Monday, January 23, 2017

Majambazi wauwawa Mwanza

Watu wawili waliokuwa wakituhumiwa kwa
ujambazi wameuawa wakati wakitaka kujaribu
kuwatoroka askari polisi wilayani Ilemela mkoani
Mwanza
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza amesema
kwamba tukio hilo lilitokea tarehe 20.01.2016
majira ya saa 2:30 usiku, katika mtaa wa
kiloleli “A” kata ya Nyasaka mkoa wa Mwanza
na kuwataja majambazi waliouawa kuwa ni Eric
Magese miaka 22, na aliyejulikana kwa jina
moja la Peter miaka kati 25 hadi 27 wote
wakazi wa Mecco jijini Mwanza.
Amesema majambazi hao waliuawa wakati
wakijaribu kutoroka askari polisi pindi
wakiwapeleka mahali ambapo wenzao
wamejificha ili waweze kufanya uvamizi.
Amesema kuwa katika tukio hilo pia ilipatikana
silaha moja aina ya short gun yenye namba TZ
CAR 103283 ikiwa na risasi tatu ambayo
inadaiwa walipora kwenye kampuni ya ulinzi
iitwayo Malika Security Service Limited
Msangi amesema majambazi hao walikuwa
wakitafutwa na polisi baada ya kufanya
unyang’anyi wa kutumia silaha katika maeneo
mbalimbali jijini Mwanza ilikiwemo tukio la
Kitangiri mnamo tarehe 19.12.2016 na tukio la
tarehe 02.01.2016 katika mtaa wa Nyasaka.
Jinsi walivyouawa
Msangi amesema baada ya upelelezi
uliofanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao,
walikubali kuwapeleka askari katika eneo
ambalo walikuwa wamepanga pamoja na
wenzao wawili kwa ajili ya kufanya matukio
zaidi ya ujambazi.
Amesema walipofika katika eneo hilo,
watuhumiwa hao walipiga kelele kama ishara ya
kuwatorosha wenzao na kuanza kuwakimbia
askari.
Askari walifyatua risasi kadhaa hewani
wakiwaamuru wasimame lakini waligoma ndipo
waliwafyatulia risasi za mguuni kwa bahati
mbaya ziliwalenga maeneo ya juu ambapo
walifariki dunia wakati wakipelekwa hospitali.

No comments:

Post a Comment