Wagonjwa wa kiakili watoroka hospitalini Kenya
Polisi wanawatafuta wagonjwa
karibia arobaini waliotoroka kutoka hospitali ya watu wenye matatizo ya
kiakili, mjini Nairobi ya Mathare. Wagonjwa hao wanasemekana
waliwashinda nguvu walinzi wao na kutoroka.
Zogo hilo lilizuka katika hospitali ya Mathare baada ya kutokea hali ya sintofahamu iliyowahusisha wafungwa arobaini wanaume.
Baadhi ya vyombo vya habari vinasema kuwa wagonjwa hao walikuwa wanateta kuhusu hali mbaya na kibinadamu
CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment