TIMU
ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' jana usiku imechapwa magoli 3-0
dhidi ya Misri katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya
Afrika (Afcon 2017) iliyochezwa mjini Alexandria.

Magoli
ya Misri yalifungwa dakika ya 61' na Rami Rabia, dakika ya 65' na Basem
Morsi na msumari wa mwisho ukatiwa kimiani dakika ya Mohamed Salah
dakika ya 70'.
Stars walijitahidi kuwazuia Misri kwa dakika 60', lakini walipoteza mwelekeo ndani ya dakika 10' tu na kupigwa magoli matatu.
Kipigo
hicho kinaiingiza Stars kwenye orodha ya nchi nyingine zilizopokea
kichapo jana ambapo imeshika namba mbili kwa kufungwa magoli mengi
katika mechi za jana jumapili.
Mauritius ndio vinara wa kuburuzwa jumapili ya jana kwani walifungwa 7-1 na timu bora ya Ghana.

No comments:
Post a Comment