Kufuatia kifo cha aliyekuwa Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanza nia
(2005-2010), Samuel Sitta, mwanae wa kiume
ameweka wazi maneno matatu ya mwisho
aliyoyatamka, yenye maana nzito katika maisha.
Akizungumza nyumbani kwa marehemu, Meya
wa Kinondoni, Benjamini Sitta ambaye ni mtoto
wa kiume wa marehemu, alisema kuwa baba
yake alitoa maneno matatu ya kuukubali ukweli
wa maisha baada ya Daktari kumueleza kuwa
asingeweza kupona.
“That’s life (hayo ndiyo maisha),” Benjamin
alikariri maneno ya baba yake. Alisema hayo
yalikuwa maneno yake ya mwisho baada ya
kuelezwa ukweli na daktari wa hospitali ya
Technical University of Munich nchini Ujerumani
alipokuwa akipatiwa matibabu.
Maneo ya Sitta ni funzo kubwa kwa watu wote
kuwa maisha huanza na huisha, hiyo ndiyo
maana ya maisha na hakuna aishie milele hivyo
tuishi kwa kuzingatia maana hiyo ya maisha na
kuikubali.
Sitta ambaye anakumbukwa kwa kauli mbiu
yake na matendo ya kusimamia ‘kasi na
viwango’, alifariki kutokana na ugonjwa wa tezi
dume uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.
Alitangaza kustaafu siasa muda mfupi baada ya
kukamilika kwa kampeni za uchaguzi mkuu wa
mwaka jana, ambapo yeye alikuwa mmoja kati
ya waliokuwa msitari wa mbele kumnadi
mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi, Dkt.
John Magufuli aliyeshinda uchaguzi huo.
Benjamini alieleza kuwa marehemu atazikwa
Urambo Mkoani Tabora na kwamba ratiba ya
mazishi itatolewa na Ofisi ya Bunge ambayo
ndiyo inayoratibu mazishi
“Tumempoteza baba na kiongozi ambaye tulikuwa
tunamtegemea kwa ushauri na masuala
mbalimbali, tutafuata yale aliyokuwa akituelekeza,”
alisema Benjamini.
Hakika Taifa limempoteza mtu muhimu, pengo
lake halitazibika kamwe. Bwana alitoa, Bwana
ametwaa, jina lake lihimidiwe!
Monday, November 7, 2016
Kauli ya mwisho ya Samuel sitta
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment