazi na kuwafanya kuishi katika mazingira magumu kiasi cha kushindwa kujituma ipasavyo na wengine kukimbilia kwenye sekta binafsi.

“Wafanyakazi ni tabaka kubwa, lakini limesahaulika. Hii inatokana na Serikali kushindwa kusikiliza kilio chao cha kuwaongezea mishahara jambo ambalo limechangia kulipwa ujira mdogo na kusababisha wengi wao kukimbilia kwenye sekta binafsi, kutokana na hali hiyo tunaamini kuwa Serikali itasikilia kilio chetu,” alisema.

Madai ya wafanyakazi

Sakata la mshahara wa wafanyakazi liliibua mgogoro mkubwa baina ya Serikali na Tucta na mwaka 2010, Shirikisho hilo liligoma kumwalika Rais Kikwete kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Mei Mosi kitaifa kama ilivyokuwa utamaduni wake.

Hatua hiyo ya Tucta ilitokana na kile lilichodai kuwa Serikali siyo sikivu na lilitumia siku hiyo kujadili na kutoa tamko la kuitaka kutangaza kima kipya cha mshahara cha Sh315,000 ndani ya siku mbili la sivyo wafanyakazi wa umma wangeingia katika mgomo nchi nzima.

Hatua hiyo ilimlazimu Rais Kikwete kuitisha mkutano na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam Mei 3, 2010 na kujibu hoja mbalimbali za Tucta na kuweka msimamo wa Serikali kuwa haiwezi kulipa kiasi hicho cha fedha.

Rais Kikwete aliwatuhumu viongozi wa Tucta kuwa ni waongo na kwamba walikuwa hawasemi ukweli juu ya kile walichokuwa wanabaliana katika vikao vyake na Serikali.

Alisema Serikali ikifanya kima cha chini kuwa Sh300,000 kwa watumishi wa umma, itabidi iwalipe Sh6.9 trilioni kwa mwaka wakati makadirio ya makusanyo ya mapato ya Serikali kwa mwaka 2010/11 ni Sh5.8 trilioni.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

- Mtoto wa Ajabu Mwenye Sehemu za Siri Usoni



NewsImages/6393250.jpg
Mtoto wa Ajabu aliyezaliwa mkoani Ruvuma

Mtoto wa ajabu amezaliwa mkoani Ruvuma akiwa na nne za siri ambapo sehemu za siri mbili za kike na kiume zipo kwenye paji la uso na sehemu zingine mbili za siri za kike na za kiume kwenye maeneo ya sehemu za siri.
Mtoto huyo alizaliwa kwenye hospitali ya mkoa wa Ruvuma akiwa na jumla ya sehemu nne za siri ambapo mbili kati ya hizo zipo usoni na zingine mbili zipo kwenye maeneo ya sehemu za siri.

Mtoto huyo ni mtoto wa nne kuzaliwa katika familia ya bwana Said Abdallah ambayo tayari ina watoto watatu ambao hawana kasoro yeyote.

Mganga Msaidizi mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Ruvuma, Bwana Mathew Chanangula alisema kuwa sababu ya kuzaliwa kwa mtoto huyo akiwa na maumbile ya ajabu huenda ikawa imesababishwa na mama wa mtoto huyo kutumia madawa makali wakati wa ujauzito.

Angalia VIDEO chini kwa video ya mtoto huyo na maelezo zaidi kuhusiana na kuzaliwa kwake.

CM: Mawaziri wenye tuhuma washtakiwe


 
5
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye
Waandishi Wetu
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakitakuwa na huruma kwa mawaziri ambao wamewajibishwa kutokana na wizara zao kutajwa kwenye Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwamba zimehusika na ufisadi, badala yake kitakuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanafikishwa mahakamani.

Kauli hiyo imekuja kipindi ambacho tayari Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), inafanya uchunguzi dhidi ya mawaziri sita ambao wametajwa kwenye ripoti hiyo ya CAG na ambao Rais Jakaya Kikwete aliwang’oa katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.

“Kama uchunguzi wa Takukuru utathibitisha tuhuma hizo, watapanda kizimbani kwa kuwa hakuna aliye juu ya sheria,” Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema jana.

Akitolea mfano wa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa kupanda kizimbani juzi kutoa ushahidi kwenye kesi inayomhusu aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, Nape alisema: “Hii inathibitisha kuwa hakuna aliye juu ya sheria za nchi.”

