Tuesday, April 2, 2013

SIRI YAFICHUKA MAUAJI YA LUMUMBA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhXA1shyolBFfGXuKjBkJqnz_cSUlcrPP14M4aA5PF8PNpp5TYJzNQhxUAEV5xEPfnuxHjnOTaVpNJD6FJRjnA833x1gZrIcu1BREoXwZIq1BEUbopmBANX05ZUZVyREQyMo2PMEPteYdA/s1600/lumumbaprint.jpg


Mbunge mmoja wa Uingereza amefichua kuwa Shirika la Kijasusi la Uingereza MI6 lilihusika katika mauaji ya Patrice Lumumba, waziri mkuu wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia Kongo.
Lord David Edward Lea amefichua ukweli huo katika barua aliyoandikia jarida la London Review of Books toleo la Machi 21.


Edward Lea ambaye ni mjumbe katika Baraza la Malodi (House of Lords) amesema alidokezewa hayo na Daphne Park ambaye alikuwa jasusi na balozi mdogo huko mjini Leopoldville ambao sasa unajulikana kama Kinshasa kuanzia mwaka 1959 hadi 1961. Amesema mwanadiplomasia huyo ambaye tayari ameshaaga dunia alimfahamisha kinaga ubaga kuwa yeye binafsi alihusika katika mpango wote wa kumuua Lumumba. Lord Lea ameongeza kuwa Bi. Park alimfahamisha kuwa sababu ya kuuawa Lumumba ni kuwa alikuwa mwanasiasa wa mrengo wa kushoto aliyekuwa tayari kuipa Russia utajiri wa Kongo hasa madini ya almasi na urani katika eneo la Katanga. Ikumbukwe kuwa Lumumba aliongoza mapambano ya kupigania uhuru wa Kongo kutoka mkoloni mbelgiji. Baada ya nchi hiyo kupata uhuru Juni mwaka 1960, Lumumba alichaguliwa kuwa waziri mkuu. Serikali yake ilipinduliwa miezi mitatu baadaye katika njama iliyopangwa na nchi za Magharibi hasa Uingereza na Marekani na kisha akapigwa risasi na kuuawa Januari 17 196


No comments:

Post a Comment