MZEE YUSUF AANGUSHA BONGE LA BURDANI, ATANGAZA NIA DAR LIVE
KAMA kawaida yake, mfalme wa muziki wa mwambao, Mzee Yusuf, na kundi lake la Jahazi Modern Taarab, usiku wa jana aliangusha bonge la burudani kwa mashabiki katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live ulioko Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.
Burudani hiyo ilifanyika sambamba na kutambulishwa kwa nyimbo zao mpya katika albamu ya ‘Mahaba Niue’ na kutangaza kwamba atagombea ubunge mwaka huu katika jimbo moja huko Mjini Magharibi, Zanzibar, katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment