Waziri wa zamani na Mbunge wa jimbo la
Mufundi Kaskazini Mkoani Iringa, Joseph Mungai
amefariki dunia jioni ya leo jijini Dar es Salaa
mujibu wa taarifa ya habari ya ITV, Mzee
Mungai amekutwa na umauti baada ya kuanza
kutapika mfululizo, familia imedia kuwa tatizo
hilo limemkuta baada ya kudaiwa kula kitu
kibaya.
Afisa Uhusiano wa Hospitali wa Taifa Muhimbili,
Aminiel Aligaesha amesema mwili wa Marehemu
Mungai umepokelewa katika idara ya magonjwa
ya dharura na kuthibitisha kifo saa 11:20 jioni
Amesema mwili wake umehifadhiwa chumba
cha kuhifadhi maiti Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mwanasiasa huyo mkongwe nchini alikihama
chama chake cha CCM na kujiunga na chama
cha siasa cha CHADEMA katika harakati za
uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Tuesday, November 8, 2016
Msiba mwingine Mungai nae afariki
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment