Monday, January 23, 2017

Trump awafuta kazi mabalozi wa Marekani duniani kote

Rais wa Marekani Donald Trump
amewafuta kazi mabalozi wote wa nchi
hiyo kote duniani na wanaohudumu
katika mashirika ya kimataifa.Kwa
mujibu wa taarifa ya mtandao wa
Independent, mabalozi hao wametakiwa
kuachia nafasi zao mara moja na
kurudi nyumbani.
Kiongozi huyo juzi alifanya ziara yake
ya kwanza katika ofisi za makao makuu
ya shirika la Ujasusi la Marekani CIA,
na kuvituhumu baadhi ya vyombo vya
habari nchini humo wakati akitoa
hotuba yake, kwamba vinawagawa
wananchi.Zaidi ya mabalozi 80 wa
Marekani katika nchi mbali mbali
duniani walifutwa kazi Ijumaa tarehe 20
Disemba saa sita mchana punde baada
ya Trump kuapishwa.
Hatua hiyo ya Trump inatazamiwa
kuvuruga uhusiano na waitifaki
muhimu kama vile Ujerumani,
Uingereza, Canada. Inatabiriwa kuwa
nchi hizo zinaweza kukaa bila mabalozi
kwa miezi kadhaa kwani baada ya
Trump kuteua mabalozi wapya
watalazimika kuidhinishwa na Bunge la
Kongresi kabla ya kuanza kazi zao.
Source: Independent

No comments:

Post a Comment