Wataka waruhusiwe kujiua Uingereza
Wanaume wawili wenye ulemavu mbaya zaidi wanakwenda mahakamani kukata rufaa katika kesi inayoonekana kuwa moja ya kesi inayotaka mageuzi makubwa ikitaka kubadilisha sheria za serikali kuhusu haki ya mtu kufa.
Mmoja wa watu hao, Pail Lamb amekuwa na ulemavu
mbaya kwa miaka mingi pamoja na kupitia uchungu mwingi, hawezi kujitoa
uhai wake na anataka madaktari waruhusiwe kumuua bila ya kukabiliwa na
kosa la mauaji baadaye.
Mwanamume mwingine anayejulikana kama Martin,
anataka uamuzi utakaowaruhusu madaktari wamsaidie kujiua ingawa waweze
kulindwa kutokana na sheria za kuweza kuwashtaki kwa kufanya kitendo cha
mauaji.
Wakosoaji wanasema kuwa ikiwa mahakama itaruhusu
wawili hao wajiue, itakuwa na athari kubwa kwa watu wazee na wenye
ulemavu kutaka kujinyonga ili kuzuia kuwahangaisha jamaa zao
kuwahudumia.
CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment