NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nassib Abdul ‘Diamond’,
ameitaka serikali kutowasahau wasanii na kuwakumbuka wakati wa kampeni.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Diamond
alisema viongozi wa Tanzania wanashindwa kutambua umuhimu wa wasanii
nchini kipindi wawapo madarakani.
“Viongozi wetu wa Tanzania wanashindwa kutambua umuhimu wa wasanii kwa
kushindwa kutambua mchango wao na kusubiri mpaka kipindi cha kampeni
ndipo wanaona umuhimu wetu,” alisema Diamond.
Alisema wamekuwa wakitoa malalamiko mengi kwa serikali, lakini hakuna kinachofanyika, badala yake wamekuwa wakitelekezwa.
“Serikali inatukumbatia tu kwa muda mfupi na kututumia wasanii kwenye
kampeni zao kwa masilahi yao binafsi, kisha wanatuacha bila kujali
thamani na mchango wetu kwao,” alisema.
No comments:
Post a Comment