
Wachezaji
na viongozi wa timu ya Simba wakiwa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Amos Makalla (katikati aliyeshika kombe).

TIMU
ya Simba SC ya jijini Dar jana ilisherehekea ubingwa wake wa 2011/2012
pamoja na mashabiki wake katika ukumbi wa burudani wa DAR LIVE.
Sherehe
hizo zilitanguliwa na msafara wa magari, pikipiki na watembea kwa miguu
ambao walianzia safari yao makao makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Msimbazi
na kupitia mitaa kadhaa ya jiji kabla ya kumalizikia katika ukumbi wa
Dar Live.
Katika msafara huo wachezaji wa Simba walikuwa katika
lori la wazi lililopambwa bendera na vitambaa vya rangi nyekundu na
nyeupe huku wakiwa na kombe lao walilolibeba.

Mashabiki
na wapenzi wa Simba SC wakiwa katika msafara kuelekea katika Ukumbi wa
Dar Live kusherehekea ubingwa wa timu yao jana.

Wachezaji na viongozi wa Simba wakifungua shampeini wakati wakisherehekea ubingwa wao ndani ya ukumbi wa Dar Live jana

Meneja
wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (kulia) akimkabidhi nahodha
wa Simba SC, Juma Kaseja shilingi milioni 3 zilizotolewa na Dar Live
kama pongezi kwa timu hiyo kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom
2011/2012

Naibu Waziri Amos Makala akimvisha medali Uhuru Selemani

Wachezaji wa Simba wakipata menyu pembeni ya kombe lao

Baadhi ya mashabiki waliohudhuria sherehe hizo.
No comments:
Post a Comment