Baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakiwa na mtendaji mwenzao wa kata iliyoibuka mfanyakazi bora
Mkurugenzi wa kampuni ya chai Mufindi ya Kisigo Bw Daud Kisigo (kulia ) akimkabidhi zawadi yake ya hundi kwa ajili ya kununua bati 15 mfanyakazi bora Jackobo Mlela mbele ya mgeni rasmi kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Leticia Warioba (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya mei mosi Iringa leo (picha na Francis Godwin)
Mfanyakazi bora ktk Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
pozi la wafanyakazi bora Iringa
Kaimu mkuu wa mkoa Dr Leticia warioba Akimkabidhi mfanyakazi bora kutoka Kisigo Tea Compuny Bw Jackobo Malela zawadi yake ya bati 15
Wafanyakazi wa Tanroads mkoa wa Iringa na furaha ya ushindi wa michezo
Mgeni rasmi katika siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mos) mkoa wa Iringa kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Leticia Warioba (wa tatu kutoka kushoto waliokaa mbele) akiwa na baadhi ya viongozi wa maadhimisho hayo na viongozi wa serikali mkoa wa Iringa pamoja na wafanyakazi bora wakiwemo waliopewa ahadi hewa ya zawadi zao
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu (kushoto) akiwa na mkurugenzi wa Halmashauri ya Iringa vijijini ,Halmashauri ya Manispaa na mtaalam wa afya kutoka Hospitali ya mkoa wa Iringa leo
Na Francis Godwin, Iringa
WAKATI maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yamefanyika leo kote ulimwenguni na kitaifa kufanyika mkoani Mbeya ikiwa ni pamoja na kuwazawadia wafanyakazi bora hali ya mambo katika mkoa wa Iringa imekuwa tofauti baada mgeni rasmi kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Leticia Warioba kudanganywa na baadhi ya waajiri kutoa zawadi hewa kwa wafanyakazi bora.
Hatua ya mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kufanya uchunguzi juu ya zawadi wanazopewa wafanyakazi bora kama ni zawadi halisi ama mkopo ilikuja baada ya kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi bora waliotangazwa miaka ya nyuma kudai kuwa kuwa baadhi ya waajiri wamekuwa wakitafuta sifa katika sherehe hizo kwa kuwatangaza wafanyakazi bora bila ya kuwapa zawadi zao.
Aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Warioba alipoulizwa kuhusu udanganyifu huo uliofanywa kwa wafanyakazi hao alikiri kukabidhio bahasha ambazo baadhi zilikuwa zimeandikwa fedha nyingi ila bado zilikuwa nyepesi zaidi kama ndani hakuna kitu chochote.
" Kweli mimi sikuweza kuzifungua bahasha hizo ila ulichoniuliza ni kweli kabisa bahasha nyingine zilikuwa hazionyeshi kama zina kitu ndani na mimi napongeza uchunguzi wako ulioufanya utatusaidia kuwabana viongozi wa wawafanyakazi ili kufuatilia hilo"
Dr Warioba ambae ni mkuu wa wilaya ya Iringa pia alipongeza ofisi za serikali mkoa wa Iringa ikiwemo ofisi ya mkuu wa mkoa ,Hospitali ya mkoa wa Iringa, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa , TANAPA pamoja na taasisi binafsi chai Mufindi ya Kisigo Tea Compuny kwa kuwa mfano katika zawadi na nyingine ambazo zimeshiriki vema kwa kutoa zawadi za kweli sio mkopo wa zawadi.
Awali baadhi ya wafanyakazi bora waliotangazwa mwaka jana walimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa fedha zao kama wafanyakazi bora mwaka jana na juzi hadi leo bado kulipwa fedha hizo zaidi ya kupewa vyeti na baadhi yao kulipwa fedha nusu .
Hivyo kutaka serikali ya mkoa wa Iringa kusimamia msimamo wake uliotolewa na aliyekuwa kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Kepten mstaafu Aser Msangi ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Njombe kwa kuahidi kuzifungua bahasha za wafanyakazi bora na kuhakikisha wanapewa fedha zao taslimu badala ya kukopwa .
Hata hivyo kabla ya maadhimisho hayo jitihada za kumsaka mratibu wa maadhimisho hayo ili kujua kama wamefanya utaratibu wa kuchunguza zawadi za wafanyakazi bora zimefanyika ama lah ! ila kamati ya maadhimisho hayo chini ya mratibu wake Bw Deus Magesa ilieleza kulifanyia kazi suala hilo na kuwa kila bahasha ya mfanyakazi atakaye tangazwa kuwa ni mfanyakazi bora itafunguliwa ila haikuwa hivyo.
Wakati kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi (TUICO) mkoa wa Iringa Thomas Mashaka ambae pia ni mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi mkoa wa Iringa (TUCTA) alisema kuwa mbali ya kuwabana waajiri ila ni kweli baadhi yao wamekabidhi ahadi na sio zawadi zilizotangazwa.
Mashaka alitoa muda wa siku tatu kwa waajiri wote waliotoa ahadi hewa kuhakikisha wanatimiza ahadi hizo kwa kuwapa zawadi zao waliotangazwa kuwa ni wafanyakazi bora.
"Ni kweli ndugu mwandishi wa habari baadhi ya watu wametoa zawadi hewa hawakutoa hundi wala pesa taslimu kama walivyoandika katika bahasha ....ila wapo walioahidi radio pia hawakuweza kuzileta radio pale ila tulipowauliza walidai maandalizi ....sasa sisi kama chama tutafuatilia kuona wahusika wamepewa zawadi zao hadi jumamosi kila kitu kitakuwa sawa"
Mtandao huu utaendelea kufuatilia zaidi kujua kama waliopewa zawadi hewa watalipwa jumamosi ama ndio funika kombe ......!!!?
No comments:
Post a Comment