Wednesday, May 1, 2013

MTOTO WA AJABU AZALIWA MPANDA

MKAZI wa Mtaa wa Makanyagio, Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Johari Raphael (35) amejifungua mtoto wa kiume mwenye viungo vya ajabu tofauti na vya binadamu wa kawaida.


Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda, Naibu Mkongwa, alisema mwanamke huyo alijifungua mtoto mweye kichwa kikubwa kama cha mtu mzima huku mikono na miguu yake ikiwa mifupi kama pingili ya miwa.
Hata hivyo, alisema mtoto huyo aliyezaliwa akiwa na kilo 4.5 alifariki dunia muda mfupi baada kuzaliwa kwa njia ya upasuaji.

Alisema walilazimika kumzalisha mwanamke huyo kwa njia ya upasuaji baada ya kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida.
Alisema hali ya Johari ambaye amelazwa katika wodi ya wazazi inaendelea vizuri na wanasubiriwa ndugu zake ili wakabidhiwe mwili wa marehemu kwa ajili ya mazishi.
Muuguzi Mkuu wa hospitali hiyo, Alexander Kasagula, alisema hili ni tukio la pili ndani ya kipindi cha miezi mitatu kuzaliwa mtoto wa ajabu, kwani miezi mitatu iliyopita alizaliwa mtoto huku utumbo ukiwa nje.

No comments:

Post a Comment