Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke, mkazi wa kitongoji
cha Chemka ,Kata ya Chanji Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa
amejikuta akipata uchungu wa ghafla na kujifungua mtoto wa kiume
chooni, nyumbani kwake kutokana na mshtuko alioupata baada ya
kutolewa kwa nguvu katika nyumba hiyo na dalali wa mahakama.
Katika tukio hilo ambalo mwanamke huyo (jina
linahifadhiwa) alipata mshtuko mkubwa baada ya dalali wa mahakama
kufika nyumbani kwake na kuanza kutoa nje vyombo vyake vyote kwa
madai kuwa nyumba hiyo ilikuwa na mgogoro.
Kwa mujibu wa mwanamke huyo baada ya dalali
kuwatoa kwa nguvu katika nyumba hiyo kwa kutoa nyombo vyao vyote
nje na kufunga nyumba hiyo kwa makufuli baada ya kuhaha na
kukosa sehemu ya kuhifadhi vyombo hivyo yeye na familia yake
walilazimika kulala nje ya nyumba hiyo na kunyeshewa na mvua usiku
kucha.
Alisema baada ya kutaabika usiku kucha kwa
kunyeshewa na mvua ilipofika saa tano asubuhi alibanwa na uchungu
mkali alipolazimika kukimbilia chooni na kujifungua mtoto wa kiume
akiwa hai.
No comments:
Post a Comment