Thursday, January 19, 2017

Mkuu wa wilaya mbinga Hakuna Njaa

Mkuu wa wilaya ya Mbinga Consimas Mshenyi amewataka wananchi wilayani hapa kuhakikisha watunza ziada ya chakula walichonacho kutokana na hali ya mvua kuto ridhisha  licha ya kusema hakuna njaa katika wilaya yake

Akitoa taarifa mbele ya waandishi wa habari kuhusu hali ya chakula katika wilaya hiyo mkuu huyo wa wilaya amesema mpaka sasa vituo vya hifadhi ya chakula wilayani hapo vina zaidi ya tani 300 huku ziada kutoka kwa wananchi ikiwa ni tani 10,000 (elfu kumi) za mahindi huku mchele ikiwa ni tani 18,000 (elfu kumi na nane) “nawataka wananchi waendelee kuhifadhi ziada ya chakula walichonacho kwani hali ya mvua si nzuri na ziada hiyo inaweza kupungua pia ziada hiyo inaweza saidia hata kwa majirani zetu” alisema Mishenyi

Aidha Mishenyi alisema kuwa hali mazao yaliyopo shambani yapo katika hali nzuri licha ya mvua kunyesha katika hali yakutolidhisha lakini kuna uhakika wa mazao hayo kukomaa na kuvunywa kwa wakati hivyo akawataka wananchi hususani wakulima kuhakikisha wasimamia utanzaji kwa kushirikiana na wataalamu wa kilimo

Katika hatua nyingine mkuu huyo nwa wilaya amepiga marufuku unywaji na uuzwaji wa pombe nyakati za kazi kwani kunazoletesha maendelea ya nwilaya hiyo “sitawavumilia wanaokunywa saa za kazi na wanaocheza pool table  nyakati za mchana yaani saa za kazi nitawamuagizaa kupitia kwa afisa biashara mkurugenzi kufuta leseni kwa wale vwote watakao kiuka mashart ya biashara zao ikiwemo kuuza pombe katika saa za kazi”
 
Kuhusu uchaguzi mdogo wa udiwani utakao fanyika januari 22 mwaka huu  katika kataa ya maguu wilayani hapa Mishenyi amewataka wanachi kupiga  kwa amani na kurejea makwao kusubiri matokeo na kupiga kura katika hali ya uturivu pia akawaomba wagombea kuto kuwa vyanzo kuvuruga amani nauturivu na kuwahakikishia ulinzi wa wa kutosha katika uchaguzi huu

No comments:

Post a Comment