Wednesday, January 25, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma awajia juu wanaokwamisha watoto kwenda shule


Na Riziki Manfred Bonzuma
Mbinga
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mh Binilith Mahenge amemaliza ziara yake ya siku mbili wilaya mbinga huku lengo la ziara hiyo ni kukagua mwenendo wa kuripoti kwa wanafunzi wa awali darasa la kwanza na kidato cha kwanza pamoja na kuzungumza na wananchi wa mbinga
Ziara hiyo iliyo Anza kwa kutembelea shule ya sekondari Ndyosa na shule ya msingi Mibuni akiwa shuleni hapo mh amehenge alikagua vyumba ya walimu 6 yaani six in one vyumba vya madarasa ambapo amemuagiza mkandarasi wa mradi hiyo anahakikiasha anakabithi baada ya Wiki mbili
  Pia Mahenge aliwaagiza watendaji wa vijiji kuhakikisha wanawakamata wazazi wawanafunzi ambao bado mpaka sasa hawajaripo katika shule walizo pangiwa na wale wenye umri wa kuanza darasa la kwanza pamoja na awali
Akiwa wilaya mbinga mkuu wa Mkoa alifanya mkutano wa hadhara na wananchi wa mbinga mjini ambapo Mahenge Alitalia mkazo suala la kujali mazingira hususani vyanzo vya maji ambapo ameuagiza uongozi wa halmashauri kuhakikisha wanaweka  alama ndani ya mita 60 ili kusaidia mwananchi kutambua maeneo ya vyanzo vya maji
Awali wananchi walio furika kumsikiliza mkuu wa Mkoa walipata fursa ya kuuliza maswali ambayo yote alijibiwa na wakuu wa Idara pamoja na viongozi wa wilaya
  Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Gombo Samandito Gombo ameahidi kuendelea kuzitatua changamoto mbalimbali hususani katika suala la ujenzi wa miundombinu katika sekta ya elimu na kuhakikisha mapato yanaongezeka mara dufu kwa kuanzisha vyanzo vipya vya mapato ikiwemo uwekezaji katika madini hususani makaa ya mawe

No comments:

Post a Comment