 Emmanuel Okwi
Ibrahim Bakari na Mashirika WAKATI
wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, Simba
wakiondoka leo kwenda Khartoum, Sudan tayari kwa mchezo wa marudiono
dhidi ya Al Ahly Shendi, washambuliaji nyota wa Wekundu hao wa
Msimbazi, Emmanuel Okwi na Felix Sunzu wameingia kwenye rekodi ya
wafungaji bora Afrika katika michuano ya Kombe la Shirikisho la soka
Afrika.
Okwi, raia wa Uganda na Felix Sunzu ambaye ni Mzambia,
wote wametajwa kuwa na mabao matatu kila mmoja kwa mujibu wa mtandao wa
tensport.com.
Mshambuliaji huyo anayechezea pia Uganda Cranes,
alifunga bao moja dhidi ya Entente Sportive de Setif katika mchezo wa
kwanza kati ya mawili walioshinda mabao 2-0 Dar es Salaam na moja
likifungwa na Haruna Moshi. Mchezo wa marudiano, Okwi alifunga moja
wakati Simba ikilala mabao 3-1. Mshambuliaji huyo alifunga dhidi ya Al
Ahly Shendi kati ya mabao matatu huku mengine yakifungwa na Boban na
Patrick Mafisango.
Kwa hali hiyo, Boban na Sunzu kila mmoja wana
mabao matatu. Sunzu aliyafunga katika mchezo walioshinda mabao 2-1 dhidi
ya Kiyovu ya Rwanda na lingine likifungwa na Parick Mafisango.
Mbali
na wachezaji hao, wengine wenye mabao matatu ni Komara, Niamba wote wa
Leopards ya Congo, Chinyengetere (Hwange ya Zimbabwe, Moco (InterClube
(Angola) na Raouf (ENPPI, Misri) na Seri wa Asec Mimosa ya Ivory Coast.
Mpaka sasa Fiston (Lydia Academic, Burundi) na Girma wa St George ya Ethiopia wana mabao manne kila mmoja.
Wakati
huo huo, msafara wa Simba unaondoka leo mchana kwenda Sudan kupitia
Nairobi, Kenya tayari kwa mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho
dhidi ya Al Ahly Shandy baada ya kukwama kuondoka kutokana na majambazi
kuvunja na kuiba katika ubalozi wa Sudan.
Juzi usiku majambazi
walivunja sefu ya kuhifadhia fedha na kuiba zaidi ya dola 40,000
ubalozini hapo pamoja fedha nyingine pamoja na kuiba kompyuta zote
zinazotumika kuhifadhia kumbukumbu mbalimbali.
Kutokana na hali
hiyo, Simba walikwama kupata viza zao juzi na jana na zinataraji
kutolewa leo asubuhi kabla ya kuondoka saa 10:00 kwenda Sudan kupitia
Nairobi ikiwa na wachezaji wote wa timu hiyo. Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alithibitisha juzi kutokea tukio hilo |
No comments:
Post a Comment