Kesi hiyo inayowakabili mahakamani hapo ni ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 11.7.
Aidha, Hakimu aliyeiahirisha jana, Sam Lumanyika amepanga kesi hiyo kutajwa tena Mei 22, mwaka huu.
Kesi hiyo jana ilitajwa na kuangalia kama taratibu za Mahakama zimeenda kama ilivyopangwa baada ya mwenendo wa kesi kukamilika na washitakiwa kupewa kuandaa majumuisho na kuyawasilisha mahakamani.
Mawaziri hao wa zamani wa Fedha, Nishati na Madini, pamoja na Mgonja, wanadaiwa kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya ukaguzi wa dhahabu ya Alex Stewart (Assayers) ambayo haikustahili kupata msamaha huo.
Kampuni hiyo inadaiwa kuwa kama ingelipa kodi, Serikali ingepata faida kupitia kodi katika kipindi chote kutoka iliposajiliwa na Mamlaka ya Mapato (TRA), Oktoba 3, 2003, hivyo Serikali inadaiwa kupata hasara ya Sh 11,752,350,148.00 kati ya mwaka 2002 na Mei 2005.
No comments:
Post a Comment