BUNGE limeelezwa kuwa ifikapo mwaka 2020 tembo watakuwa
wametoweka nchini iwapo kasi ya ujangili wa wanyama hao itaendelea bila
kudhibitiwa.
Kwa sasa idadi ya tembo imeelezwa kupungua kutoka 109,000 mwaka 2009 na kufikia 70,000 mwaka jana, hali ambayo inachangiwa na ongezeko la ujangili nchini.
Hayo yalisemwa bungeni jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli, alipokuwa akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2013/2014.
Lembeli alisema kuwa kwa sasa ujangili wa tembo nchini umekuwa ni janga la kitaifa ambapo kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori zinaonesha kwamba tembo wasiopungua 30 huuawa kwa siku, 850 kwa mwezi na kwa mwaka ni 10,000.
“Hali hii ni hatari na aibu kwa nchi yetu ambayo ni ya pili barani Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya tembo, kinachosikitisha ni wizara kuwa na kigugumizi katika kuitikia kauli ya Rais Kikwete iliyoitaka wizara kuomba msaada kwake kama tatizo la ujangili limewashinda,” alisema.
Alisema ili kunusuru wanyama hao kuweko katika mapori nchini kamati iliiagiza serikali kufanya operesheni kwa nchi nzima na kufanyia marekebisho sheria ya wanyamapori na kuweka adhabu kali kwa watakaothibitika kuhusika na ujangili wa tembo.
Katika hatua nyingine, kamati hiyo ilisikitishwa na kitendo cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuzuia silaha bandarini ikidai kodi, silaha hizo zilinunuliwa na wizara kwa ajili ya kufanikisha mchakato wa kupambana na ujangili, hivyo iliiagiza serikali kuruhusu utoaji japo kwa masharti.
Waziri Kagasheki
Awali Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki, akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo alisema katika kuimarisha ulinzi wa wanyamapori zilifanyika jumla ya doria 59,338 ndani na nje ya mapori ambapo jumla ya watuhumiwa 1,215 walikamatwa.
Mbali na watuhumiwa hao pia zilikamatwa bunduki 85 na risasi 215 za aina mbalimbali, ambapo kesi 670 zilifunguliwa katika mahakama mbalimbali nchini, kati yake 272 zilikwisha na washtakiwa 247 walilipa faini ya sh milioni 175.002 na washtakiwa 71 walipewa adhabu ya vifungo vya miaka 99.
Aidha, kesi 398 zenye jumla ya washtakiwa 897 bado zinaendelea katika mahakama mbalimbali nchini ambapo wizara ilifanya operesheni ya kiintelijesia wilayani Liwale na Tunduru na kukamata watuhumiwa 354, bunduki 435 za aina mbalimbali na risasi 1,129, maganda 514, mbao 10,332 na nyara mbalimbali za serikali zenye thamani ya sh milioni 855.014.
Kagasheki aliomba kuidhinishiwa sh bilioni 75.6, kati ya hizo sh bilioni 64 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh bilioni 11 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

No comments:
Post a Comment