Nape alikuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa chama hicho, mjini Dodoma ambako pamoja na mambo mengine, alitangaza ratiba ya Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec).

“Katika hilo nasema kuwa hakuna aliye juu ya sheria, jana (juzi) Mzee Mkapa alipanda mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi, iweje hao wengine waachwe? Nasema kama walihusika na ikathibitika kweli hata kama wengine wamebaki katika baraza, ni lazima watawajibika,’’ alisema.

Mawaziri walioachwa katika baraza hilo jipya ni Mustafa Mkulo (Fedha), Mhandisi Omary Nundu (Uchukuzi), Dk Hadji Mponda (Afya na Ustawi wa Jamii), Dk Cyril Chami (Viwanda na Biashara), Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii) na William Ngeleja (Nishati na Madini).

Wengine waliokuwa wakitajwa kuguswa katika ripoti ya CAG ni George Mkuchika aliyekuwa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi na Profesa Jumanne Maghembe aliyuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika. Mawaziri hao sasa wamehamishwa katika wizara hizo. Mkuchika sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora) na Profesa Maghembe ni Waziri wa Maji.

Nape alikiri kupata taarifa za mawaziri hao wa zamani kuchunguzwa na Takukuru, lakini akasema katika mtego huo si wote ambao wanaweza kunaswa.
Kuhusu wabunge wa CCM waliotia saini barua kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ikiwa ni shinikizo la kutaka mawaziri hao wajiuzulu au wawajibishwe, Nape alisema chama chake hakifikirii na hakitathubutu kuwajadili.

Akizungumzia ratiba ya kikao hicho, alisema Kamati ya Maadili ya CCm itakutana Jumamosi ijayo chini ya Uenyekiti wa Rais Kikwete na baadaye siku hiyohiyo, Kamati Kuu itakutana.

Alisema Mei 13, itakuwa ni siku ya semina kwa wajumbe wa Nec ambayo pamoja na mambo mengine, watapata nafasi ya kuipitia Katiba mpya ya CCM pamoja na marekebisho.

Jumatatu ya Mei 14, kutakuwa na kikao cha Nec ambacho  kitajadili mustakabali wa siasa nchini pamoja na mabadiliko ya Katiba ya nchi.

Mawaziri waanza kazi
Mawaziri wapya jana walianza kazi baada ya kukabidhiwa na watangulizi wao ambao ama waliondolewa kwenye nafasi zao, au walihamishiwa wizara nyingine.

Mawaziri wapya waliokabidhiwa ofisi jana ni William Mgimwa (Fedha), Profesa Sospeter Muhongo (Nishati na Madini), Dk Abdallah Kigoda (Viwanda na Biashara), Dk Fenella Mukangara (Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo) na Christopher Chiza (Kilimo, Chakula na Ushirika).

Katika makabidhiano hayo, Dk Mukangara aliwataka watendaji wa wizara hiyo kuhakikisha kuwa wanasimamia uwajibikaji na nidhamu ili kutimiza mpango wa miaka mitano.

Akizungumza na wafanyakazi wa wizara hiyo, Dk Mukangara alisema kila mfanyakazi ana wajibu wa kuhakikisha kuwa anatimiza majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kujua anachokifanya akiwa kazini.

“Suala la uwajibikaji ni muhimu kwa sababu kila mmoja anajua wajibu wake, hivyo basi hapaswi kusukumwa,” alisema Dk Mukangara.

Waziri wa Fedha, Willim Mgimwa pamoja na manaibu wake, Janeth Mbene na Saada Mkuya Salumu waliahidi kusimama imara kuhakikisha kodi za Serikali zinakusanywa kikamilifu.
Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda hakutaka kuzungumza lolote kwani alisema alikuwa na majukumu mengi ya kufanya katika ofisi yake hiyo mpya.

Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria waliwapokea mawaziri wao kwa mbwembwe. Waziri wake, Mathias Chikawe alirejea tena wizarani hapo akitokea Ofisi ya Rais (Utawala Bora) na jana aliingia akiwa na naibu wake, Angela Kairuki.

Wizara ya Maliasili na Utalii, imeandaa sherehe ya kumuaga aliyekuwa Waziri wake, Ezekiel Maige na kumkaribisha Balozi Khamis Kagasheki.

