Saturday, January 21, 2017

Kassim majaliwa aunguruma Makete

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa ametoa kiasi cha Shilingi Milioni 5 za kukamilisha ukarabati wa Zahanati ya kijiji cha Ivalalila ambayo ni kubwa kuliko zote Wilayani hapa na imejengwa kwa nguvu za Wananchi na ushirikiano na Serikali

Waziri Mkuu ametoa fedha hizo kufuatia msafara wake uliotokea Matamba kusimamishwa kwa Mabango katika kijiji hicho cha Ivalalila wakidai kuongezewa wahudumu wa afya na Serikali iwasaidie kukamilisha ukarabati wa Zahanati yao

Baada ya kuona Mabango hayo Waziri Mkuu alilazimika kusimama na kuwasikiliza Wananchi hao na kuahidi kutoa fedha hizo haraka ili zisaidie kukamilisha Zahanati hiyo, pia amemwagiza Mkurugenzi wa Wilaya ya Makete Ndg. Fransis Namaumbo kuhakikisha anaongeza wahudumu wa afya katika Zahanati hiyo mara baada ya ajira mpya

Waziri Mkuu alianza Ziara yake jana katika kata ya Matamba hapo jana,kukagua Shamba la Mifugo Kitulo,Kuwasalimia Wananchi wa kijiji cha Ujuni,alisimamishwa Ivalalila na Wananchi na kuhitimisha Ziara yake katika uwanja wa Mabehewani Makete Mjini

Lengo la ziara ya Waziri Mkuu ni kukagua miradi ya Maendeleo inayosimamiwa na Serikali huku akipokea kero kubwa ya Maji katika Vijiji vya kata ya Matamba na kata ya Kinyika, Ujuni ambapo  amemwagiza Kaimu Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Wilaya ya Makete Sylvester Ndaki kuhakikisha kuanzia jumatatu ya Wiki ijayo anaanza kushughulikia matatizo hayo ya maji kwa Wananchi

No comments:

Post a Comment