Vita dhidi ya ufisadi nchini China
Maafisa wa Uchina wameanzisha
uchunguzi juu ya afisa wa ngazi ya juu katika kile kinachoonekana kama
hatua ya hivi karibuni ya kiongozi wa nchi hiyo Xi Jinping ya
kukabiliana na ufisadi.
Katika ripoti fupi iliyotolewa na serikali ya
Uchina kupitia shirika la habari la uchina Xinhua imesema kuwa Liu
Tienan - mkuu wa sera za uchumi - alisimamishwa kazi baada ya
kushutumiwa kukiuka vikali nidhamu.
Hii ni kesi ya kwanza kwa afisa wa
ngazi ya juu wa uchina kutolewa hadharani tangu mwaka jana baada ya
mwandishi wa habari wa kichina kumshutumu wazi Bwana Liu kwa ufisadi ,
kugushi vyetii vyake vya elimu na kutishia kumuua hawara wake .
Nchini Uchina ambako vyombo vya habari vinabanwa
, shutuma hizi ni kubwa dhidi ya afisa wa ngazi ya juu. Lakini sasa
maafisa wanasema bwana Liu anachunguzwa , licha ya kwamba hawakueleza
bayana anakabiliwa na shutuma gani hasa .
Tangu aingie mamlakani Rais Xi Jinping - aliapa
kukabiliana na ufisadi , akionya kuwa ni tisho kwa utawala wa chama
chake cha kikomunisti .
Uchunguzi huu utaangaliwa kama jaribio kwa rais mpya la kuweza kushawishi umma kuwa anaweza kweli kumaliza uhalifu huo
CHANZO :BBC
No comments:
Post a Comment