Msemaji wa wizara hiyo, George Matiko alisema  wataandaa sherehe hiyo kuonyesha upendo waliokuwa nao kwa waziri aliyepita.

Matiko alisema wasingependa kumuaga Maige kimyakimya hivyo kwa kuandaa sherehe ambayo itaonyesha ni jinsi gani walikuwa karibu naye.

Jana, Maige alifika wizarani hapo na kukabidhi ofisi kwa Balozi Kagasheki.
Imeandikwa na Habiel Chidawali, Dodoma, Boniface Meena, Patricia Kimelemeta,  Pamela Chilongola, Aisha Ngoma na Zaina Malongo, Dar.

Mwalimu mkuu ajitia kitanzi afisini mwake


Mikonge
Shamba la mikonge katika kijiji cha Singila, eneo la Mwatate. Mwalimu mkuu wilayani Mwatate alijiua siku ya kwanza ya muhula wa pili Jumatatu. Picha/MAKTABA 
Na KENYA NEWS AGENCY  ( email Mwandishi)
Imepakiwa - Tuesday, May 8  2012  at 10:54
Kwa Mukhtasari
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Mwandala, Taita Taveta alijifungia ndani ya afisi yake na kujinyonga siku ya kwanza ya muhula. Baada ya matokeo ya KCPE, alikuwa amezomewa na kufurushwa nje ya shule na wazazi waliokuwa na hasira kutokana na matokeo mabaya. Haijabainika nini hasa kilimfanya ajitoe uhai.

MWALIMU Mkuu wa shule ya msingi ya Mwandala, wilayani Mwatate, Kaunti ya Taita Taveta, alijiua baada ya kujifungia ndani ya afisi yake, siku ya kwanza baada ya shule kufunguliwa kwa muhula wa pili.
Mwili wa Bw Peter Mwabili ulipatikana ukining’inia kwenye paa na walimu waliokuwa waliovunja mlango waweze kuingia ndani ya afisi yake.
Polisi wakiandamana na viongozi wa eneo hilo, waliwasili baadaye na kuuchukua mwili huku wakiwaacha wakazi, walimu na wanafunzi wakiwa wameshangazwa na kushtushwa mno na tukio hilo.
Marehemu aliacha barua iliyoelezea jinsi ambavyo mali yake ilistahili kugawanywa kati ya wanawe na mkewe. Alisema mkewe anafaa kurithi robo ya mali huku watoto wake wanne wakipata thumni (sehemu moja kati ya nane), huku kitinda mimba akipata sehemu moja kati ya 16 ya mali yake.
Barua hiyo pia iliwataja watu aliokuwa akiwadai na kiasi cha pesa anazowadai na kuwataka walipe madeni kwa familia yake.
Mapema asubuhi
Mkuu wa tarafa ya Mwatate,  Bw Aswani Were, alisema Bw Mwabili alifika shuleni mapema asubuhi Jumatatu na kujifungia ndani ya afisi yake kabla ya kujitoa uhai.
“Alifika kazini kama kawaida na kujifungia afisini mwake. Walimu wengine waliompata walilazimika kuvunja mlango kwani alikuwa amejifungia kutoka ndani,” akasema.
Marehemu alikuwa na wakati mgumu katika shule ya Mwandala huku wazazi wakati mmoja wakimfurusha na kumfungia nje ya shule mwishoni mwa mwaka jana wakiitisha kuhamishwa kwake kutokana na matokeo duni ya Mtihani wa Kitaifa wa Darasa la Nane (KCPE).
Alikuwa amehudumu kwa muda mrefu kama mwalimu mkuu katika shule za eneo hilo, ikiwa ni pamoja na shule za msingi za Kamutonga na Mwachabo kabla ya kuhamishiwa Mwandala kutoka shule ya msingi ya Mwandisha ambapo alikuwa akihudumu kama naibu mwalimu mkuu.
Mkuu wa polisi wa kituo cha Taita Charles Kibet alisema mwili ulipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti cha Wesu kusubiri kufanyiwa upasuaji.
“Uchunguzi umeanzishwa kuhusu kisa hicho,” akasema. “Tunajaribu kuchunguza tubaini ni nini huenda kilimfanya ajitoe uhai,” akasema Bw Kibet.

rekodi mpya simba







Emmanuel Okwi
Ibrahim Bakari na Mashirika
WAKATI wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, Simba wakiondoka leo kwenda Khartoum, Sudan tayari kwa mchezo wa marudiono dhidi ya Al Ahly Shendi,  washambuliaji nyota wa Wekundu hao wa Msimbazi, Emmanuel Okwi na Felix Sunzu wameingia kwenye rekodi ya wafungaji bora Afrika katika michuano ya Kombe la Shirikisho la soka Afrika.
Okwi, raia wa Uganda na Felix Sunzu ambaye ni Mzambia, wote wametajwa kuwa na mabao matatu kila mmoja kwa mujibu wa mtandao wa tensport.com.
Mshambuliaji huyo anayechezea pia Uganda Cranes, alifunga bao moja dhidi ya Entente Sportive de Setif katika mchezo wa kwanza kati ya mawili walioshinda mabao 2-0 Dar es Salaam na moja likifungwa na Haruna Moshi.
Mchezo wa marudiano, Okwi alifunga moja wakati Simba ikilala mabao 3-1. Mshambuliaji huyo alifunga dhidi ya Al Ahly Shendi kati ya mabao matatu huku mengine yakifungwa na Boban na Patrick Mafisango.
Kwa hali hiyo, Boban na Sunzu kila mmoja wana mabao matatu. Sunzu aliyafunga katika mchezo walioshinda mabao 2-1 dhidi ya Kiyovu ya Rwanda na lingine likifungwa na Parick Mafisango.
Mbali na wachezaji hao, wengine wenye mabao matatu ni Komara, Niamba wote wa Leopards ya Congo, Chinyengetere (Hwange ya Zimbabwe, Moco (InterClube (Angola) na Raouf (ENPPI, Misri) na Seri wa Asec Mimosa ya Ivory Coast.
Mpaka sasa Fiston (Lydia Academic, Burundi) na Girma wa St George ya Ethiopia wana mabao manne kila mmoja.
Wakati huo huo, msafara wa Simba unaondoka leo mchana kwenda Sudan kupitia Nairobi, Kenya tayari kwa mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahly Shandy baada ya kukwama kuondoka kutokana na majambazi kuvunja na kuiba katika ubalozi wa Sudan.
Juzi usiku majambazi walivunja sefu ya kuhifadhia fedha na kuiba zaidi ya dola 40,000 ubalozini hapo pamoja fedha nyingine pamoja na kuiba kompyuta zote zinazotumika kuhifadhia kumbukumbu mbalimbali.
Kutokana na hali hiyo, Simba walikwama kupata viza zao juzi na jana na zinataraji kutolewa leo asubuhi kabla ya kuondoka saa 10:00 kwenda Sudan kupitia Nairobi ikiwa na wachezaji wote wa timu hiyo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alithibitisha juzi kuto
kea tukio hilo

Quran Yachomwa Moto Tena Marekani



NewsImages/6382646.jpg
Mchungaji Terry Jones alipoichoma moto Quran kushinikiza mchungaji wa Iran aachiwe huru

Mchungaji wa Marekani ambaye alizua kizaazaa mwaka jana alipoichoma moto Quran na kuweka video online, amezua tena balaa jingine kwa kuichoma moto Quran safari hii akisema anapinga kutupwa jela kwa mchungaji wa kanisa moja nchini Iran.
Mchungaji wa kanisa la Florida, Terry Jones, ambaye mwezi machi mwaka jana alisababisha mtafaruku duniani alipoichoma moto Quran, amezua balaa kwa mara nyingine kwa kuichoma moto Quran na picha walizozichora wakidai ni za mtume.

Tukio la kuchomwa moto Quran lilifanyika jumamosi usiku kwenye kanisa la mchungaji huyo la Dove World Outreach Center lililopo kwenye kitongoji cha Gainesville, Florida.

Takribani watu 20 walishuhudia tukio hilo ambapo mchungaji Jones alijifanya ni hakimu akitoa hukumu dhidi ya Quran akitaka mchungaji Youcef Nadarkhani, wa nchini Iran aachiwe huru.

Mchungaji Youcef Nadarkhani amehukumiwa kunyongwa nchini Iran kwa makosa ya uhalifu na ubakaji ambapo mashirika ya kutetea haki za binadamu yamedai sababu hasa ni kubadili kwake dini kutoka uislamu na kuingia kwenye ukristo. Alihukumiwa adhabu ya kifo mwaka 2010.

Pamoja na serikali ya Marekani kumshinikiza mchungaji Jones asihatarishe maisha ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan na kwingineko duniani kwa kuichoma moto Quran kwa mara nyingine, mchungaji Jones aliendelea na zoezi lake la kuichoma moto Quran jumamosi usiku na kulionyesha LIVE kwenye internet tukio hilo.

Mchungaji Jones aliichukua misahafu aliyoizamisha kwenye mafuta ya taa na kuichoma moto. Alichukua pia picha alizodai ni za mtume Muhammad (S.A.W) na kuzichoma moto.

Muda mfupi baada ya tukio hilo, kitengo cha zimamoto cha mji wa Gainesville kilitoa taarifa ya kulifikisha mahakamani kanisa la mchungaji huyo.

Zimamoto walidai kuwa kanisa hilo litapigwa faini ya dola 271 kwa kuchoma moto vitabu na pia litatakiwa kulipa gharama za kesi hiyo mahakamani.

Watu 12 walipoteza maisha yao sehemu mbali mbali duniani wakati mchungaji Jones alipoichoma moto Quran mwaka jana.
Askari wawili wa Marekani waliuliwa kwa kupigwa risasi nchini Afghanistan na mtu aliyevaa nguo kama polisi wa Afghanistan.

Katika historia yake, mchungaji Jones aliwahi kufukuzwa na waumini wake mwenyewe kwenye kanisa alilokuwa akiliongoza alipokuwa nchi

Friday, May 4, 2012





MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Juni 27, mwaka huu kutoa uamuzi kama washitakiwa wana kesi ya kujibu au la katika kesi inayowakabili mawaziri wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona pamoja na Katibu Mkuu mstaafu wa Hazina, Gray Mgonja.

Kesi hiyo inayowakabili mahakamani hapo ni ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 11.7.

Aidha, Hakimu aliyeiahirisha jana, Sam Lumanyika amepanga kesi hiyo kutajwa tena Mei 22, mwaka huu.

Kesi hiyo jana ilitajwa na kuangalia kama taratibu za Mahakama zimeenda kama ilivyopangwa baada ya mwenendo wa kesi kukamilika na washitakiwa kupewa kuandaa majumuisho na kuyawasilisha mahakamani.

Mawaziri hao wa zamani wa Fedha, Nishati na Madini, pamoja na Mgonja, wanadaiwa kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya ukaguzi wa dhahabu ya Alex Stewart (Assayers) ambayo haikustahili kupata msamaha huo.

Kampuni hiyo inadaiwa kuwa kama ingelipa kodi, Serikali ingepata faida kupitia kodi katika kipindi chote kutoka iliposajiliwa na Mamlaka ya Mapato (TRA), Oktoba 3, 2003, hivyo Serikali inadaiwa kupata hasara ya Sh 11,752,350,148.00 kati ya mwaka 2002 na Mei 2005.

Rais Kikwete ateua wabunge wapya









WAKATI kukiwa na shauku ya kutaka kujua Rais Jakaya Kikwete atakuja na Baraza gani la mawaziri, amefanya uteuzi wa wabunge watatu wapya.

Amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa mamlaka ya uteuzi aliyonayo chini ya Ibara ya 66(i) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, iliwataja wateule hao kuwa ni Profesa Sospeter Muhongo, Janet Mbene na James Mbatia. Uteuzi huo unaanza mara moja.


Kuteuliwa kwa wabunge hao watatu kunaleta hisia kuwa huenda miongoni mwao wakapata nafasi ya kuwa mawaziri kama Rais atafanya mabadiliko katika Baraza lake kutokana na tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa kwa baadhi ya mawaziri wake.


Kwa mujibu wa Ibara iliyotajwa hapo juu, Rais ana mamlaka ya kuteua wabunge 10 kujiunga na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wabunge hao walioteuliwa wanafanya idadi ya waliokwishateuliwa kufikia sita.


Wengine wa awali ni Zakia Hamdan Meghji, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa ambaye hivi sasa ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Shamsi Vuai Nahodha ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.


