akiwa katika mahojiano na Blog ya www.kalulunga.com
Na, Gordon
Kalulunga, Mbeya
WANANCHI
waliojiajiri wakiwemo Mama Ntilie, Machinga na wengine wenye vipato vidogo na vikubwa ambao hawako kwenye
sekta rasmi za ajira, wametakiwa kujiunga na mfuko wa pensheni wa watumishi wa
umma kwa kuchangia kwa hiari.
Akizungumza
na mtandao wa www.rizikimgaya.com Afisa
mfawidhi wa PSPF mkoa wa Mbeya Side Kipindula, amesema kuwa mfuko huo
umeanzisha utaratibu wa kuwakomboa wananchi hasa ambao hawako kwenye mfumo
rasmi wa ajira.
‘’Baada ya
kujikita kwa wafanyakazi walio kwenye ajira rasmi, sasa mfuko umeona ni jambo
jema kwenda pia kwa wananchi ambao hawapo kwenye mfumo rasmi wa ajira kwa
kuwapa mafao wale wanaohamasika kujiunga’’ alisema Kipindula.
Alisema kwamba,
mwananchi ambaye anataka kujiunga na mfuko huo kupitia uchangiaji wa hiari
anatakiwa kila mwezi kuchangia Shilingi 10,000/= ama zaidi na hata anapokwama
hashurutishwi kuchangia.
Amezitaja faida
za kuchangia mfuko huo kwa hiari ambazo ni kupata mafao ya elimu, mafao ya mwanachama anayeamua kujitoa,
ujasiliamali nk.
‘’Faida za mwanachama
anayejiunga nasi katika mfumo wa uchangiaji wa hiari ni kubwa ikiwemo kukopa
fedha baada ya kuchangia kwa miezi 12 ambapo mwanachama anayechangia fedha
kubwa kila mwezi anaweza kukopa muda wowote’’ alisema afisa huyo.
Aliitaja faida
nyingine kubwa kuwa ni pamoja na kila mwanachama kuwekewa fedha za faida
kutokana na gawio la faida ya mfuko huo kulingana na kiasi alichoweka kwenye
mfuko wa PSPF kila mwezi.
Fedha hizo huwekwa kwenye kila akaunti ya mwanachama mwezi Januari na mwezi Juni.
Anatoa wito
kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiunga na mfuko huo hasa kupitia mfumo wa
uchangiaji wa hiari ambao alisema kuwa anaamini wananchi wengi wapo katika
ajira zisizo rasmi.
Kwa upande
wa wanachama ambao wapo kwenye ajra rasmi, alisema shirika hilo limeanzisha
mpango wa kujenga nyumba na kuwakopesha.
Sifa za mwanachama anayeweza kukopa
hizo nyumba za kuishi ni yule aliyechangia kwa miaka mitano na kuendelea.
‘’Kwa mkoa
wa Mbeya tupo katika harakati za kutafuta viwanja na pindi tutakapopata
tutaanza kupokea maombi ya wanaohitaji kukopa nyumba hizo, lakini kwa wale
waliokaribia kustaafu na kubakiza miaka mitano kazini tunawapa fedha taslimu nusu ya kiinua mgongo
chao’’ alisema Side Kipindula.
No comments:
Post a Comment