Dar es Salaam. Linapotajwa jina la Sambwee
Shitambala, linaakisi sura nyingi za aina tofauti – Ni mwanajeshi,
mwanasheria, mwanasiasa wa upinzani na dani ya chama tawala. Kuyaweza
yote hayo ndani ya muda mfupi, ndiyo sababu ya safu hii kutaka
kumfahamu, Endelea.
Swali: Hongera kwa kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC)
Jibu: Asante sana
Swali: Ulipata nafasi hii yenye ushindani CCM mara tu baada ya kujiengua Chadema, nini kilikusaidia kuipata?
Shitambala: Kweli, ushindani ni
mkubwa na wagombea wengi ni wenye sifa na uwezo wa kila namna.
Kilichonisaidia ni sera yangu binafsi ya kuendesha siasa nikilenga
kuleta maendeleo kwa wananchi hata kama sijawa na uongozi wa
kuchaguliwa.
Swali: Una mfano wowote unaoonesha uhalisia wa maelezo yako?
Shitambala: Ndiyo, kwa mfano sasa
nimejikita kuleta maendeleo kwa vijana Mbeya mjini, kwa kuanzia
nimewaunganisha wasiokuwa na ajira, wenye ajira zisizo rasmi na wakulima
katika vikundi na kuwawezesha kimawazo na mitaji.
Kati ya Februari mwaka jana na sasa nimeunda
vikundi vitano; Ibala Hope Center, Uyole Center, Nsalaga Center, Kabwe
Center na Mabatini Center vyote vinahusisha vijana wa rika tofauti,
vikilenga kuwajengea uwezo kifikra na kiuchumi ili wajiletee maendeleo.
Miongoni mwa shughuli zinazotekelezwa na vijana
walio katika vikundi hivyo ni pamoja na, kushona nguo na kudarizi,
ukulima na kutengeneza matofali yanayotumika katika ujenzi bila kutumia
saruji.
Swali: Wewe ulikuwa mwanajeshi na mwanasheria, ilikuwaje ukaingia katika siasa?
Jibu: Baada ya kutoka jeshini
mwaka 2006, nilianzisha ofisi yangu ya uwakili jijini Dar es Salaam.
Absalom Kibanda alikuwa mmoja wa marafiki zangu wa karibu, hivyo
nilikuwa nikimtembelea ofisini kwake, Tanzania Daima, ndipo
nilipofahamiana na Freeman Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema - taifa) ambaye
alinishauri kuingia kwenye siasa na kupendekeza nikagombee kwenye
uchaguzi mdogo wa ubunge Mbeya Vijijini, mwaka 2008.
Swali: Katika uchaguzi huo wewe mgombea wa Chadema ulienguliwa; nini kilitokea?
No comments:
Post a Comment