Wachunguzi wa masuala ya siasa wanadai kuwa uteuzi huo unaonesha dalili zote za Rais kuwa tayari kutangaza mabadiliko katika Baraza lake, katika utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).


Pia ripoti tatu za Kamati za Bunge za mwaka 2009/10, ambazo zimependekeza kuwajibishwa kwa baadhi ya watendaji serikalini, wakiwamo mawaziri wanane.


Taarifa iliyowasilishwa katika mkutano uliopita wa Bunge, ilizua mjadala mkali miongoni mwa wabunge hata kufikia kutaka kumpigia kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.


Hata hivyo, lengo lao lilikuwa ni kushinikiza mawaziri waliotajwa kwa ubadhirifu na CAG wajiuzulu kama si kuondolewa.


Mbatia ambaye ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi anakuwa mpinzani wa pili kuteuliwa na Rais Kikwete tangu aingie madarakani mwaka 2005.


Mpinzani wa kwanza kuteuliwa na Kikwete ni Ismail Jussa Ladhu wa CUF, ambaye ni Mwakilishi wa Mji Mkongwe, Zanzibar ambaye aliteuliwa katika muhula wa kwanza wa Rais Kikwete.


Hii ni mara ya pili kwa Mbene kuteuliwa na Rais Kikwete kuwa mbunge na hivi karibuni aligombea ubunge wa Afrika Mashariki kwa tiketi ya CCM lakini hakufanikiwa.


Profesa Muhongo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambaye anateuliwa kwa mara ya kawanza, ni Profesa wa Heshima wa Chuo Kikuu cha Pretoria, Afrika Kusini; mjumbe wa Taasisi ya Kitaaluma ya Jiolojia ya London, Uingereza; Mjumbe wa Heshima wa Taasisi ya Utafiti wa Jiolojia ya China, Mjumbe wa Heshima wa Taasisi ya Kitaaluma ya Sayansi ya Nchi Zinazoendelea (FTWAS).


Pia ni mjumbe wa Taasisi ya Kitaaluma ya Jiolojia ya Afrika (FGSAf) na Mjumbe wa taasisi zingine nane za kitaaluma za Sayansi duniani.


Alikuwa mtu wa kwanza kushinda tuzo ya Robert Shackleton mwaka 2004 baada ya kufanya utafiti kuhusu Jiolojia Afrika. Ni Makamu wa Rais wa Kamisheni ya Ramani ya Jiolojia ya Dunia (CGMW). Hakupata kuingia katika masuala ya siasa huko nyuma.


Mawaziri ambao walitawala mjadala wa Bunge huku wabunge wakiwatolea macho ili wang’oke ni Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo, Waziri wa Tamisemi, George Mkuchika, Waziri wa Kilimo na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe, William Ngeleja (Nishati na Madini), Omari Nundu (Uchukuzi), Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii), Dk Hadji Mponda (Afya na Ustawi wa Jamii), Dk Cyril Chami (Waziri wa Viwanda na Biashara).


Hata hivyo taarifa ya Ikulu haikusema wabunge hao wateule wataapishwa lini na wapi, lakini Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alipoulizwa jana alisema alisema kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, mtu yeyote anayeteuliwa kuwa mbunge, ataapishwa katika mkutano wa Bunge unaofuata baada ya uteuzi wake, bila kujali ni mbunge wa kuteuliwa au wa jimbo.


Ndugai alisema kwa msingi huo, wabunge hao wateule wataapishwa wakati wa Mkutano wa Nane wa Bunge la Bajeti unaotarajiwa kuanza mjini Dodoma, Juni 12.


Alipoulizwa itakuwaje ikitokea wateule hao wa Rais wakateuliwa pia kuwa mawaziri na kuendelea na kazi kabla ya kuapishwa kuwa wabunge, Naibu Spika alisema kwa hali ya kawaida, hilo haliwezekani.


“Kwa mujibu wa Katiba, mawaziri watateuliwa kutoka miongoni mwa wabunge, na anakuwa mbunge mteule hadi pale anapoapishwa, na ndiyo maana baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu, kazi ya kwanza ya Bunge ni kuchagua Spika na Naibu Spika, ambao baadaye watafanya kazi ya kuwaapisha wabunge, na ndipo atateuliwa Waziri Mkuu na kisha mawaziri,” alifafanua Naibu Spika.

 

kwa msaada wa habari leo